Sunday, March 24, 2019

UMUHIMU WA KUWA FURAHA


Furaha ni utulivu ulio ndani ya nafsi ya mtu mwenyewe,mara nyingi msingi wa Furaha uleteleza utulivu wa Mwili na Roho ambavyo uleta matumaini na upendo kwa ndani ya nafsi ya mtu.
Wakati mwigine ili kuipata  vema  kukaa na watu wanaokupa furaha na kufanya mambo yanayokupa furaha, . Watu wengi wanakosa furaha na amani na kujaa na msongo wa mawazo katika maisha yao ya kila siku hasa makazini, majumbani, kifamilia.
Kama unaamini kuwa unakosa furaha kutokana na ugumu wa maisha, haujapata kazi, unasumbuliwa na mahusiano, umefeli kwenye masomo, umetengwa kwenye familia, unatafuta mtoto lakini hupati na mengine kadha wa kadha inabidi  ubadilike kwani hata ukifanikiwa kuvipata vitu hivyo unavyovihitaji kamwe furaha yako haiwezi kukamilika kutoka na tabia za asili za binadamu.

Msomaji wa BLOG Hii Naomba nikushirikishe kidogo umuhimu kwa kuwa na furaha maishani;
 Kuwa na furaha kunalinda moyo wako
Utafiti unaonesha kuwa asili ya upendo na furaha siyo moyoni lakini husaidia kuulinda huku ikibainika kuwepo kwa uhusiano baina ya furaha na vipimo vingine vya afya ya moyo kama vile muda unaotumika wakati wa pigo moja la moyo na lingine na kuzilinganisha na hatari kadhaa za magonjwa ya moyo.
Furaha huzuia mkazo
Makazo yaani sterss hausababishi matatizo ya kisaikolojia pekee bali pia husababisha mabadiliko ya kibiology katika homoni zetu na shinikizo la damu. Furaha inatajwa kupoza hasira za athari hizi na wakati mwingine kutusaidia kurudi katika hali ya kawaida kwa haraka.

VITU VYA KUEPUKA
Hali ya kukata tamaaa,
Walio wengi hali hii imetukumba sana na tumeikosa furaha lakini ili  uweze kuwa na furaha ya kudumu epuka kukata tamaa au kukatishwa tamaa na mtu, kwa sababu kitendo cha kuruhusu kukataa tamaa ni hatua ya mwisho ambayo hauna uwezo wowote wa kujitoa.Kamwe usiruhusu hali hiyo jitahidi kuishi kwenye mtazamo chanya muda wote kuwa utafanikiwa kila jambo unalopigania hata kama ukifeli usikate tamaa utayashinda.
Epuka kutoridhika,
Katika maisha hakuna hatua ambayo mwanadamu utafika na kusema kuwa umeridhika kwa maana hata mwandamu apewe kitu gani hakuna wakati atakaposema inatosha.Wengi wamepoteza furaha kutokana na kutoridhika,akipata kitu hiki anataka kingine . Simaanishi watu waridhike  nachomanisha kiridhika na unachokipata kutegemeana na hali ya kipato chako.Mfano kama auna uwezo wa kunua gari na unatarajia upate furaha baada ya kupata gari itachukua muda hio furaha yako kuipata kama ukifeli usikate tamaa utayashinda.

Ni matumaini yangu kwamba umeweza kuongeza kidogo uelewa namna furaha ilivyo bora katika maisha yetu.
Kauli za washindi nikwamba hawakubali kuikosa furaha .Je mimi na wewe tunaikosaje kwa mfano?.
''Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa''
Kwa maoni na ushauri maarifarobert@gmail.com
Instagram @lackiusrobert
KARIBU.


No comments:

Post a Comment