HATUA KADHAA ZA KUKUWEZESHA KUWA NA MAISHA BORA KUTOKANA NA UCHAMBUZI WA DR.MAKIRITA AMANI.
VOLUME 1.CHUKUA HATUA
Ø -Tengeneza akili ya kibilionea. Huwezi kuwa na maisha mazuri kama huna maarifa mazuri unayoingiza kwenye akili yako. Jifunze kila siku kwa kusoma vitabu, kuhudhuria semina na mikutano, kuangalia video, kusikiliza vitabu na kila fursa inayojitokeza mbele yako ya kujifunza.
Ø -Tengeneza mageuzi yanayokuwezesha kufanikiwa. Charles Darwin aligundua kwamba, viumbe hai wenye nguvu ndiyo walioweza kuishi na kuzaliana, wale waliokuwa dhaifu walikufa. Ili uweze kuwa na maisha mazuri, lazima uweze kutengeneza mageuzi ambayo yatakuwezesha kuendelea kuwepo wakati wote. Uwe tayari kubadilika, usibaki pale ulipo wakati wote.
Ø -Kuwa mnyenyekevu. Jua kwamba huwezi kujua kila kitu, unahitaji msaada wa wengine kufanikiwa.
Ø Kuwa na mtu/watu ambaye unamwangalia na anakuhamasisha kuchukua hatua. Watu hawa wanaitwa mamenta, ni watu ambao watakuwezesha kupiga hatua kubwa zaidi ya ulipo sasa.
Ø Tofauti ya watu masikini na matajiri ni nidhamu. Wote wanapata fedha, matajiri wana nidhamu ya kudhibiti matumizi, kuweka akiba na kuwekeza. Masikini wanatumia fedha yote mpaka iishe, na wanaenda kukopa.
Ø -Ondokana na mawazo ya bahati nasibu/kamari. Hakuna kitu kizuri kinachotokea kwa bahati na kwa haraka au njia ya mkato. Wapo ambao wamekuwa wakifikiria wanahitaji kushinda bahati nasibu au kamari ili wafanikiwe, dunia haifanyi kazi hivyo. Hata wanaoshinda bahati nasibu au kamari, haiwachukui muda, wanarudi kwenye umasikini.
Ø -Ondokana na hali ya kuona kwamba huwezi. Tumefundishwa woga na kuona peke yetu hatuwezi, mpaka tufanyiwe kile ambacho wengine wamekuwa wanatufanyia. Unahitaji kuondokana na hali hiyo, na kujua kwamba una uwezo mkubwa wa kufanya makubwa. Utumie.
Ø Usizichukie jumatatu na kuzipenda ijumaa. Kwa maisha ya mafanikio, siku zote zinapaswa kuwa sawa. Lakini wasio na mafanikio, huchukia jumatatu na kuziita blue Monday na kuzipenda ijumaa na kuziita TGI (Thank God It’s Friday). Fanya kile unachopenda, ambacho utakifanya kila siku ya maisha yako.
Ø - Unaweza kusoma kitabu kimoja kila siku. Kusoma vitabu ni njia ya kutengeneza timu yako ya washauri kwenye kila unachofanya. Tai Lopez amekuwa na utaratibu wa kusoma kitabu kimoja kila siku, kwa kutafuta yale maarifa muhimu ya kitabu na kukazana na hayo. Anasema vitabu vingi vina maelezo mengi ambayo huyahitaji, ukishajua unataka nini, ni rahisi kusoma vitabu vingi.
Ø -Kugeuza makaa kuwa almasi. Almasi ndiyo kitu kigumu kuliko vitu vyote duniani, lakini inatengenezwa na makaa ambayo siyo magumu sana. kinachotokea ni makaa hayo kuwekwa kwenye presha kubwa mpaka yanakuwa almasi. Hivyo kama wewe unataka kuwa almasi, lazima upitie mazingira magumu, yanayokutengeneza na kukufanya kuwa bora zaidi.
Ø - Jiandae kwa matokeo mabaya, lakini tegemea matokeo mazuri. Mara nyingi mambo hutokea kwenye maisha na kujikuta hatujajiandaa. Hii ni kwa sababu huwa tunafikiri kila kitu kitaenda kama tunavyotaka. Ukweli ni kwamba mambo hayaendi kama tunavyotaka sisi, bali yanaenda kama yanavyoenda yenyewe. Hivyo ni muhimu ujiandae kwenye lolote unalofanya, ili matokeo yakija mabaya, uwe na maandalizi, na yakija mazuri, ufurahie.
Ø -Nguvu za asili. Jua kwamba kuna nguvu za asili, ambazo huwezi kuzivunja na ukabaki salama. Kama ambavyo ukipanda kwenye jengo refu na kujiachia lazima uanguke chini na uumie, japo ndege hawaumii kwa kufanya hivyo. Kila unachofanya, usilazimishe mambo ambayo yatakwenda kinyume na nguvu za asili. Mfano usitake kuanza biashara leo halafu kesho ikawa ina mafanikio makubwa, kila kitu kinachukua muda.
