Saturday, June 01, 2019
Tafakari kuhusu tathimini
Tafakari kuhusu tathimini
Ndugu,karibu katika blog hii ya daraja la
mafanikio yenye lengo la kukuongezea maarifa zaidi katika kuyafikia malengo yako.
Siku ya leo napenda kuchukua wasaa huu kukumbusha kufanya tathimini katika malengo uliyoweka.Katika kipindi chote cha mwaka 2019 ili kujua yalipofikia.
Lengo la kufanya tathimini ni kutaka kujua ulipotoka,ulipo na unapoelekea katika kuyafanikisha malengo uliyoweka. Ni ngumu sana wewe kufikia malengo uliyojiwekea bila kufanya tathimini maana utaona changamoto ni zile zile .
Huoni mabadiliko yoyote na Unashangaa siku,miezi inaenda bila kupiga hatua yoyote au uko palepale au hatua kidogo ndo umepiga.
Nikumbushe kuwa bado haujachelewa kufanya tathimini .Lakini pia inakusaidia kujua vitu gani umekamilisha, vitu gani hujakamilisha, na vitu gani unategemea kuvikamilisha.
Tathimini inakusaidia kujua vizuizi vya vinavyokuzonga au kukukwamisha kukamilisha malengo yako.Kwa kuweza kuvitambua je vizuizi hivuo ni muda,watu, ni mtaji ? Au kwa kufanya tathimini utaweza kutambua kipi ni kizuizi zaidi. Pia utatafuta mbinu za kutatua vizuizi hivyo.
Usisubilie ufanye kesho maana KESHO inaandaliwa na bwana mmoja aitwaye LEO. Huyu LEO unatembea naye popote unapokwenda lakini KESHO atabiliki hata kidogo.
Ili kuweza kuyafikia makubwa unahitaji kubadilika ,Mwezi mpya na mabadiliko mapya anza kwa kufanya tathimini.
Jicho lako lielekeze palipoandikwa tathimini hii hapa.
Usiangalie wanaongea nini kuhusu mipango yako bali angalia unataka nini kwenye maisha yako.
"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".
Karibu.
Kupata post zilizopita follow on Instagram page
@ lackiusrobert
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment