Tuesday, June 04, 2019
Jinsi ya kuishinda hofu ya kushindwa season III
Jinsi ya kuishinda hofu ya kushindwa season III
Ndugu,
Karibu katika sehemu ya tatu na ya mwisho katika jinsi ya kuishinda hofu ya kushindwa.
=•Uvumilivu,
Watu wote waliofanikiwa wamekuwa na uvumilivu mkubwa maana ,Hofu haianzi siku moja bali inaweza kujengwa kwa siku kadhaa kuendana na mazingira watu wanaoukuzunguka n.k .
Mfano watu waliokuzunguka wanaweza kukwambia hawezi,wakakudharau ukiwasikiliza yote wanayosema tayali hofu itakuwa kubwa.
Mara nyingi unapokuwa na uvumilivu pia imani yako tayari inakuwa na falsafa ya ushindi.Yapo mambo magumu yanakutokea lakini kwa tayali subconscious mind yako inakuwa na positive thinking kitu kinachokupeleka katika ushindi.
Kumbuka safari ndefu aijuaye msafiri Uvumilivu katika safari ya mafanikio ni wa msingi sana.Elly David finest speaker aliwahi kusema 'Uvumilivu siku zote unakupa kilicho bora'.
Ukiishinda hofu ya kushindwa hakika utapata mafanikio bora.
=•Kujaribu ,
kutokana na changamoto unazopitia njia bora ni kujaribu kufanya jambo ambalo unawiwa nalo mfano biashara ,kuanzisha familia, n.k na unaposhindwa jaribio usione kama umefika mwisho jaribu tena.
Mfano wanasayansi waga hawakubali kufanya jaribio mara moja, bali wanafanya mara kadhaa ili kuona majibu ya majaribio.
Mfano Thomas Edison mgunduzi maswala ya umeme(bulb) alifanya majaribio zaidi ya 1000 licha ya kwamba yote yalikuwa yanagoma lakini aliendelea mpaka akafanikiwa kushinda kuanzia 1001.Kuna wakati najiuliza je angeishia jaribio la 100 ingekuwaje ?.
Kumbuka,Unapoanza kitu kipya unaweza ukashindwa Mara kadhaa lakini ni vema kujipa moyo kujaribu kufanya na unafanikiwa.
Jaribu Jaribu Jaribu Tena Wish all the best.
"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".
Karibu katika page yangu ya katika page yangu ya instagram lackius Robert.
Pia kwa maoni Maarifarobert@gmail.com.
Karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment