Saturday, August 17, 2019

Vijue vichocheo vya mgogoro ili uishinde migogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Vichocheo vya migogoro:

Ndugu,
Ni siku nyingine tena tunakutana katika morning motivation diary yenye lengo kubwa kuongezea maarifa na kuing'alisha siku yako.
Karibu katika mwendelezo wa vichocheo vya migogoro:

Ubaguzi (Descrimination) Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakibaguliwa miongoni mwa sehemu za kazi kutokana hali fulani fulani.
Ukiangalia sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu kidogo cha 7 inakataza ubaguzi wa aina yoyote katika sehemu za kazi iwe rangi,ugonjwa ,dini,kabila,.
Hivyo katika sehemu ya kazi ikitokea mtu kubaguliwa mgogoro mkubwa unaibuka kwa sababu ,inaonesha thamani yake aionekani ,pia mchango wake hauonekani kuthaminiwa.Binadamu sote ni sawa tukiondoa tofauti zetu za kikabila kidini.

Matarajio usiyoyatarajia (unrealistic expectations).
,Hali huchochea  migogoro zaidi hasa pale ambapo mmojawapo anapokuwa anatarajia kupata kitu Fulani.Mfano Mshahara labda mwisho wa mwezi ikatokea hajaupata hivyo siku zimeongezwa mbele. Labda ameongeza elimu akitarajia kupandishwa cheo(promotion) na kuongezeka kwa bonus lakini hivyo vyote vikawa havijatendeka.Matarajio yake yanakuwa tofauti na alivyoyanga hivyo usababisha kuongezeka kwa mgogoro kati yake na wshusika ofisini.Inaweza kusababisha presenteism yani mfanyakazi yupo kama hayupo kazini.

Mawasiliano hafifu,
Ili kazi iweze kufanikiwa zaidi inahitaji uwepo wa ushikiriano mzuri unaoambatana na mawasiliano mazuri.
Maana kila mmoja atatimiza wajibu wake ikiwemo kuhudhulia mikutano husika ikihitajika,kubadilisha mawazo na mambo mengine ili kazi ziweze kwenda zaidi.
Mawasiliano yanategemea sana maneno inabidi kuhakikishia kuwa mawasiliano yako yanaenda zaidi ya maneno.Ikiwa unazungumza na mtu mmoja au zaidi tambua maneno pia matendo yanaweza kuathiri uhusiano wako pamoja na ukweli utakaoutoa kutumia maneno sahihi na hisia sahihi, wakati wa kuzungumza na mtu.

Pindi mawasiliano yakosapo kuna baadhi ya kazi hazifanyiki kwa wakati kitu kinachopelekea mgogoro kuibuka.

Kukosekana uaminifu ,Kuna usemi unaosema uaminifu ni mtaji.Hivyo katika sehemu za kazi ata ili ufanisi uongezeke uaminifu inabidi uwepo.Kwa maana ya kwamba mfanyakazi anaweza achiwa kazi zingine kama anaaminiwa akazimalizia bila ofu.

Lakini kama uaminifu aupo miongoni mwa wafanyakazi hali hii husababisha baadhi kukosa fursa,au kutopewa kazi badala yake wanapewa waaminifu.Hali hii huibua mgongano mkubwa kwanini wengine wanaachiwa au kupewa kazi ama pengine kupandishwa vyeo na wengine hawapandishwi. Je hali ikoje katika sehemu unayofanyia kazi?. Wish you all the best let's meet on the next discussion.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert

Wednesday, August 14, 2019

Vijue vichocheo vya mgogoro ili kuepuka mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Vichocheo vya migogoro:

Ndugu,
Inawezakana katika sehemu ya kazi migogoro isiwepo lakini ni  nadra sana kutoka na asili ya migogoro.
Tunasema migogoro ni "HISIA ZILIZOLALA" ukiziamsha zinaamka.
Karibu tuangalie vichocheo vya migogoro:

Migogoro binafsi
Wapo wafanyakazi wengine  huruhusu  migogoro  yao  binafsi, ambayo  haihusiani ,kuharibu kazi zao.Labda Unakuta mfanyakazi Fulani na fulani wana  mgogoro  wa  kinafsia  ambao unahamishwa  kwa  wafanyakazi wengine na  kusababisha  kutoelewana.  Akitokea mtu  anataka kuwakosoa au  kuwashauri waache hiyo migongano wanakataa kuongea  naye.  Na wakiongea wanaongea kwa ukali  na  matusi hali hiyo inachochea mno usambaaji wa  Mgogoro katika sehemu za kazi .Migogoro hio mara nyingi hutokana na wivu wa maendeleo yaani mtu fulani hataki fulani afanikiwe,Akiona ana maendeleo fulani nafsi inamuuma, kama ni mfanyakazi mwenzie anaanza chokochoko ndogo ndogo baadae mgongano kamili.

