MOTIVATION DIARY
Jinsi ya kuishinda hofu ya kushindwa, Season 1
Ndugu,karibu
Ni siku nyingine tena tunakutana katika motivation diary yenye lengo la kufanya siku yako kuonekana murua.
Siku ya Leo naomba nikushirikishe maelezo ya kina juu ya kuishinda hofu ya kushindwa.
Hofu naweza ifananisha na hisia zilizolala,kwa maana muda wowote zinaweza kuamka.
Neno hofu linatumika katika nyanja tofauti mfano kuwa na hofu ya mungu,kwamba nikifanya kitu hiki mh! Si itakuwa ni dhambi n.k.
Ukiachana hiyo hofu kubwa miongoni mwa wengi ni katika hatua ya kufikia mafanikio.
Hapo ndipo hofu ya kushindwa inapoanzia.
Hofu sio kwamba ni mbaya muda wote maana kuna wakati inasaidia katika kupata positive impact.
Bali hofu mbaya ni yenye negative impact.
Ninapozungumzia hofu ya kushindwa hiyo iko katika negative way.
Najua kazi kubwa uliyonayo kwenye safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio yako ni kuishinda hofu ya kushindwa.
Maana hofu hiyo ndicho kikwazo kikubwa cha ndani yako, ambacho kama hutakivua, hutaweza kujaribu mambo makubwa.Utajawa na woga wasiwasi kwa kila unachojaribu kufanya iwe biashara,kuboresha mahusiano,kuanzisha familia n.k
Hakuna mtu ambaye hana hofu kabisa, kila mtu anakutana na hofu mbalimbali, lakini kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa ni jinsi wanavyozikabili hofu zao.
Wanaoshindwa wanachukua hofu kama kikwazo, na kwa kuwa hawataki kuonekana wakishindwa au hawataki lawama, basi hawachukui hatua yoyote.
Wanaoshinda wanaiona hofu kama mrejesho kwamba wanajaribu kitu kikubwa, hivyo wanachukua hatua na hofu hiyo inapotea.
Nini kifanyike au hatua gani zichukuliwe ili kuishinda hofu ya kushindwa karibu katika sehemu itakayofata.
Siku zote naamini wewe ni mshindi na thamani yako ni kubwa na utabaki kuwa juu maana
"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".
Karibu pia katika ukurasa wangu wa Instagram
Lackius Robert
Maarifarobert@gmail.com.
No comments:
Post a Comment