Sunday, June 09, 2019
Faida za neno asante
Mwambie Asante
Karibu,
Siku ya Leo nikushirikishe tatafakri kuhusu neno asante.
Asante ni neno la kuwashukuru watu wengine kwa kizuri ambacho wamefanya kwa ajili yako.
Unapomwambia asante mtu anaamini unamjali lakini pia huonesha jinsi gani umemheshimu kwa kizuri alichokufanyia.
Ni neno dogo sana lenye herufi chache kulitamka kwake hakutumii sekunde nyingi,lakini huwa linaleta faraja kwa yule anayelisikia, hasa linapotolewa kwa uhalisia. Linamsukuma mtu kujituma zaidi,na zaidi katika kila kitu anachofanya.
Ni neno lenye ushawishi mkubwa, ambalo tunapaswa kulitumia sana kwenye maisha yetu.
Watu wengi wamekosa fursa mbalimblai kutoka na kushindwa kuonesha shukrani baada ya kufanyiwa kitu kizuri.
Unapomwambia mtu asante kuna hisia fulani hivi !!!!!! Yaani zinaonekana kuamka katika ubongo.Ili ujue kwamba unayemwabia amefurahia asante yako utaona tabasamu fulani au ishara fulani ya kutingisha kichwa kama ni(Face to face).
Kama ni kwa njia ya mazungumzo ya simu utajua pia kwa kusikia mwitikio.
Miongoni mwa faida ni kuimarisha mahusiano ,hali ambayo kama sio kutoweka.Pia linaongeza ufanisi katika sehemu za kazi,Mahusiano n.k .
Nikualike sehemu inayofatia ambapo nitaelezea Ni wakati gani unapaswa kusema asante.
Wish you all the best with favourable day.
"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"
Kupata mafunzo yaliyopita tembelea ukurasa wangu wa Instagram
Lackius Robert
Pia blog ya
https://darajalamafanikio.blogspot.com/?m=1
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment