Monday, September 30, 2019

Jinsi ya kupata mtaji wa biashara au mradi

MORNING MOTIVATION DIARY

Jinsi ya kupata mtaji

Ndugu,
Ni siku nyingine tena ambapo tunakutana katika program yetu ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.

Unaweza kuomba mkopo Kutoka Kwenye Vyama na Vikundi mbali mbali,

Vyama vya kama SACCOS na Vikoba  Sifa kubwa unayotakiwa Kuwa nayo ni kuwa mwanachama wa chama chenye kukopesha na kufuata masharti ya chama husika.Mara nyingi vyama hivi na vikundi huwa vinatoa mkopo wenye riba na masharti ambayo siyo magumu kuyazingatia.
Watu wengi wamekuwa wanaanza biashara kwa kukopa Pesa kutoka kwenye VICOBA na kuweza kufanikiwa .
Miongoni mwa faida ni kwamba unakuwa na uhakika wa mtaji kuupata japo ata kama utakuwa ni mdogo ,na na mara nyingi wanakikundi wanakuwa wanakujua jinsi unavyochangia au jinsi unavyojituma.Inaweza kuanza na mtaji  mdogo, kama unahisi au unaepuka kufilisiwa mali zako ,lakini ukishaanza kuizoea biashara na ukaziju changamoto zake unaweza kukopa zaidi na ukawa inarudisha faida. Ni muhimu kutumia kanuni ya
 MAUZO _FAIDA= MATUMIZI hii ni kutokana na mwandishi Mike Michalowicz kayika kitabu kinachotwa  Profit First: A Simple System To Transform Any Business From A Cash-Eating Monster To A Money-Making Machine kilichoandikwa na Mike Michalowicz.Mwandishi anasema wafanya biashara wengi wamekuwa wanachukua mauzo na matumizi afu mwisho wa siku wanakuja kutafuta faida hivyo kama mjasriamali inabidi utoe faida kwanza uiweke pembeni ndo uangalie mauzo.

Ndugu yangu mpendwa hata kama umepata mtaji mdogo usisite kuanza kisa mtaji ni mdogo anza tu utakuwa unaongezea kidogo kidogo.

Unaweza kukopa kupitia taasisi za kifedha,
Taasisi mfano Benki
 Vigezo vikubwa wanavyoangalia benki ili wakukope ni kuwa na biashara ambayo umeianzisha angalau kuanzia miezi  sita au zaidi ambayo  ina mzunguko mzuri wa fedha.Uwe na account ya benki husika au uwe unaitumia benki husika pia uwe na dhamana ambayo utaiweka ili kama unashindwa kulipa waweze kuichukua ile dhamana ili kufidia.
Kadili unavyokuwa unaitumia benki ndivyo unavyozidi kuipa ushwawishi benki kukukopa maana benki nao wanaangalia mihamara (transaction) unazokuwa unazifanya.Wakati mwingine kama wewe ni mdau mzuri benki wenyewe wanaweza kukushawishi kukukopa maana kutokana na mihamara unayofanya unaonekana kukopesheka.

Lakini pia zipo  microfinances, hizi ni taasisi za kifedha ambazo hutoa mikopo midogo midogo kwa wahitaji.Hivyo unaweza tumia hizo na kuweza kuifanikisha biashara yako au mradi wako.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kwa mawasiliano zaidi 0767702759 Lackius Robert
Karibu.


Jinsi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara au mradi

 MORNING MOTIVATION DIARY

Jinsi ya kupata mtaji

Ndugu,
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika programu yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako kwa kukuongezea maarifa na kuifanya kuonekana mpya.

Kujiwekea akiba wewe mwenyewe (saving),Akiba ni sehemu ya mapato ya ambayo huwekwa kando kama akiba ya dharura na mahitaji yasiyotarajiwa,mara nyingi akiba hutegemea sana jinsi mtu alivyojithatiti katika kuwekeza.Ukiweka akiba kubwa utakuwa na faida kubwa ,ukiwekeza kidogo utakuwa na faida kidogo.
Hii ndiyo sehemu ya kwanza na muhimu sana ambayo kila mmoja wetu anaweza kuanzia. Japo wengi hukosa nidhamu katika fedha na akiba zao, lakini unapaswa kujua hii ni sehemu nzuri ya kuanzia kupata mtaji wa kuanza au kukuza biashara yako.

Mara nyingi unashauriwa kukigawa kipato kabla hujakipata na mara unapokipata unakigawa kabla ujakitumia baada ya kukigawa kipato na kuweka akiba ndo unafanya matumizi mengine.
Njia hii ya kujiwekea akiba  umuwezesha mtu kuanza biashara akiwa na mani na bila ya usumbufu wowote wa kwamba ataanzia wapi .Hivyo mi nakushauri anza leo kujifunza kuweka akiba, ni ngumu sana kufika juu bila kuweka akiba.Angalia ni kiasi gani unapata kisha tenga faida au tumia ,kanuni ya asilimia 10 tu ya kipato chako na huo ni mtaji wako wewe mwenyewe.Mfano unapokea 100000/= kwa mwezi tenga 10000/= kama umepata 50000/= tenga 5000/= Mara nyingi mwanzo wa kujiwekea kipato huwa ni mgumu hivyo unajitahidi kufanya hivyo angalau miezi mitatu ya mwanzo ili uweze kuzoea.

Kama bado hujaanza ni muda wa kuanza ,kama tayali ushaanza jitahidi uyashinde majaribu maana saving inazo changamoto zake.

Kutoka kwa ndugu,jamaa na marafiki,
Ukiacha njia ya kwanza ya kuweka akiba(saving),njia nyingine inayoweza kukusaidia kupata mtaji ni kutoka kwa ndugu na marafiki.
Zama hizi watu wapo tayali kutoa pesa nyingi kwenye harusi ila ukiwaambia kuhusu biashara mtakimbizana,na watakukwepa utasikia yaani kama ungenambia jana au leo asubuhi  maana kuna mtu nimemwazima kiasi fulani.Mwingine atasema njoo ijumaa,jumamosi lengo ni kutaka kukukwepa lakini nakushauri usisite kumfatria atakupa tu ila wengi wamekuwa hawathubutu kuwabana vizuri.
Unaweza kuwatumia ndugu, jamaa na marafiki kupata mchango wa kuanza au kukuza biashara yako. Jambo lingine la msingi ni kuandaa vizuri wazo la biashara yako, na kuonesha ni kiasi gani cha fedha unahitaji ,ahadi zote utakazopewa jitahidi uzifatrie amini usiamini watu wengi wametajirika kupitia ndugu, jamaa na marafiki, mfano mtu tajiri kuliko wote barani Afrika kutoka Nigeria Dangote yeye wakati anaanza ujasiriamali aliomba msaada kwa ndugu, na kwa sasa tunaona maendeleo yake amekuwa bilionea ambaye amewekeza sana barani Afrika kwa vitu mbalimbali anavyouza kama  unga , mchele, mafuta, sukari,cement.Wakati anaomba hakuona haya kama wengi wetu tulivyo.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa Unapoomba usitegemee msaada wa fedha tu bali wapo watakaokupa msaada wa mawazo ushauri.Kuwa makini sana 'ongea na wote wasikilze wachache'  wengine watakupa msaada wa kifedha na uo utakuwa ni mwanzo wa wewe kusimama imara katika mradi/biashara.

Unaweza tumia mwekezaji wa biashara,
Mwekezaji ni mtu ambaye ana fedha ambazo anaweza kuziweka kwenye biashara mbalimbali na zikazalisha. Huwa hatoi fedha kama mkopo, bali naye huwa anakuwa sehemu ya umiliki wa biashara.
Kigezo kikubwa kinachohitajika ni kuwa na mpangilio mzuri unaoonesha mchanganuo wa biashara inahusu nini, wateja ni kina nani, wanapatikanaje na mipango ya ukuaji wake,jinsi utakavyokuwa ujalipa kodi.  katika hali hiyo unaweza kumshawishi mwekezaji kuwekeza kwenye biashara au mradi wako.

Anapowekeza kwenye biashara yako maana yake unampa hisa, hivyo unapopata faida na yeye anapata faida kulingana na mtaji alioweka katika biashara au mradu wako.Ikitokea hasara imepatikana na yeye hasara anapata hasara pia.
Kwenye hili unahitaji kuwa makini kwa mwekezaji unayemchagua inabidi awe  wa kuaminika na awe tayari kusubiri biashara hiyo ifanye vizuri. Pia wewe binafsi unahitaji kujituma sana kuhakikisha biashara inafanya vizuri ili usije kumwangusha yule anayekusaidia.

Kwanini ninasema unahitaji kuwa makini ni kwa sababu
biashara isipotengeneza faida kwa muda mliokubaliana inaweza sababisha kushitakiana na hatimaye biashara na mali zako kufilisiwa,ili kukwepa hiyo inabidi uwe unampatia taarifa ili ajue kinachoendelea.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu.



Monday, September 23, 2019

Mambo usiyoyajua kuhusu ujasriamali

 MORNING MOTIVATION DIARY

Mambo usiyoyajua Kuhusu ujasriamali,

Ndugu,
Karibu katika siku nyingine tena katika mwendelezo unaoelezea mambo usiyoyajua kuhusu ujasriamali,
Karibu:
Ujasiriamali ndiyo njia yenye hatari ndogo kwenye kipato.
Kuna watu  wameambiwa na  kuaminishwa kwamba  ujasiriamali ni hatari sana kwenye upataji wa  kipato. Kwamba unapokuwa mjasriamali unakuwa huna huakika wa kupata kipato asa pale unapokuwa na uhitaji wa fedha na usiweze kuzipata kwa haraka.Badala yake wameaminishwa kwamba ajira ndiyo njia ya  uhakika na yenye hatari ndogo kwenye upande wa kipato. Kwakuwa kila mwezi mtu anakuwa na  uhakika wa kupokea mshahara wake na hivyo ni kitu anachoweza kukitegemea.Kwa mjasriamali anayechukua tahadhari (take risk ) kwake siyo tatizo kubwa maana anakuwa amejipanga in case lolote likitokea.

Hali hii imekuwa kikwazo kwa wengi kufanikiwa kwenye ujasiriamali kwa sababu wanaingia wakiwa wnajua kwamba, kuingiza kipato siyo ni jambo ambalo kidogo siyo haraka.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa  katika kazi yoyote ile unayoifanya lolote linaweza kutokea kama uko katika ujasriamali unaweza kuyumba kifedha  na kwa aliye kwenye ajira anaweza kusimamishwa kwa hiyo wote  wanakuwa kwenye wakati mgumu kifedha.Ila utafiti unaonesha ujasriamali una hatari kidogo kulinganisha na kazi nyingine yoyote kwa mtu aliye makini.

Ujasiriamali ni asili yetu binadamu,
Watu wamekuwa wanaamini kwamba kuna watu ambao wamezaliwa kuwa wajasiriamali na wengine wamezaliwa kuwa waajiriwa pekee.Hali hii imewafanya wengi kushindwa kwenye ujasiriamali, wakiamini kwamba wao sio wajasriamali.

Lakini ukweli ni kwamba ujasiriamali ni asili yetu kama binadamu, kila mtu ana ujasiriamali ndani yake. Ukiangalia historia ya maisha ya wanadamu hapa duniani, kwa kipindi kirefu tumekuwa tunaendesha maisha yetu kupitia shughuli za kiujasiriamali

Wazee waliotutangulia waliweza kwa kujiusisha na shughuli za kijasiriamali ili kupata mahitaji yao makubwa ambayo mara nyingi yalikuwa ni chakula, mavazi, malazi na usalama.

