Monday, August 05, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Visababishi vya migogoro:

Ndugu,
Ni kweli kwamba kuna wakati tumekuwa tunafanya matendo ambayo yanasababisha kuibuka kwa migogoro pasipo kujua kama vile:

=•Majivuno
Hulka ya mtu kujiona yuko juu na anastahili yeye kuabudiwa na kusikilizwa tu.Inapotokea watu wanalingana nae hutaka yeye tu aonekane wengine wasionekane.
Hali ya majivuno pia imechangia uwepo wa migogoro baina ya mhusika na waliomzunguka.

 Mfano majivuno katika maofisini ambapo mfanyakazi fulani akiwa na gari pesa nyingi ambao hawana wanaona cha moto.Pia kwenye vikundi vidogo vidogo mfano VICOBA yeye anataka kila kitu aguse kila mada akazie yeye tu wengine wasikazie zaidi.Wakati huo ajui kwamba wengine anawakela kwahali hiyo mgogoro unatokea na unasababisha watu kumtenga na pengine kutotaka kumsalimia na vitu kama hivyo.Pengine hajui kama kuna mgogoro unaendelea baina yake na wenzake,kisa majivuno yake.

=•Kukurupuka/Kufanya kitu pasipo kufikiria zaidi.
Hii husababishwa Mara nyingi  habari za kusikia kutoka kwa mtu fulani na kuamini pasipo kutafuta ukweli wa jambo.
Kitaalamu tunasema (Hearsay) habari za kuambiwa ambayo zinaweza kusababishwa na mambo mengi juu ya maisha yetu.Mmojawapo anaambiwa kitu bila ya kukitafakari zaidi anachukua hatua mwisho wa siku anajikuta anakosea kinachotokea mgogoro.Mfano anaambiwa ,"nimesikia jirani anasema we mwizi " ndio maana siku hizi unaonekana mara chache chache au umefanikiwa haraka. Unasema mh !! Mimi mwizi!!! Oh!! Atanikoma leo. Baadala ya kuwa mwelewa wa kutumia busara unaenda unaanaanza kumfokea kumbe hakuwa anamanisha wewe labda na yeye alisikia tu kutoka kwa wengine wenye wivu na mafanikio yako ,mgogoro kati yako na jirani unaanza.Chukua hatua ,Fikiri kabla ya kutenda,Wish you all the best let's meet on the next discussion.

" Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".
Unaweza kuwasiliana na Mimi kupitia 0767702659
Kupata makala zaidi tembelea page yangu ya Instagram Lackius Robert
Karibu.

No comments:

Post a Comment