Kutomsikiliza mtu (Not hearing not listening).Watafiti wanasema watu wengi wamekuwa wakichochea migogoro bila kujua ,kutokana na kutotoa nafasi ya mtu kujielezea.
Kusheria tunasema kila mtu ana haki ya kusikilizwa" right to be heard" ambayo inampa mtu uhuru kujielezea. Wakati mwingine mtu amechelewa kazini au nyumbani kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake ila akifika unamfokea uku ukimwambia maneno makali na magumu.Akitoka hapo anaona thamani yake aieshimiwi mgogoro tayali unakuwa katika hatamu.
Nakusihi usikose makala ijayo ,wish you all the best.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"
Unaweza kuwasiliana na mimi 0767702659
Au katika page yangu Instagram Lackius Robert.
Karibu

Tuesday, August 13, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

 Jinsi kazi(Workplace conflict) inavyoathiri falimia.

Ndugu,
Kama ilivyo kwenye familia kwamba familia ikiyumba na kazini panayumba pia.
Ndivyo ilivyo kazini na kwenye familia pia panayumba:
Karibu tuone jinsi kazi inavyoleta migogoro katika familia:

Kama mshahara ni mdogo (Insufficient wage),Mfanyakazi anafanya kazi ili apate kipato cha kuisaidia familia kama kipato ni kidogo,alafu anafanya masaa mengi kwa long working hours.Hali hii usababisha migogoro kwa sababu familia itashindwa kumuelewa muhusika kwa kutotoa baadhi ya mahitaji.

Mikutano isiyotarajiwa(unexpected meeting) mfano muda wa kazi unaisha hivi pa! Unaambiwa kuna kikao mnakaa kwa muda kadhaa.Hivyo nyumbani ukitoa taarifa unaambiwa umeanza njia ya pembeni kelele zinaanza mkishindwa kuelewana mapigano kususiana.

Safari nyingi extensive travel hizi pia husababisha mgogoro kwa sababu mmoja wapo anaweza hisi kuna namna fulani.Katika kazi kama ni mwanaume unaweza hisiwa kuwa na nyumba ndogo mkishindwa kuelewana mgogoro tayali unaanza.

Pia vyote hivi husababisha kukosa muda mzuri kwa mazazi  kuzungumza na watoto, mzazi anaondoka usiku anarudi usiku wikend anaudhulia vikao hali inayopelekea watoto kutopata malezi bora kutoka kwa wazazi wote.
Wish you all the best let's meet on the next discussion.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Unaweza kuwasiliana na Mimi 0767702659
Au ukatembelea page yangu ya Instagram lackius Robert
Karibu.

Monday, August 12, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Hivi ndivyo migogoro ya familia inavyoleta athari katika sehemu za kazi.

Ndugu,
Karibu katika siku nyingine tena katika program ya morning motivation diary yenye lengo la kuing'alisha siku yako.

Ni wazi kwamba kila mfanyakazi anatokea kwenye familia,Yaani anatoka nyumbani anaenda kazini hivyo nyumbani kukiwa na amani pia kazini patakuwa na amani.
Chunguza mifano hii katika familia kama uchumi umeyumba mmoja wapo labda mwanaume akauza kitu au Mali bila kutoa taarifa kwa mkewe pindi kile kitu au mali ikija kuchukuliwa mwanamke atokuwa na amani na mgogoro utaanza ,pindi akienda kazini atakama anafanya kazi baadae atakuwa na mawazo maana nyumbani mambo apako sawa.

 Mmojawapo amezaa nje ya ndoa hali itakayoanzishwa hapo ni balaa kelele zitakuwa nyingi sana hadi kufikia hatua ya kupigana katika kupigana kwa bahati mbaya mmoja akiumia kinachofuata ni kwenda hospitali kitu kinachopelekea kutoudhulia kazini sababu ni malumbano na mapigano.

Talaka wawili walikuwa wanapendana pindi wanapotalakiana inachachukua siku zisizopungua angalau 14 ili kuona umeanza kupata unafuu kidogo wa mawazo  pia na kuzoea hio hali ,kipindi chote hicho kinakuwa kinaathili utendaji wa kazi maana mfanyakazi anakuwa yupo kazini  kama hayupo (presenteeism) badala ya kufanya kazi anawaza namna ya kurejesha furaha au amani kwenye moyo wake.

Nikumbushe tena mfanya kazi anatoka kwenye familia hivyo ni wachache wanaoweza kuhimili hekaheka hizo.Familia ikiyumba kazini pia panayumba maana kuna uhusiano mkubwa kati ya familia na kazini .
Kama una maoni au ushauri kuhusu makala hizi  naomba unijulishe. Wish you all the best let's meet on the next discussion.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kupata makala zilizopita bonyeza hapa
https://www.instagram.com/p/B0kJTHfFJNt/?igshid=17zwddxlmeig5

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Hivi ndivyo migogoro ya familia inavyoleta athari katika sehemu za kazi.

Ndugu,
Karibu katika siku nyingine tena katika program ya morning motivation diary yenye lengo la kuing'alisha siku yako.

Ni wazi kwamba kila mfanyakazi anatokea kwenye familia,Yaani anatoka nyumbani anaenda kazini hivyo nyumbani kukiwa na amani pia kazini patakuwa na amani.
Chunguza mifano hii katika familia kama uchumi umeyumba mmoja wapo labda mwanaume akauza kitu au Mali bila kutoa taarifa kwa mkewe pindi kile kitu au mali ikija kuchukuliwa mwanamke atokuwa na amani na mgogoro utaanza ,pindi akienda kazini atakama anafanya kazi baadae atakuwa na mawazo maana nyumbani mambo apako sawa.

 Mmojawapo amezaa nje ya ndoa hali itakayoanzishwa hapo ni balaa kelele zitakuwa nyingi sana hadi kufikia hatua ya kupigana katika kupigana kwa bahati mbaya mmoja akiumia kinachofuata ni kwenda hospitali kitu kinachopelekea kutoudhulia kazini sababu ni malumbano na mapigano.

Talaka wawili walikuwa wanapendana pindi wanapotalakiana inachachukua siku zisizopungua angalau 14 ili kuona umeanza kupata unafuu kidogo wa mawazo  pia na kuzoea hio hali ,kipindi chote hicho kinakuwa kinaathili utendaji wa kazi maana mfanyakazi anakuwa yupo kazini  kama hayupo (presenteeism) badala ya kufanya kazi anawaza namna ya kurejesha furaha au amani kwenye moyo wake.

Nikumbushe tena mfanya kazi anatoka kwenye familia hivyo ni wachache wanaoweza kuhimili hekaheka hizo.Familia ikiyumba kazini pia panayumba maana kuna uhusiano mkubwa kati ya familia na kazini .
Kama una maoni au ushauri kuhusu makala hizi  naomba unijulishe. Wish you all the best let's meet on the next discussion.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kupata makala zilizopita bonyeza hapa
https://www.instagram.com/p/B0kJTHfFJNt/?igshid=17zwddxlmeig5

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Hivi ndivyo migogoro ya familia inavyoleta athari katika sehemu za kazi.

Ndugu,
Karibu katika siku nyingine tena katika program ya morning motivation diary yenye lengo la kuing'alisha siku yako.

Ni wazi kwamba kila mfanyakazi anatokea kwenye familia,Yaani anatoka nyumbani anaenda kazini hivyo nyumbani kukiwa na amani pia kazini patakuwa na amani.
Chunguza mifano hii katika familia kama uchumi umeyumba mmoja wapo labda mwanaume akauza kitu au Mali bila kutoa taarifa kwa mkewe pindi kile kitu au mali ikija kuchukuliwa mwanamke atokuwa na amani na mgogoro utaanza ,pindi akienda kazini atakama anafanya kazi baadae atakuwa na mawazo maana nyumbani mambo apako sawa.

 Mmojawapo amezaa nje ya ndoa hali itakayoanzishwa hapo ni balaa kelele zitakuwa nyingi sana hadi kufikia hatua ya kupigana katika kupigana kwa bahati mbaya mmoja akiumia kinachofuata ni kwenda hospitali kitu kinachopelekea kutoudhulia kazini sababu ni malumbano na mapigano.

Talaka wawili walikuwa wanapendana pindi wanapotalakiana inachachukua siku zisizopungua angalau 14 ili kuona umeanza kupata unafuu kidogo wa mawazo  pia na kuzoea hio hali ,kipindi chote hicho kinakuwa kinaathili utendaji wa kazi maana mfanyakazi anakuwa yupo kazini  kama hayupo (presenteeism) badala ya kufanya kazi anawaza namna ya kurejesha furaha au amani kwenye moyo wake.

Nikumbushe tena mfanya kazi anatoka kwenye familia hivyo ni wachache wanaoweza kuhimili hekaheka hizo.Familia ikiyumba kazini pia panayumba maana kuna uhusiano mkubwa kati ya familia na kazini .
Kama una maoni au ushauri kuhusu makala hizi  naomba unijulishe. Wish you all the best let's meet on the next discussion.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kupata makala zilizopita bonyeza hapa
https://www.instagram.com/p/B0kJTHfFJNt/?igshid=17zwddxlmeig5

Sunday, August 11, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Migogoro katika sehemu za kazi
(Workplace conflicts)

Ndugu,
Karibu katika mwendelezo kuhusu migogoro sehemu katika sehemu za kazi,sehemu iliyopita tumeangalia migogoro ya katika familia:

Sehemu za kazi panaweza kuwa kiwandani,Shuleni,Ofisini,Kwenye taasisi ambapo panausisha wafanyakazi kwa maana ya waajiri na waajiriwa.Sehemu za kazi zimegawanyika katika makundi mawili Serikalini (public) na Binafsi (private).
MWAJIRI anaweza kuwa Serikali au mtu binafsi.

Migogoro kazini :
Hii ni migogoro inayotokea baina ya waajiri (employers) na waajiriwa (employees) baada ya kutofautiana katika maslai (interests) au mahitaji.
Katika sehemu yoyote ya kazi mwajiri unaweza muita Bosi anataka uzalishaji mzuri pamoja kama ni kiwanda cha nguo au viatu yeye anataka kila siku watengeneze pair nyingi sana kuliko kawaida,Kama ni shule wanafunzi wote wafaulu kwa kiwango cha juu,pia kubalance mshahara (profit maximization).

Upande wa mfanyakazi yeye anataka mshahara mzuri mazingira mazuri ya kufanyia kazi ikiwemo uwepo wa pangaboi(feni) au Air Condition AC,Viti,meza ,Taraklishi (Computer ),usafiri,maji safi na salama, na huduma ya afya na usalama (safety and health).Lakini mahitaji haya yote yanategemea vigezo na mashariti vilivyowekwa kwenye mkataba (Terms and Conditions according to contract of employment).

Vitu hivi visipopatikana au kukitokea utofauti au hali ya kutoelewana hapo ndipo mgogoro huibuka.
Huku dalili zake ni kama kutosalimia baina ya wafanyakazi na Bosi wao ,yaani Bosi akija mfanyakazi anatafuta mlango wa kupitia ili asikutane nae.Au bosi akiwa anamtazama mfanyakazi fulani anajisikia vibaya maana uhasama unakuwa ni mkubwa sana.
Naomba niishie hapo ,Wish you all the best let's meet on the next discussion.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kupata makala zilizopita bonyeza hapa
https://www.instagram.com/p/B0hlaRzFRYU/?igshid=1jka3jel8u4nv au wasaliana nami 0767702659 Lackius Robert.
Karibu

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Overview kuhusu migogoro

Ndugu,
Migogoro kama tulivyoona Kwenye makala iliyopita kuwa ni uwepo wa uhasama,kutoelewana au kutofatiana kinawazo au kimahitaji baina ya mtu mmoja au zaidi.Zipo aina mbali mbali za migogoro ,ikiwemo migogoro binafsi(intrapersonal conflict)mtu na mtu (interpersonal conflict),Familia(family conflict) ,Nchi na nchi kwa upande wa  kiuchumi,kisiasa kijamii na  kiutamaduni.
Lakini pia kuna migogoro sehemu za kazi(Workplace/Organization conflict).

Licha ya kuwepo aina nyingi za migogoro lakini napenda kuelezea tu Kwenye migogoro ya kifamila (family conflict )na migogoro kazi(workplace conflicts).

Nianze na migogoro ya kifamilia(Family conflicts):
Hii ni migogoro inayokea kutokana na uwepo wa mivutano kati ya wanafamilia baba,mama pia watoto au ndugu.
Taaaisi ya The Better Health Channel ya Australia 2019 baada kufanya utafiti kutokanana watu inaowahudumia wanasema wakati mwingine mgogoro hutokea kutokana na uwepo wa kutoelewana baina yao na kurukia hitimisho ambayo siyo nzuri yaani wrong conlusion.Kwa maana ya kwamba wabashindwa kuelewana hivyo hukimbilia hitimsho lisilo sahihi hali ambayo upelekea mgongano kuendelea.