Kila mmoja anaweza kuwa mjasriamali, Kama nilivyotangulia kuandika somo lililopita kuwa ujasriamali ni asili yetu hivyo ni wazi kwamba kila mtu anaweza kuwa mjasriamali.Kwa kuwa ujasriamali auchagui rangi ,kabila au jinsia au kusema mpaka uwe na elimu kubwa sana.Ujasriamali unategemea kwa jinsi gani ulivyojiandaa na kuingia kwenye shughuli.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa,Usiingie kwenye mradi wowote au biashara kwa kufuata mkumbo kisa umeona  fulani kafanya jipange kwanza ili ukianza umeanza.Jiambie Mimi ni mshindi usikubali kurudi nyuma wala kuyumbishwa na mtu mwingine,Wish you all the best.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu.

Mambo usiyoyajua kuhusu ujasriamali

MORNING MOTIVATION DIARY

Mambo usiyoyajua kuhusu ujasriamali

Ndugu,
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika programu yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako kwa kukuongezea maarifa na kuifanya kuwa mpya.

Hakuna njia ya mkato kwenye ujasiriamali,

Watu wengi wamekuwa wanaingia kwenye ujasiriamali kwa mtazamo kwamba ni njia ya mkato na ya haraka ya kupata fedha. Ndiyo maana watu wamekuwa wanatumia muda mwingi kukimbizana na fursa zinazojitokeza ili wapate mafanikio haraka.

Lakini ukweli ni kwamba ujasiriamali unahitaji ufanye  kazi, utumie muda wako kujifunza pia kuwa na uvumilivu katika yale unayofanya.

Ukijaribu kuangalia kuna watu wamedanganywa sana kuhusu fursa mpya mpya ambazo zimekuwa zikijitokeza kila siku. Wamepewa hesabu za kwenye karatasi, zikawahamasisha, wakaingia kichwa kichwa na kupata hasara kubwa sana.Mwishowe kuanza kujilaumu kwa maamuzi waliyoyafanya.

Nikukumbushe ndugu mpendwa ,ujasiriamali unahitaji ujipange kama kweli umeamua kuufanya na kuwa tayali kupambana na kila hali itakayokutokea.

Kama inawezekana anzia sehemu yenye mkusanyiko kidogo,
Malengo makubwa ni kujifunza zaidi maana unapoanzia padogo kuna vitu vingi unavielewa zaidi kuliko kuanzia pakubwa maana kuna baadhi ya changamoto utazifahamu na kujifunza jinsi ya kuzitatu.Sasa Kosa kubwa ambalo watu wamekuwa wanalifanya kwenye ujasiriamali ni kuiga wengine. Mfano wanapoona wengine wanafanya biashara fulani, hujiambia hiyo biashara inalipa na hivyo huamua kuifanya matokeo yake kushindwa kuiendeleza baada ya kutoenda vizuri.

Kama mtu anayetaka kufanikiwa kwenye ujasiriamali, unapaswa kwenda sehemu yenye mkusanyiko mdogo, kwa kufanya kile ambacho hakuna wengine wanaokifanya.na  kama kuna wanaofanya, basi wewe unakuwa na utofauti fulani fulani.
Ambacho wateja wako hawawezi kukipata sehemu nyingine isipokuwa kwako pekee.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa ,una uwezo wa kufanya kitu kikaonekana cha upekee maana hakuna mtu mwingine ambaye ni bora zaidi yako,na upekee ulionao ni mkubwa kama yupo anakarbia kufanana na wewe ila hawezi kulingana na wewe.

Unapofanikiwa katika biashara moja hakumanishi unajua biashara zote,
Mafanikio kidogo kwenye ujasiriamali kwa wengi imekuwa kikwazo kwa mafanikio makubwa zaidi. Mtu anaanzisha biashara moja, inafanikiwa na kufanya vizuri na hapo ndipo kushindwa kunapoanza. Wengi uamini kwa kiwa wamefanikiwa kwenye biashara moja, basi wanaweza kufanikiwa kwenye kila aina ya biashara zingine.Hivyo huanza kujihusisha na biashara nyingine nyingi na tofauti tofauti kwa kuamini uzoefu wao kwenye biashara moja utawasaidia kwenye biashara nyingine wanazoanzisha.

Hali hii imekuwa inafanya wengine kurudi nyuma kimafanikio maana wanapoanzisha biashara yingine huweka nguvu nyingi kule tofauti na ilivyokuwa awali.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa ,Biashara zinatofautiana na pia zina changamoto ambazo ni tofauti tofauti ,hivyo unapofanikiwa kwenye biashara ya aina fulani, ni vyema kuendelea kuweka nguvu ili ufanikiwe zaidi.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659

Lackius Robert karibu.

Sunday, September 22, 2019

Zijue kanuni za kuwa mjasriamali bora

MORNING MOTIVATION DIARY

Zijue kanuni za ujasriamali,

Ndugu,
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kukuongeza maarifa na kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.Karibu katika mwendelezo unaoelezea kanuni ambazo mjasiriamali anapaswa kuzizingatia:

Kuwa na umakini,hii ni moja ya kanuni bora kwa sababu ndiyo inayosababisha biashara au mradi wako kusonga mbale maana kila kitakachofanyika kinahitaji umakini mkubwa.Katika kuajiri,katika kusambaza huduma ,katika kuzungumza na wateja n.k
Ukiangalia waliofanikiwa siyo tu walikuwa tayari kufanya kazi bali waliweka umakini mkubwa katika kazi walizokuwa wakifanya. Kama mjasiriamali unatakiwa kuwa mwangalifu kwa kila jambo, unatakiwa kujua soko linaendaje na pia ni lazima awe na uelewa wa kutambua mabadiliko yanayojitokeza katika soko, uzalishaji na uendeshaji kwa jumla.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa,
Kushika namba moja kwenye kile unachofanya siyo bahati ila ni umakini mkubwa.
CHONDECHONDE "Mazuri ya dunia ni mengi na yapo kila sehemu kuwa makini usipotee njia".

