Wednesday, August 07, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Visababishi vya migogoro

Ndugu,
Hongera kwa kuendelea kufatria makala za morning motivation diary.Hakika unazidi kunifanya kujitahidi zaidi na zaidi kukupatia kilicho bora na kuing'alisha asubuhi yako.
 Fedha imekuwa ikichangia kuwepo kwa migogoro kama tulivyoona kwenye Usaliti,majivuno, kukurupuka na wivu:

=•Fedha
Naweza sema fedha ni njia ya  mabadilishano ya thamani  ambayo ipo katika mfumo wa noti na sarafu .
Kabla ya ujio wa fedha mabadilishano yalikuwa kwa njia ya thamani kwa thamani,mfano mahindi kwa maharage au mbuzi n.k Ila ujio wa fedha umerahisisha zaidi mabadilishano hayo  badala ya mahindi unayauza na kupata fedha unamfata mtu mwenye mbuzi anayetaka fedha unampatia.

Ukuaji wa sayansi na teknolojia umesababisha urahisi fulani katika uthibiti wa matumizi ya fedha.Kwa maana ya kutembea na fedha nyingi kila wakati badala yake inakuwa benki au kwenye mitandao mbalimbali unatembea na kiasi kidogo kinachotosha kulingana na matumizi uliyoyapanga.
Kwa hali ya sasa sio rahisi kumtambua mtu pindi akiwa na fedha au la! Kama ilivyokuwa zamani kutembea na kiasi kingi cha fedha.
Fedha inahitajika kutumika katika mahitaji kwa familia,ndugu,jamaa na majirani.Katika jamii au sehemu fulani ni dhahili kuna mtu  anayetegemewa kwenye kutoa msaada au kuwasaidia wengine kifedha .Watu wakigundua mtu huyo muda fulani ana fedha hutumia njia mbadala kuhakikisha anawapatia fedha kulingana na mahitaji yao.

Lakini natambua watu wengi wanakuwa na bajeti kuendana na kipato wanachopata kitu ambacho sio rahisi mtu wa nje kukitambua.
Hali kama hio ya kuombwa fedha na watu wengi kwa wakati mmoja,Mhusika akibanwana au akiwa hana kwa huo muda hapo ndipo maneno na migogoro inapoanza Mara Fulani mbahiri,mchawi ana roho mbaya ukimuomba fedha hakupi mbona Jana kanunua kitu fulani, Yaani wanasema kila maneno.
Watu wakishagundua mtu fulani ana fedha na wakishaanza kumtegemea wanaamini hawezi kuishiwa lakini wanashindwa kujua kwamba hata siku hazifanani sio muda wote mtu anakuwa na fedha.

Swala la fedha kusababisha migogoro unalionaje katika jamii uliyopo? Naomba maoni yako ntashukuru.Wish you all the best.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".
Unaweza kuwasiliana na Mimi 0767702659
Kupata makala zaidi tembelea page ya Instagram lackius Robert
Karibu.

No comments:

Post a Comment