Utafiti unaonesha migogoro ni kitu cha asili kipo,hivyo ni  sehemu ya maisha hata kwa mtu mmoja na familia pia maana familia inaundwa na watu. Hivyo isipotatuliwa kwa amani na itaendelea kuwa inatokea tokea.
Mfano unapokuwa njiani unatembea pindi ukijikwaa bila kujua taarifa zinaenda haraka kwenye ubongo ,kuna hali fulani ya maumivu unayasikia na unachukua dakika kadhaa kurejea katika hali yako ya kawaida.Hivyo ndivyo ilivyo wakati mgogoro umepamba moto
.Ndiyo maana kuharibu mahusiano kwa Sababu mmoja wapo hushindwa kuthibiti hisia zake na kuanza kulumbana na pengine kupigana.Baadhi ya visababishi kwenye familia ni kupeleka watoto shule,Kuzaa mtoto mwingine mfano nje ya ndoa,Kazi za Masafa marefu,magonjwa.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kupata makala zilizopita tembelea ukurasa wangu wa Instagram Lackius Robert au wasiliana nami 0767702659

Friday, August 09, 2019

Usipite njia ya mkato

MORNING MOTIVATION DIARY

Usipite njia ya mkato

Ndugu,
Karibu katika siku nyingine tena ambapo tunakuatana katika program ya morning motivation diary ,yenye lengo kubwa la kukuongezea maarifa na kuing'alisha siku yako

Katika ulimwengu huu ukitaka  mafanikio ,haupaswi kupita njia ya mkato ili kuyafikia mafanikio hayo.Licha ya kwamba kuna usemi unaoitwa ukitaka kujua njia ya mkato kula nauli.

Unapokuwa na haraka, utafanikiwa ndio lakini mara nyingi ,Njia za mkato huwa na madhara, hasa unapokatisha kwenye ubora wa kile unachofanya.Kwa sababu unakuwa hauna maandalizi mazuri ikiwemo ujuzi,maarifa,changamoto n.k.Kwa kupitia njia sahihi zitachukua muda  kukamilisha jambo lakini ndo ukweli.Ukishakamilisha autahitaji gharama kubwa ikiwemo nguvu n.k

Tuwematazama ndugu ,marafiki wenzetu waliotaka kufanikiwa haraka walivyojiingiza katika matendo mabaya ikiwemo wizi,Uuzaji wa madawa ya kulevya ,Utekaji,ukahaba n.k pia yaliyowakuta baadhi tumeyaona.Malengo yao makubwa ni kutaka kufanikiwa haraka na kwa kipindi kifupi.
Tukumbuke hata mbuyu ulianza kama mchicha,ukiutazama umbo lake ukubwani uwezi amini kama umetokea kwenye umbo dogo.Hivyo mafanikio ya kweli na mazuri ni yale yenye maandalizi muda mzuri wa kutafakari,kujipanga na  kupitia njia sahihi za kuaminika.Jifunze ,elimika,Fanya kazi kwa bidii,usiubanie uwezo wako mafanikio ya kweli utayapata katika njia ya kweli.Wish you all the best.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa maelezo zaidi 0767702659
Kwa makala zaidi tembelea page yangu ya Instagram Lackius Robert
Karibu.

Thursday, August 08, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Visababishi vya migogoro.

Ndugu,
Karibu katika mwendelezo wa makala hii inayozungumzia migogoro katika jamii tunazoishi.

=•Matarajio makubwa, pia suala lingine ambalo husababisha kutoelewana na migogoro mikubwa sana kuibuka  ni kuwa na matarajio makubwa sana endapo hayo matarajio yasipo kamilika migogoro hutokea.Mfano wakulima wanalima mazao wakitarajia mvua inyeshe ili mazao yawe mengi mwishoni mwa mavuno lakini hali inapokuwa ndivyo sivyo.Huanza kulalamika na kuongea mengi huku wakiwa wanaofia baadhi ya watu kwa kuwasingizia wao ndo wanaosababisha mvua isinyeshe au mazao yasitoke mengi..Hivyo migogoro ndipo huanza baina yao na wanajamii.

Wanafunzi huanza shule wakiwa na matarajio makubwa ya kumaliza masomo yao na kupata ajira .Hali inapokuwa tofauti migogoro kati yao na serikali wakati mwingine huwalamu wazazi wao au jamaa zao waliowatarajia kutoa assistance katika kuwapatia ajira.

 =••Dhuluma,Hi na yenyewe pia insababisha mgogoro katika sehemu,au kazi tunazofanya.

