MORNING MOTIVATION DIARY
Binadamu hatujakamilika.
Ndugu karibu katika siku nyingine tena natumaini unaendelea kufutahia makala nzuri.
Ni kweli kwamba hakuna binadamu aliyekamilika kila mmoja analopungufu lake ambalo ni tofauti kabisa na mwingine.Tutumie muda wetu kujenga madaraja ya mafanikio badala ya vikwazo katika mahusiano yetu.
Alikuwepo kijana mmoja mzuri,mwenye busara,hekima, akili kila mmoja alitamani sana kuwa karibu na yeye.Licha ya kuwa na sifa zote hizo lakini alikuwa na hasira sana kiasi kwamba alikuwa anashindwa kuzizuia.
Baba yake alifikiria jambo moja kubwa la kumsaidia mwanae .Akaandaa misumari mingi ili mwanae akipata hasira achukue misumari na kuigonga kwenye moja ya geti lililokuwa nyumbani kwao.
Aliendelea kufanya hivyo siku hadi siku pindi anapopata hasira ,mwishowe zikaenda zinapungua.Akamwambia baba yake kuwa anashukuru maana hasira zimepungua .
Baba alimwambia haijalishi kinachotokea tangu sasa lakini uzio huu hautakuwa sawa siku zote.
Haijalishi mara ngapi unasema pole, au miaka ngapi inapita, kovu bado itakuwapo. Na jeraha ya maneno ni mabaya uliyowafanyia watu litakuwepo licha ya kwamba umeomba msamaha.
Watu ni thamani zaidi kuliko uzio wa zamani ,wanakufanya utabasamu wanakusaidia kufanikiwa. Wengine watakuwa marafiki ambao wanashiriki furaha zako na kukusaidia kupitia nyakati mbaya. Na ukiwa umekosa tumaini watakupa, watakufungua pia moyo wako.
Tunahitaji kuepuka makovu mengi kwa wengine katika maisha yetu ya kila siku .
"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"
Karibu pia katika page ya Instagram lackiusrobert
Wish you all the best.

No comments:
Post a Comment