Umuhimu wa kuwa mwaminifu,Kama mjasiriamali mwenye malengo makubwa ya kufika mbali kanuni hii ni muhimu kuifanyia kazi na kuenenda nayo.
Maana uaminifu ni silaha kubwa itakayokulinda mjasiriamali na kuwafanya watu wengi wapende kufanya biashara na wewe au kuwekeza kwenye miradi yako.Ni vema kuwa mwangalifu katika  kulipa madeni hata kama ni madogo unapodaiwa, pia wauzie wateja wako huduma au bidhaa kwa bei halali.Kama tunavyojua serikali yetu inajiendesha kwa kutumia kodi hivyo mjasiriamali ni vema sana kulipia kodi na vibali vyote muhimu vinavyohitajika ili kukuweka katoka hali ya uhuru pindi uwapo kazini .Ili kuboresha huduma zako usiwe unatoa bidhaa zilizokwisha muda ,zingatia kutoa bidhaa bora maana mteja anapokuja kwako anakuwa anakuamini hivyo zidisha uaminifu kwake ili kesho arudi.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa "Uaminifu wako ndio mtaji na mafanikio ya kazi yako wala  huhitaji elimu kubwa ,Pesa n.k uaminifu upo ndani yako kazi kwako kuukuza na kuuboresha.CHONDE CHONDE" Usimuuzie mteja bidhaa kwa kumukomoa utampoteza".

Tumia pesa vyema
,Ukija kuangalia miongoni mwa
changamoto zinazowakabili wengi wakiwemo wajasriamali ni kwenye  matumizi ya pesa.Hii inaanzia kwenye matumizi yao binafsi ya pesa, Watu wengi wanapata pesa lakini zinaisha bila ya kufahamu wamezitumiaje au wamefanya kipi chenye tija.Hivyo kuwa na  matumizi mazuri ya pesa ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali, kwani kwa njia hii utaweza kukuza biashara yako kila siku. Jifunze kufahamu hii ni pesa kwa ajili ya nini, na uitumie kwa mambo ya msingi pekee. Epuka tabia za kibadhirifu na anasa. Ikiwa biashara au uwekezaji wako ni mkubwa, basi unaweza kumwajiri mtu aliye na taaluma ya utunzaji na usimamizi wa pesa.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa,Fedha ndio uti wa mgongo wa biashara yako ukiitumia vizuri itakudaidia ukiitumia ndivyosivyo hatamatokeo yake yatakuwa hivyohivyo.

"Ushindi upo mikononi  mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu.

Saturday, September 21, 2019

Zijue kanuni bora za ujasriamali

MORNING MOTIVATION DIARY

Zijue kanuni za ujasriamali

Ndugu,
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kukuongezea maarifa na kuing'alisha siku yako na kuiona mpya.

Ujasiriamali una kanuni zake ambazo ni muhimu sana kuzijua na kuzifuata ili kuyafikia mafanikio ya kweli. Ili ufanikiwe katika Ujasiriamali kama ilivyo katika shughuli nyingine yoyote, zipo kanuni na misingi ziliyowekwa ili uzizingatie na kuzifanyia kazi .Mara  nyingi kanuni hizi ni kama mwongozo unaotuongoza katika kufanikisha jambo, kanuni hizi hapa:

Kujituma na kupenda  kazi unayoifanya,
Ni kweli kwamba kuna watu wanafanya kazi ambazo hawazipendi ila wanafanya tu ilimradi tu mtu apate kipato.Kama mjasiriamali ili ufanikiwe katika biashara yoyote, lazima uwe na moyo wa kujituma na uipende kazi unayoifanya. Usisubiri kusukumwa kwa sababu hakuna atakayefanya kazi hiyo. Jifunze kuwahi kuamka asubuhi ili uendane na kasi ya soko, jitume kufanya mambo yatakayoiboresha biashara yako bila kuchoka na fanya kazi kwa moyo wako wote.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa, hakuna kitu kinachompa mtu furaha kama kufanya anachopenda ,mtu wa aina hiyo awezi kuchoka,huwa yuko tayali kufanya kazi muda mwingi hata changamoto zinazojitokeza haziwezi kumnyumbisha.Hii ni kanuni bora kuizingatia kama mjasiriamali ili uweze kufika mbali kama unachofanya bado haujakipenda jitahidi ,ongeza juhudi Kaza """ dunia inakutegemea""".

Kuthubutu,
Mjasriamali bora ni yule mwenye uwezo na utayari wa kufanya maamuzi magumu ya kuingia kwenye biashara au mradi fulani huku akiwa ameondoa nidhamu ya woga na kuanza kupiga kazi.Ukweli ni kwamba kuna watu ambao  ni waoga wa kuchukua hatua ya kuanzisha biashara au  kuingia katika miradi fulani fulani sababu ya woga wa kushindwa mbeleni. Hasa hasa watu wengi huogopa kupata hasara na kuzomewa pindi waangukapo au wanapoyumba katika kuiendesha biashara au mradi walioanzisha.Kama  mjasiriamali bora ni lazima awe na uwezo wa kuthubutu kufanya mambo makubwa ,ikiambatana na uelewa mkubwa zaidi baada ya kujiridhisha na kufanya biashara yako.Ili kuepuka kuanguka au kuyumba inabidi uwekeze katika kitu ambacho umefanya angalau utafiti ili ujue hekaheka zake kabla aujaanza kukifanya.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa hakuna mbadala wa mafanikio tofauti na kuthubutu na kuongeza juhudi katika kitu unachofanya.

Kuwa na usimamizi mzuri,
Kama mjasiriamali ambaye unahitaji kufika mbali kimafanikio kupitia biashara yako au mradi wowote unaoufanya ni vema zaidi
Kuwa na uwezo wa kuisimamia vizuri.
Hii inaambatana na kutoa maamuzi sahihi mara zote. Katika Ujasiriamali, uwezo wa kusimamia na kuwaongoza watu walio chini yako ni muhimu sana kwani hata kama ukianza na biashara ndogo, lazima baadaye itakuwa kubwa hivyo utalazimika kuajiri watu wengine wa kukusaidia ili kazi zako ziende.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu.