Katoka point hii nimekusanya Maoni kutoka kwa baadhi ya watu wamesema hivi:

[7/26, 06:23] ,Wachache wenye busara ndio wanaweza vumilia dhuluma wanazofanyiwa bila kuingia kwenye mgogoro na mdhulumu wake.

[7/26, 06:21], Ni kweli bro, dhuluma humfanya mtu ajenge chuki na mwenzie, ata kama walikuwa na mahusiano mazuri yataisha, matokeo yake wanakuwa kama adui, wakikutana,Na hapo mgogoro unakuwa mkubwa mno.Hali hii imekuwa mara nyingi inatokea kwa wenye fedha nyingi na wenye fedha kidogo.Ambapo wenye fedha nyingi uchukulia matatizo ya wenye fedha kidogo kwa kuwadhulumu badala ya kuwapa huduma inayostahili anawapa kidogo maana wanakuwa hawana namna.Je hapo ulipo hali ipoje ? Naomba maoni yako,Wish you all the best.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".
Unaweza kuwasiliana na Mimi 0767702659
Kupata makala zaidi tembelea page yangu ya Instagram lackius Robert
Karibu.

Wednesday, August 07, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Visababishi vya migogoro

Ndugu,
Hongera kwa kuendelea kufatria makala za morning motivation diary.Hakika unazidi kunifanya kujitahidi zaidi na zaidi kukupatia kilicho bora na kuing'alisha asubuhi yako.
 Fedha imekuwa ikichangia kuwepo kwa migogoro kama tulivyoona kwenye Usaliti,majivuno, kukurupuka na wivu:

=•Fedha
Naweza sema fedha ni njia ya  mabadilishano ya thamani  ambayo ipo katika mfumo wa noti na sarafu .
Kabla ya ujio wa fedha mabadilishano yalikuwa kwa njia ya thamani kwa thamani,mfano mahindi kwa maharage au mbuzi n.k Ila ujio wa fedha umerahisisha zaidi mabadilishano hayo  badala ya mahindi unayauza na kupata fedha unamfata mtu mwenye mbuzi anayetaka fedha unampatia.

Ukuaji wa sayansi na teknolojia umesababisha urahisi fulani katika uthibiti wa matumizi ya fedha.Kwa maana ya kutembea na fedha nyingi kila wakati badala yake inakuwa benki au kwenye mitandao mbalimbali unatembea na kiasi kidogo kinachotosha kulingana na matumizi uliyoyapanga.
Kwa hali ya sasa sio rahisi kumtambua mtu pindi akiwa na fedha au la! Kama ilivyokuwa zamani kutembea na kiasi kingi cha fedha.
Fedha inahitajika kutumika katika mahitaji kwa familia,ndugu,jamaa na majirani.Katika jamii au sehemu fulani ni dhahili kuna mtu  anayetegemewa kwenye kutoa msaada au kuwasaidia wengine kifedha .Watu wakigundua mtu huyo muda fulani ana fedha hutumia njia mbadala kuhakikisha anawapatia fedha kulingana na mahitaji yao.

Lakini natambua watu wengi wanakuwa na bajeti kuendana na kipato wanachopata kitu ambacho sio rahisi mtu wa nje kukitambua.
Hali kama hio ya kuombwa fedha na watu wengi kwa wakati mmoja,Mhusika akibanwana au akiwa hana kwa huo muda hapo ndipo maneno na migogoro inapoanza Mara Fulani mbahiri,mchawi ana roho mbaya ukimuomba fedha hakupi mbona Jana kanunua kitu fulani, Yaani wanasema kila maneno.
Watu wakishagundua mtu fulani ana fedha na wakishaanza kumtegemea wanaamini hawezi kuishiwa lakini wanashindwa kujua kwamba hata siku hazifanani sio muda wote mtu anakuwa na fedha.

Swala la fedha kusababisha migogoro unalionaje katika jamii uliyopo? Naomba maoni yako ntashukuru.Wish you all the best.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".
Unaweza kuwasiliana na Mimi 0767702659
Kupata makala zaidi tembelea page ya Instagram lackius Robert
Karibu.

Tuesday, August 06, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Visababishi vya migogoro

Ndugu,
Karibu katika mwendelezo unaoelezea visababishi vya migogoro katika sehemu tunazoishi au tunakofanyia kazi zetu:

=•Ubinafsi(Selfishness)
Hali ya mtu kujipenda mwenyewe pasipo kuwajali wengine.Licha ya kwamba tunasema jipende kwanza jisifie kama wakishindwa kukusifu lakini ni vema kuwapa nafasi wengine.

Kitendo cha kuweka mahitaji yake mbele,Kutosikiliza maoni ya watu wengine.Mtu mbinafsi anataka kudhibiti kila kitu kinachotokea katika maisha ,kazini au popote anapokuwa. hivyo, hafikirii mawazo ya wengine kama ni bora zaidi badala yake huona ya kwake ndio bora wakati wote. Kutokana na hali hiyo hali ya mawasiliano na wenzake inatokea iwe ofisini,kanisani ,shuleni kwenye mikutano mbali mbali kitu ambacho baadae kinaleta mgogoro mkubwa.

=•Usaliti,
Usaliti ni ukiukwaji mkubwa wa makubaliano baina na ya mtu mmoja au kikundi.Upo katika mahusiano baina ya wawili,kwenye familia,kazini, kwenye vikundi kama SACCOS ,VICOBA .Usaliti unaleta maumivu makubwa na huathiri malengo na mipango ya watu.
Uchungu wa kusalitiwa mara nyingi hutokea pale msaliti ukimtazama mbele na hapo ndipo utata unapoanza na kupelekea kukata kwa mawasiliano.Kwa wengi, maumivu ya usaliti ni mbaya zaidi kuliko ukatili wa kimwili, udanganyifu, au chuki.
Usaliti huharibu msingi wa uaminifu kwa kiasi kikubwa mwishowe upelekea migogoro. Chukua hatua acha ,fikiria kabla ya kutenda wape nafasi wengine.Wish you all the best let's meet on the next discussion.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Wasiliana namimi 0767702659
Kupata makala zaidi Instagram Lackius Robert

Monday, August 05, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Visababishi vya migogoro:

Ndugu,
Ni kweli kwamba kuna wakati tumekuwa tunafanya matendo ambayo yanasababisha kuibuka kwa migogoro pasipo kujua kama vile:

=•Majivuno
Hulka ya mtu kujiona yuko juu na anastahili yeye kuabudiwa na kusikilizwa tu.Inapotokea watu wanalingana nae hutaka yeye tu aonekane wengine wasionekane.
Hali ya majivuno pia imechangia uwepo wa migogoro baina ya mhusika na waliomzunguka.

 Mfano majivuno katika maofisini ambapo mfanyakazi fulani akiwa na gari pesa nyingi ambao hawana wanaona cha moto.Pia kwenye vikundi vidogo vidogo mfano VICOBA yeye anataka kila kitu aguse kila mada akazie yeye tu wengine wasikazie zaidi.Wakati huo ajui kwamba wengine anawakela kwahali hiyo mgogoro unatokea na unasababisha watu kumtenga na pengine kutotaka kumsalimia na vitu kama hivyo.Pengine hajui kama kuna mgogoro unaendelea baina yake na wenzake,kisa majivuno yake.

=•Kukurupuka/Kufanya kitu pasipo kufikiria zaidi.
Hii husababishwa Mara nyingi  habari za kusikia kutoka kwa mtu fulani na kuamini pasipo kutafuta ukweli wa jambo.
Kitaalamu tunasema (Hearsay) habari za kuambiwa ambayo zinaweza kusababishwa na mambo mengi juu ya maisha yetu.Mmojawapo anaambiwa kitu bila ya kukitafakari zaidi anachukua hatua mwisho wa siku anajikuta anakosea kinachotokea mgogoro.Mfano anaambiwa ,"nimesikia jirani anasema we mwizi " ndio maana siku hizi unaonekana mara chache chache au umefanikiwa haraka. Unasema mh !! Mimi mwizi!!! Oh!! Atanikoma leo. Baadala ya kuwa mwelewa wa kutumia busara unaenda unaanaanza kumfokea kumbe hakuwa anamanisha wewe labda na yeye alisikia tu kutoka kwa wengine wenye wivu na mafanikio yako ,mgogoro kati yako na jirani unaanza.Chukua hatua ,Fikiri kabla ya kutenda,Wish you all the best let's meet on the next discussion.

" Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".
Unaweza kuwasiliana na Mimi kupitia 0767702659
Kupata makala zaidi tembelea page yangu ya Instagram Lackius Robert
Karibu.

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Visababishi vya migogoro:

Ndugu,
Ni kweli kwamba katika utendaji wa kazi zetu na uendeshaji wa maisha yetu ya kila siku kuna wakati tunasababisha
Mgogoro pasipo kujua:

=•Mtazamo
jinsi mtu anavyochukulia au kufikiria jambo ,mawazo ya mtu juu ya jambo fulani.
mtazamo wako ndio huamua ikiwa utakuwa na furaha au la! Mtazamo unaweza kuamua kama utatimiza lengo lako au utakata tamaa. Pia mtazamo utaamua ikiwa utaenda katika njia inayofaa sahihi au isiyo sahihi.