Ø -Tengeneza mfumo bora wa kupanga mambo yako. Kupanga kuna faida kuliko kutokupanga. Lakini kupanga pekee hakuna msaada mkubwa. Unahitaji kuwa na mfumo wa mipango, ambapo unakuwa na mpango zaidi ya mmoja. Unakuwa na mpango wa mambo yakienda vizuri, unakuwa na mpango wa mambo yakienda vibaya, halafu unakuwa na mpango wa mambo yanavyoweza kwenda. Kwa kuwa na mipango hiyo mitatu, hutakwama pale mambo yanavyokwenda tofauti na ulivyotegemea.
Ø -Tengeneza kundi la kukusaidia kufanikiwa. Hakuna mtu anaweza kufanikiwa kwa nguvu zake yeye mwenyewe, kila mtu anahitaji msaada wa watu wengi ili kuweza kupiga hatua kubwa. Unahitaji kuwa na kundi la watu ambao unawategemea na wanakusaidia kupiga hatua. Unahitaji kuwa na marafiki ambao wanakupa hamasa ya kupiga hatua na kukushauri vizuri. Unahitaji kuwa na kundi la washauri (mastermind) ambao wanakufuatilia kwa karibu kwa kila unachofanya. Pia unahitaji wasaidizi kwenye yale unayofanya.
Ø -Zima ujinga wako. Watu wengi hufikiri wanajua sana kumbe hata hawajui, wengine wanaamini wapo sahihi zaidi kumbe hawapo sahihi. Ili uweze kujifunza, lazima ukubali kuzima ujinga wako. Lazima ukubali kwamba hujui ndiyo ujifunze, lazima ukubali kwamba huenda unakosea ili uwe sahihi.
Ukiamini unajua na uko sahihi mara zote, utakuwa na ujinga wako milele.
Ø -Kuwa mmoja kati ya mia moja. Allen Nation aliwahi kunukuliwa kusema siri ya mafanikio kwenye maisha ni kuwapuuza watu 99 kati ya watu 100 na kumsikiliza mtu mmoja. Tafuta yule anayekufaa, yule anayejua na anayekupa hamasa ya kupiga hatua, na msikilize huyo, wapuuze wengine kwa sababu huna muda, fedha wala nguvu za kumsikiliza kila mtu. Kwa upande wa pili, wewe pia unahitaji kuwa mmoja kati ya 100 wanaofanya kile unachofanya wewe, ukifanye kwa ubora na tofauti kubwa sana.
Ø -Chagua eneo dogo unaloweza kulitumikia vizuri. Watu wengi wamekuwa wakifikiria kuanza na eneo kubwa, kuhudumia kila mtu na kuishia kushindwa kabisa. Chochote unachotaka kufanya, anza kulenga eneo dogo, chagua kikundi cha watu ambao utawatumikia vizuri, ambacho utatawala kwa kile unachofanya, na hapo utatengeneza mafanikio makubwa kuliko kutaka kumfikia kila mtu.
Ø -Tengeneza makosa madogo na Kila mtu anakosea kwenye maisha, lakini kukosea kwenye mambo madogo na machache, kunakuwezesha kujifunza na kutokurudia makosa hayo. Kukosea kwenye mambo makubwa na mengi, kunaweza kukuondoa kabisa kwenye safari ya mafanikio. Kwa mfano kama hujawahi kuanza biashara kabisa si vyema kuchukua mkopo mkubwa na kwenda kuanza biashara, utakosea halafu utapata hasara kubwa. Badala yake unahitaji kuanza na biashara ndogo na kukua, utajifunza kupitia makosa madogo utakayofanya, ambayo hayataua kabisa biashara yako.
Ø -Nguvu ya mawasiliano. Siyo unachosema, bali unakisemaje ndiyo kina nguvu. Unahitaji kutengeneza mawasiliano yenye nguvu, ambayo yatakuwezesha kufikisha ujumbe wowote ambao unataka uwafikie watu na waweze kuchukua hatua. Unapotoa ujumbe, wafikirie wale unaowapa ujumbe, na jua kitu gani kinawahamasisha kuchukua hatua. Kwa kujua hayo, utaweza kuwahamasisha kuchukua hatua.
Ø Kila mtu ashinde au usikubaliane kabisa. Kuna aina tatu za makubaliano, moja mmoja ashinde na mwingine ashindwe, mbili, wote washinde, tatu wote washindwe. Unapoingia kwenye makubaliano yoyote na mtu yeyote, hakikisha kila upande unashinda, kama hilo haliwezekani basi ondoka kwenye makubaliano hayo, hata kama wewe unashinda na upande mwingine unashindwa. Njia pekee ya kujijengea sifa bora na ushirikiano na wengine, ni kumwezesha kila mtu anayejihusisha na wewe kushinda.
NI Nimatumaini yangu makubwa kuwa kuna kitu umeweza kujifunza ,karibu upate uchambuzi wa vitabu kwa lugha ya kiswahili tena kwa bei nafuu vitabu kama Rich dad poor dad,think and grow rich na vitabu vingine kadha wa kadha tayali tumevichambua tayali tuwasiliane kupitia 0767702659 Lackius Robert au bonyeza link kujiunga katika kundi letu la telegram
MMungu akubariki zaidi.
N