Monday, June 03, 2019

Jinsi ya kiishinda hofu ya kushindwa



Jinsi ya kuishinda hofu ya kushindwa season II

=•Kujiamini,
 Mafanikio ya kweli yanaanzia moyoni mwako .Siku zote Ukitaka kumshinda adui yako, hakikisha unamfanya apunguze kujiamini .Hali hiyo inamfanya akose mwamko au msukumo katika kufanya jambo.

Hivyo kwa kujiamini unakuwa na nguvu na mwamko kutoka akilini mwako hata viungo vingine vya mwili pia vinakuwa active katika kupambana hofu hiyo.
Watu wasio jiamini siku zote huwa hawapati wanayostahili,bali  inafanya wanaishia kutamani.
Mfano mzuri kwa mwandishi na mhamasishaji Rodrick Nabe kabla ya miaka ya 2016,alikuwa anafanya kazi zake za ufundishaji shuleni,
Lakini kuna kitu alikuwa anaona akiendi sawa hasa hasa katika kipato.

Baadae akaja kugundua kuna kitu inabidi afanye kinaweza kuwa na mabadiliko makubwa kwenye maisha na malengo pia.Ndipo akaanzisha road to success kwa maana  ya kutoa mafundisho mbalimbali.
Aliweza kujiamini licha ya kwamba safari ilikuwa na changamoto kibao lakini hakuwa na hofu yoyote ya kushindwa.
Mpaka sasa amegusa maisha ya wengi nikiwemo Mimi pia na wewe msomaji kwa namna moja ama nyingine. Ata wewe unaouwezo mkubwa wa kufanya makubwa kama ukijiamini.

=• Kutokata tamaa,
 Mwandishi na mhamasishaji Joel Nanauka aliwahi kuwa katika nafasi za chini sana kimasomo hali hiliyompelekea kudharauliwa na kila mmoja ikiwemo walimu wake.Mfariji mmoja tu amabaye ni mama yake ndiye aliyemwambia unaweza kila jambo endapo autakata tamaa. Ilikuwa ni amazing pale aliposhika nafasi ya kwanza darasani mpaka kila mmoja akawa anamyoshea kidole amewezaje kufika pale.
Ni kweli yapo makubwa unataka kuyafanya lakini ,kwa kuyaangalia na kuyafikilia unaona auwezi hadi unakata tamaa.

Hali hiyo usipoivua hautaweza kusogea kamwe utabaki pale pale siku zote.Washindi wote hawakuta tamaa mwishowe wakaishinda hofu ya kushindwa.
Itaendelea sehemu ya tatu na ya mwisho kuhusu mada hii wish you nice day

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Karibu
Kupata ujumbe zaidi follow on Instagram page lackius Robert
Email Maarifarobert@gmail.com.
Asante.

No comments:

Post a Comment