Katika maisha na utendaji wetu wa kila siku sisi sote tuna mitazamo tofauti.
Hivyo usilazimishe mtu jinsi unavyotazama au kuchukulia kitu na mwezako achukulie hivyo au aelewe hivyo.Kwa kulazimisha huko ndipo panapotokea utafauti na mgogoro unaanzia hapo.
Mara nyingi hali hii imekuwa inajitokeza katika mahusiano yetu unavyochukulia kitu unataka mwenza wako na yeye akufate na unamlazimisha ,Familia zetu,katika kazi zetu maofosini na wakati mwingine kuendelea kushikilia msimamo uleule bila kubadilishwa.

=WIVU,Ile hali ya kutopenda maendeleo ya mwenzake au kuona mwenzake anapata yeye hapati hata kama wanatofautiana katika sifa tabia na uwezo.
Binadamu ni kweli tumezaliwa na wivu ndiyo sikatatai lakini sio wivu wa kununiana kutosalimiana au kuzungumza kisa mmojawapo amepata mafanikio fulani fulani labda amenunua kagari,amefanikiwa zaidi kibiashara,au ata kimasomo.
Hali ya wivu Mara nyingi imekuwa ikisababisha sana migogoro binasfi miongoni mwa waliowengi.Kitu kinachowafanya watu wengi kukosa furaha,amani na upendo.

Sio hapo tu bali kuanza kutafuta mazingira ya kumporomosha yule ambaye anaonekana kufanikiwa zaidi.
Kwa kusambaza habari za masimango na maneno mabaya kwa watu ili nao wamuone kama mtu mbaya kumbe ni wivu tu.Kumbuka Wivu ni adui wa maendeleo,Wish you all the best let's meet on the next discussion.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Unaweza kuwasiliana na Mimi kupitia 0767702659
Kupata zaidi makala tembelea ukurasa wangu wa Instagram Lackius Robert
Karibu.

Sunday, August 04, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Ujue zaidi mgogoro

Ndugu,
Karibu katika siku mpya ya leo ambapo tunakutana katika program yetu ya morning motivation diary,Yenye lengo kubwa la kukuongezea maarifa zaidi.
Siku ya leo nazungumzia kuhusu mgogoro:

Mgogoro ni hali ya kutoafikiana baina ya pande mbili au zaidi kutokana na kupishana mahitaji yaani (divergence in nterest).Anahitaji kitu fulani unampatia kingine au unampiga tarehe oh! mara kesho pasipo taarifa inayoeleweka, anataka laki moja unampa elfu kumi hio tisini iliyobaki unamkwepakwepa hapo ndipo utata unapoanzia.Pia maisha kuwa magumu,ukosefu wa Pesa inachangia uwepo wa mgogoro miongoni mwa wahusika.

Hivyo:Mgogoro ni jambo asilia na kwahiyo haliepukiki katika maisha yetu na kazi tunazofanya ,Migogoro inaweza kuwa kati ya wahusika, familia zao, matabaka yao, au hata katika nyadhifa mbalimbali. Vilevile migogoro yaweza kuwa ya kiuchumi, kijamii, mogogoro ya nafsi, na migogoro ya kisiasa ambayo hujitokeza katika mitazamo tofauti kulingana na mazingira.

Mara nyingi katika ushauri tunasema shida sio kujikuta ndani ya migogoro bali shida ni namna tunavyoishughulikia migogoro hiyo kuitatua au kuipunguza makali(Conflict management).
Mgogoro wakati wowote ni dalili ya hitaji lililofichika ambalo alijatatuliwa.

Mara nyingi kinachoonekana kwa nje ni matokeo tu ila tatizo linakuwa mwanzo na kama halijatatuliwa kwa kuangalia mwanzoni (the causative)kuna uwezekano mgogoro kutokea tena.Unaweza sema mgogoro ni kama makaa ya moto yanayoonekana kuzima ukiwasha tena yanawaka.Tiba kubwa ya mogogoro sio kusema huukimbie,uhame familia,mkoa au nchi bali ni kuutatua .Let's meet on the next discussion ,Wish you all the best.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Unaweza kuwasiliana na Mimi kupitia 0767702659.
Kupata makala zaidi ingia katika page yangu ya Instagram Lackius Robert.
Karibu.