Friday, September 20, 2019

Faida za kuwa mjasriamali bora

 MORNING MOTIVATION DIARY

Faida za ujasriamali

Ndugu,
Leo ni  siku nyingine tena kwenye program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuiboresha siku yako na kuifanya iwe mpya.Karibu tujifunze faida za kuwa mjasiriamali:

Kuongeza kipato,
Hii ndiyo dhana ambayo kila mmoja wetu anahihitaji.Unapokuwa mjasiriamali unakuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza kipato chako na kukudhi baadhi ya mahitaji ambayo pengine mshahara ulikuwa auyatimizi.
Kila mmoja ana ndoto nyingi ambazo anataka kuzitimiza,Kama ulikuwa unajiuliza utawezaje kuzitimiza basi jibu mojawapo ni kuwa mjasriamali ambaye anajituma na kufanya kazi kwa bidii.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa,ili kuweza kuongeza kipato chako lazima uwe mpambanaji ,mbunifu inabidi uwe  mjasriamali ambaye anaenda na wakati.Tofauti na hapo utachukua muda mrefu kutimiza ndoto zako kama bado  auna vyanzo imara vya kipato chako.Hali ambayo itaendelea kukunyima Uhuru wako kifedha,Kumbuka mjasriamali wa Leo ni tajiri wa kesho.

Kuwasaidia watu wengine,
Katika kitabu cha My philosophy of success chake Jim Rhom katika sura ya pili kwenye "Falsafa ya utendaji na uzalishaji " anasema ili kufanikisha utajiri na ukuu katika dunia hii inabidi utafute namna ya kuwasaidia watu wengine.Tumia ujuzi wako kuhakikisha watu wanapata msaada wako, hivyo                     hutaweza kufanikiwa katika maisha yako kama bado auwasaidii watu wengine.Hapa ndipo watu wengi hufa wakiwa masikini bila wao kujua,kwa sababu ya kushindwa kuwasaidia watu wengine katika nyanja / kazi mbali mbali.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa unapokuwa kuwa mjasiriamali unakuwa na uwezo wa kuwaajiri watu,kuwapatia huduma bora na ukizingatia katika kanuni za biashara kwamba mteja siku zote ndiye bosi.Hivyo unapokuwa unatoa huduma bora kama mjasiriamali unakuwa unajihakikishia ukuu na utajiri unaunyemelea.Angalia wajasiriamali wakubwa jinsi wanavyowasaidia watu mbali mbali wenye uhitaji,na wanapowasaidia ndivyo kazi zao zinavyozidi kusonga mbele zaidi.Unachotoa ndicho unachopata ni sawa na unavuna ulichopanda,kupitia ujasriamali wako waoneshe wengine jinsi ya wao kufika pale hakika utakuwa katika nafasi kubwa ya kufanikiwa zaidi.

Kutatua matatizo na kutumia fursa,
Malengo makubwa ya watu kuingia kwenye ujasriamali ni kutoa huduma bora kwa watu , kwa kuwasaidia kuwapatia hudumabora.
Kama tunavyojua fursa nyingi zinatokana na matatizo tuliyonayo au mahitaji mbalimbali tunayoyahitaji katika maisha yetu ya kila siku.
Mfano kama kuna watu wana uhitaji wa maji katika jamii /mtaa uliopo ,kama mjasiriamali ukitengeneza mfumo wa kuwapatia watu maji tayali umetatua tatizo la maji na umetumia fursa hio.Hivyo unawapatia maji na wao wanakupatia Pesa,inakuwa ni win win situation.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa mafanikio yoyote tunayoyata yanategea sana kwa jinsi gani tunatoa huduma zilizobora kwa watu wanaotuzunguka.Hasa hasa kwa kutatua matatizo mbalimbali yanowakumba.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659
Lackius Robert karibu.

Thursday, September 19, 2019

Faida za kuwa mjasriamali

MORNING MOTIVATION DIARY

Zijue faida za kuwa mjasriamali,

Ndugu,
Karibu katika program nzuri ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kukuongezea maarifa ,kuing'alisha siku yako na kuonekana mpya.Faida za kuwa mjasriamali:

Uhuru wa kifedha,
Ujasiriamali unatajwa moja ya shughuli kubwa ambayo endapo ikitumika vizuri na kwa malengo itakupa uhuru mkubwa wa kifedha.moja kati ya wajasiriamali niliobahatika kusoma makala zao ni Coach Bassanga yeye anasema aliamua kuwa mjasiriamali ili akidhi aweze kupata Uhuru kifedha.Anasema hakuna kitu ambacho kilikuwa kinamuudhi kama ikitokea shida ya pesa halafu huwezi ihimili.Kama ni mfanyakazi mpaka kusubiri mshahara utoke na kama siyo mfanyakazi unaangaika kuipata hiyo pesa .Kwa upande wa  mishahara Mara nyingi inapotoka watu wengi huwa wanalipa madeni waliyokopa hivyo ikija kufika tena mwisho wa mwezi tayali Pesa inakuwa imeisha.
Kwa mjasiriamali ambaye ana kitu kingine cha ziada cha kumuingizia kipato inamsaidia kukidhi mahitaji mengine sio kutegemea mshahara.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa ,tafiti nyingi zinaonesha mshahara hautoshelezi mahitaji ya watu ,hivyo kama unahitaji kupata Uhuru wa kifedha unaweza anzisha kitu cha ziada cha kukuingizia Pesa ili usiwe unategemea mshahara tu.Coach Bassanga anasema "mjasiriamali wa Leo ni tajiri wa kesho".

Ujasiriamali utakupa nafasi ya kufanya kile unachokipenda.
Tafiti na takwimu nyingi zinaonyesha kuwa asilimia kubwa  ya watu,wanafanya kazi ambazo hawazipendi ila wanafanya tu kwa sababu hawana namna nyingine ya kujiingizia kipato. Hivyo uamua kukomaa nazo hivyo hivyo  ili kusogeza siku ,lakini kwa wafanyakazi wanaoamua kufanya pia ujasiriamali wanapata fursa ya kuwa na unafuu.Maana kwenye ujasriamali unafanya kilicho moyoni bila kushinikizwa na mtu wala kulazimishwa.
Kupitia ujasiriamali utaamua nini ukifanye na kwa wakati gani,wapi na lini kulingana na matakwa yako.
Hapa wewe mwenyewe unaamua biashara ipi ufanye ,kulingana na nafasi /muda ulionao inaweza kuwa ya nguo,chakula,vinywaji na vingineo.Ili uweze kujipatia kipato cha ziada na kuanza kukidhi baadhi ya mahitaji mengine ambayo kazi uliyokuwa unaifanya awali ilikuwa aijakidhi.

Uwezo wa kupanga ratiba yako binafsi.Sana sana hii ipo kwa watu ambao wameamua kuwa wajasiriamli moja kwa moja.
Pamoja na ukweli kwamba unatakiwa kufanya kazi kwa bidii sana na kuwa na usimamizi thabiti kama mjasiriamali, ukweli ni kwamba unakuwa na  uhuru wa kupanga ratiba na muda wake kulingana na vipaumbele ulivyonavyo. Hii ni tofauti kabisa na mtu ambaye yeye huuza muda wake kwa mwajiri ili aweze kujipatia kipato.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa ,kila mtu anawaweza kufanya ujasriamali na kuwa miongoni mwa watu wenye mafanikio makubwa.Kitu ambacho bado kinatukwamisha ni maneno na mipango ,yaani tuna mipango mingi sana.Unaweza kuzungumza na mtu akawambia mipango mpaka ya 2025 lakini ukimuliza ambayo ametimiza kwa sasa utasikia ,unajua kuna mtu namsubilia kidogo,muda sio mrefu ntaanza inafika mpaka mwakani ajaanza.Kama mjasiriamali panga jambo na ulitende muda unao unaweza kuutumia vyovyote unavyoweza.
"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert
Karibu.

Wednesday, September 18, 2019

Zijue sifa za mjasriamali bora

MORNING MOTIVATION DIARY

Zijue sifa za mjasiriamali bora

Ndugu
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.
Ili kuwa Mjasiriamali bora /au kujiboresha mwenyewe katika ujasiriamali wako ,sifa zifuatazo ni muhimu kuzifatria na kuzijua kwa undani:

Mtu mwenye kuongeza bidii,
Moja kati ya msemo unaopendwa kutumiwa na mwandishi na muhamasishaji Rodrick Nabe ni huu "Mafanikio ni mchakato" hivyo mafanikio huja kwa wale ambao wanakuwa na bidii kubwa kuyatafuta.Kama mjasiriamali ni vema kuongeza juhudi katika mambo mbali mbali ambayo yanaweza kukuvusha kutoka hatua moja hadi nyingine ,ikiwemo kuongeza bidii katika kujifunza vitu vipya ili kuenenda na kasi ya mabadiliko kwenye ulimwengu huu.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa
Bidii ni msingi wa kufanikiwa kwenye jambo au shughuli yoyote,pia ni muhimu kukumbuka kuwa mjasiriamali ni mwajiri na ni boss wake yeye mwenyewe. Ni vema kuongeza bidii binafsi pamoja na  kujituma katika kufanya kazi bila ya kusukumwa na mtu yeyote.

 Kujifunza kutokana na makosa,
Kuna ukweli usiopingika kuwa "makosa ni shule muhimu kwa kila mtu", ndivyo ilivyo pia kwa mjasiriamali ambaye ana malengo ya kufika mbali.
Mjasiriamali anapaswa kuwa na sifa ya kupenda kujifunza kutokana na makosa ili asiyarudie tena mbeleni na wala si kuyaogopa au kuyakimbia.
Kama uliwekeza pesa zako zikapotea, basi usiache ujasiriamali bali baini ni nini kilisababisha ukapoteza pesa zako ili ukiepuke mbeleni.
Kuanza biashara kutoka kiwango cha kidogo mpaka kuwa mjasiriamali mkubwa siyo kazi ya mchezo mambo mengi inabidi uyafanye.Kama mjasiriamali utakutana na changamoto nyingi. Hili haliwezi kuwa tatizo ikiwa uko tayari kujifunza kutokana na makosa na kufahamu njia za kuyaepuka huko mbeleni. Hivi ndivyo wajasiriamali wengi wanavyojifunza na kukua zaidi na zaidi.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa usemi wa kosa siyo kosa bali kurudia kosa ndilo kosa,hivyo unapokuwa kwenye biashara au kazi yoyote ni lazima ufahamu makosa ambayo yanaweza kuathiri biashara au uwekezaji wako ,mfano makosa kama ,kujifanya unajua kila kitu,kutaka wateja wakufuate,matumizi yasiyo mazuri ya fedha,kupuuza baadhi ya mambo.Hii inakusaidia kuongeza umakini katika mambo yako mwisho wa siku inakusaidia kulitimiza lengo lako.

Mtu ambaye ni dynamic (anayeenda na mabadiliko),Mjasiriamali bora ni yule asiye static kwa maana ya kubakia tu na kitu alichonacho miaka nenda miaka rudi bali ni yule ambaye anaenda na mabadiliko.Kwa sababu kuna mabadiliko makubwa kiuchumi,kiteknolojia ,kisiasa ,kimazingira pia na kimahitaji.
Ili kuenenda vizuri ni vema kuongeza juhudi ya kuangalia nini kinahitajika ,na nini kiboreshwe zaidi ili uhutaji wake uendele.Hasa hasa katika utoaji bidhaa mbalimbali kwenda kwa watumiaji hivyo unavyokuwa unabadilika kuenenda na mabadiliko ndivyo unavyozidi kuwa sokoni tofauti na wale wasio na mabadiliko katika utoaji wa huduma.

Ndugu yangu mpendwa ni imani yangu kuwa sifa za ujasriamali bora umezielewa zaidi na utazifanyia kazi.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert.
Karibu.

Tuesday, September 17, 2019

Sifa za mjasiriamali bora

MORNING MOTIVATION DIARY

Zijue sifa za mjasiriamali bora,

Ndugu,
Ni siku nyingine tena tunakutana katika program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.
Ili kuwa Mjasiriamali bora /au kujiboresha mwenyewe katika ujasiriamali wako ,sifa zifuatazo ni muhimu kuzifatria na kuzijua kwa undani:

Mtu anayejitahidi kutafuta taarifa,Kama unavyojua sasa hivi tuko kwenye kipindi ambacho teknolojia inakua kwa kasi ,na mambo yanabadilika kila uchao ili kuendanana na kasi hiyo ni muhimu kusaka taarifa zaidi.
Mjasiriamali bora anatafuta taarifa kutoka sehemu mbalimbali kwa watu tofautitofauti kama vile wateja, washindani,kusoma vitu mbali mbali ikiwemo vitabu husika.
Pia hufanya utafiti binafsi wa namna mbalimbali za kuvutia wateja na kuboresha huduma bora ili kuongeza wigo wa wateja na kipato kwa ujumla.
Mjasiriamali Pia uomba ushauri kutoka kwa wataalamu na  wadau mbalimbali wa masoko kulingana na biashara anayofanya lengo kubwa ni kuongeza uelewa zaidi.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa, taarifa sahihi zinaleta maarifa sahihi ukiwa na chanzo chenye taarifa sahihi unakuwa na uwezo mkubwa wa kufanikiwa kwenye unachofanya.Je ni taarifa gani unapokea au unaingiza ? Chanzo chako cha taarifa ni kipi? Ukipatia majibu hakika hautabakia hapo ulipo.

Mtu mwenye nidhamu,
Mtaalamu wa mafanikio na mjasiriamali mkubwa Jim Rhon aliwahi kusema "nidhamu binafsi ndiyo daraja la malengo( goals)na unapokwenda")(destination)
Nidhamu ni sifa muhimu sana  kwa mjasiriamali kwani itamtenga na mambo mengi yasiyokuwa na umuhimu. Ni lazima mjasiriamali awe na nidhamu ya maswala kama vile matumizi ya muda pamoja na pesa.
Mjasiriamali bora ni yule anayeweza  kujinyima na kukataa vitu vyote ambavyo havimwezeshi kufikia malengo yake.
Ndugu yangu mpendwa sijamanisha kujinyima kila kitu ,nachomanisha vitu ambavyo havikufikishi kwenye malengo yakob.Simamia nidhamu yako kwa kutumia muda vizuri,Maana muda uliopoteza hauwezi kujirudia.
Upande wa Pesa unahitaji nidhamu ya hali ya juu sana maana walio wengi hapo pana wasumbua,heshimu sana kilicho kwenye ratiba au kipaombele hakika utakuwa mjasiriamali bora zaidi.Nidhamu yako bora mafanikio yako.

Mtu mwenye uvumilivu,
Kuna ukweli usiopingika kwamba kila jambo lina changamoto zake katika kulitenda. Ujasiriamali una changamoto nyingi ambazo zinahitaji uvumilivu ili kuzimudu na kuyafikia malengo uliyopanga.

Naomba niishie hapo tukutane wakati ingine.
Kwa mawasiliano 0767702659 Lackius Robert. Karibu.

Monday, September 16, 2019

Sifa za mjasiriamali bora

MORNING MOTIVATION DIARY

Ujasiriamali na mafanikio

Ndugu
Karibu katika siku nyingine tulivu kwenye morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.

Ujasiriamali ni uwezo wa kukabiliana na changamoto za kiuchumi zinazojitokeza na kugeuza au kutumia changamoto hizo kama fursa.
Mjasiriamali anabuni bidhaa mpya au njia mpya ya uzalishaji wa bidhaa ambayo soka linahitaji bidhaa hiyo au huduma hiyo ambayo haijapata kusambazwa hapo kabla.
Nikumbushe ndugu yangu mpendwa Ili kubobea katika ujasiriamali unatakiwa kuwa MJASIRI Pamoja na kutumia vizuri MALI ULIZONAZO.Kwa kufanya hivyo utakuwa umekamilisha neno zima la MJASIRIAMALI.
mfano katika mtaa au eneo fulani  kuna shida kubwa ya maji basi mjasiriamali atakabiliana changamoto hiyo kwa kuchimba kisima cha maji na hatimaye atakuwa ametatua changamoto hiyo ya maji na kugeuza kuwa fursa.Ambapo atakuwa anawauzia watu maji lakini wakati huo huo anapata kiasi fulani cha fedha.

Kwa hakika ujasiriamali ni chaguo muhimu sana kwenye karne hii ya sasa ili kujiongezea kipato zaidi na zaidi.
Wataalamu wanasema.
 “Siri ya mafanikio yeyote ni kutokukata tamaa katika kazi tunazofanya".Jaribu kuangalia wajasiriamali wadogo wadogo jinsi wanavyofanya kazi bila kujali mazingira yakoje wanavyofanikiwa.Kina mama wauza mbogamboga,migahawa ,watu wanaouza bidhaa za kutembeza wanapata Pesa.Unapochagua kuwa mjasiriamali haupaswi kuwa mtu wa kuyumbishwa na kuendeshwa na watu bali kile unachoona jamii inaweza kunufaika nacho.
Zijue sifa za mjasiriamali
Ili kuwa Mjasiriamali bora /au kujiboresha mwenyewe katika ujasiriamali wako ,sifa zifuatazo ni muhimu kuzifatria na kuzijua kwa undani:

1.Uwezo mkubwa wa kuona fursa na kuifanya kazi,
Mjasiriamali mzuri ni vizuri uwe na jicho la kuona fursa au kuona kitu gani kinahitajika  katika jamii inayokuzunguka.Ndio maana Muasisi wa fursa Lughe Mutahaba aliwahi kusema "Matatizo yetu ndio fursa zenyewe".
 Mjasiriamali ni vema kuziangalia changamoto zinazojitokeza katika jamii yako na kutumia changamoto hiyo kama fursa kwako. Kwa mfano sehemu unayokaa watu wanauhitaji wa huduma za kibenki kama vile (tigo pesa, m-pesa ,airtel money )ukifungua kibanda tayali tatizo umelitatua na umejitengenezea fursa,Mahitaji muhimu ya kutumia nyumbani katika mapishi.Bidhaa za urembo ,dukani kama mafuta vyakula n.k.

2.Unahitaji kuwa mbunifu,UBUNIFU  naweza sema ni  matumizi ya njia bora zaidi zinazokidhi kutatua changamoto mpya, changamoto ambazo tayari zipo lakini hazijapatiwa ufumbuzi bado, au changamoto zilizopo kwenye soko au jamii kwa kipindi husika.Dhana hii hutimilika pale ambapo bidhaa, huduma, teknolojia, mpangilio  wa biashara au njia nyingine yoyote inayoweza kutatua changamoto husika.Unaweza kubuni kitu kipya au kuboresha kilichopo,
Kama mjasiriamali yakupasa uwe mbunifu ,hata kwa bidhaa au huduma ambayo wanaokuzunguka wanayo ,unajaribu kutengeneza utofauti fulani .Kitu kinachomfanya mtu kuja kuchukua bidhaa kwako na sio kwa mwingine kama ni una kibanda cha chips mfano ,mandazi ,chapati au mgahawa,genge, n.k .

Hali hiyo inamfanya mteja kurudi ,Sam Walton ambaye ni mwanzilishi wa  WalMart anasema "Hakuna bosi kama mteja" kwa sababu ndiye anayetulipa hivyo ni jukumu lako kubuni namna ya kumshawishi katika bidhaa au huduma yoyote unayotoa. Nikukumbushe ndugu yangu '''Ubunifu wako ndio mafanikio yako'''.

3.Mtu anayependa kuongeza jitihada katika kutenda (practice),
Mara nyingi ujasiriamali mzuri ni ule wa vitendo,pamoja na kubadilisha mawazo (ideas) kuwa vitendo halisi. Hivyo mjasiriamali ni mtu anaechukua hatua na kutenda bila kujali vikwazo pia hachoki wala kukata tamaa.
Anaposhindwa hili hufanya lile au hubadilisha mbinu ili kufikia malengo aliyokusudia.
Ukijaribu kuangalia watu wengi wanayo mawazo mengi mazuri lakini inapofika wakati wa utendaji kama ni kuanzisha duka ,genge ,mgahawa ndipo utata unapoanzia sababu zinakuwa nyingi.Mara oh kuna mchakato Fulani nausikilizia ,Mipango haijakaa sawa au anasubilia ukamilifu wa kitu Fulani ndo aanze.Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa kesho imewaponza wengi,Anza leo ,majasiriamali bora ni yule anayekubali kuingia katika utendaji sio maneno na sababu nyingi ,Jiulize kama kesho sijui inavyofanana kwa nini nisianze?.

4.Mtu mwenye anayeweka malengo ,Kuna usemi unaosema "" kama hujui unapokwenda basi popote wewe unakuwa umefika""
Ili kujiboresha zaidi mjasriamali bora huweka malengo ya nini anataka afanye kwa muda fulani .
Ninaamini na wewe ndugu yangu mpendwa ambaye ni mjasiriamali kuna malengo umeyaweka.Faida kubwa ya kuweka malengo ni kwamba inakusaidia kukupa mwongozo(guideline) na kufanya uachane na vitu amabavyo sio vya msingi au vilivyopo nje ya malengo.

Malengo anayoweka huwa  ni ya muda mfupi (short term goals ) na  ya muda mrefu (long term goals) baada ya kuyaweka huwa anajituma zaidi ili kuyakamilisha malengo hayo.
Malengo hayo lazima yawe makubwa yanayoweza kufikika yasiwe madogo yanayoweza kukufanya kuwa MZEMBE wala yasiwe makubwa sana yasiyofikika. Kama wengi tunavyojua mafanikio ni mchakato.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Naomba niishie hapo tukutane wakati mwingine.
Lackius Robert unaweza kuwasiliana na Mimi kupitia 0767702659.



Wednesday, September 11, 2019

Mti kukua vizuri unahitaji ukomavu

MORNINGS MOTIVATION DIARY

Ili mti uzae vizuri mizizi inahitaji ukomavu na maji.

Ndugu,
Karibu katika siku nyigine tena ambapo tunakuatana katika program ya morning motivation diary ,yenye lengo kubwa la kukuongezea maarifa na kuing'alisha asubuhi yako.

Katika maisha yetu ya kila siku ili kuwa na ufanisi mzuri katika shughuli tunazofanya tunahitaji kuwa na ukomavu mzuri.Ukomavu unaoendana na maarifa ya kutosha katika kile tunachofanya.

Ukiangalia fishing law inasema "kamwe huwezi kupata samaki wakubwa katika sehemu yenye kina kifupi" .Hivyo basi ili tuwe na ukomavu mzuri katika shughuli tunazofanya na kutimiza malengo yetu .Lazima tupanue mawazo na kuanza kuwa na ndoto kubwa.

Maana Ukiwaza kidogo utapata kidogo,
Ukiwaza kikubwa utapata kikubwa maana mwili,akili,fikra zako zote zinawaza kikubwa na hautachoka.Lakini ukiwaza kidogo ndivyo mwili utakavyolegea maana kitu kidogo mara nyingi ni cha muda mfupi.

Mti mdogo mizizi yake hata umwage maji mengi kiasi gani haiwezi kwenda mbali sana lakini mti mkubwa mizizi yake husambaa na kwenda mbali zaidi.

Usisubili upewe kila kitu ndo ufanye jambo,Imwagilie akili yako kwa kuendelea kujifunza kitu kipya kila siku.
Anza na kidogo vingine vitakukuta njiani.Usiwe na mawazo kama ya  mtu anayesema kama napewa maziwa kila siku yanini kufuga Ng'ombe'''.Anaamini siku zote ataendelea kupewa ,anashindwa kuwaza yajayo anawazia yaliyopo na yanayoonekana mbele yake.
Wish you all the best.

 " Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa ".

Nikukaribishe ili uzidi kujifunza zaidi na zaidi pia tembelea page yangu ya Instagram jina lackius Robert.Karibu