Thursday, June 13, 2019

Afya yako ni muhimu kuliko kitu chochote

MORNING MOTIVATION DIARY



Kuwa makini na Afya yako.

Ndugu, ili uweze kufanikiwa katika jambo lote unalofanya ,Afya ikiwa bora una uwanja mkubwa wa kufanikisha.
Kuwa bora kimwili na kiakili ni ukweli usiopingika kwamba  unaweza kufanya chochote unachotaka.

Afya inakupa nguvu ,hamasa ,utulivu na uwezo wa kuyatenda yote unayoyahitaji.
Magonjwa ni mengi kuwa makini na afya yako.Hakuna mwingine wa kuilinda au kuitunza afya yako Kama si wewe mwenyewe,Tamaa ndogo ndogo zisiharibu ndoto zako za maisha yako.

N.B Wanasema' majuto ni mjukuu' ila ukitaka kumjua baba yake yakishatokea utamjua tu! Maana utaanza kuwaza na kuwazua kwa nini nilifanya vile? .Bora ningevumilia ona  sasa nilivyo nateseka ase!!! Lakini ndo yanakuwa tayali yametokea.

Mwenye nguvu muite power !!!!!!!

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Karibu Instagram lackiusrobert
Wish you all the best.

Wednesday, June 12, 2019

Binadamu hatujakamilika

MORNING MOTIVATION DIARY

Binadamu hatujakamilika.

Ndugu karibu katika siku nyingine tena natumaini unaendelea kufutahia makala nzuri.

Ni kweli kwamba hakuna binadamu aliyekamilika kila mmoja analopungufu  lake ambalo ni tofauti kabisa na mwingine.Tutumie muda wetu kujenga madaraja ya mafanikio badala ya vikwazo katika mahusiano yetu.

Alikuwepo kijana mmoja mzuri,mwenye busara,hekima, akili  kila mmoja alitamani sana kuwa karibu na yeye.Licha ya kuwa na sifa zote hizo lakini alikuwa na hasira sana kiasi kwamba alikuwa anashindwa kuzizuia.

Baba yake alifikiria jambo moja kubwa la kumsaidia mwanae .Akaandaa misumari mingi ili mwanae akipata hasira achukue misumari na kuigonga kwenye moja ya geti lililokuwa nyumbani kwao.

Aliendelea kufanya hivyo siku hadi siku pindi anapopata hasira ,mwishowe  zikaenda zinapungua.Akamwambia baba yake kuwa anashukuru maana hasira zimepungua .
Baba alimwambia haijalishi kinachotokea tangu sasa lakini uzio huu hautakuwa sawa siku zote.

Haijalishi mara ngapi unasema pole, au miaka ngapi inapita, kovu bado itakuwapo. Na jeraha ya maneno ni mabaya uliyowafanyia watu litakuwepo licha ya kwamba umeomba msamaha.

Watu ni thamani zaidi kuliko uzio wa zamani ,wanakufanya utabasamu  wanakusaidia kufanikiwa. Wengine watakuwa marafiki ambao wanashiriki furaha zako na kukusaidia kupitia nyakati mbaya. Na ukiwa umekosa tumaini watakupa, watakufungua pia moyo wako.

Tunahitaji kuepuka makovu mengi kwa wengine katika maisha yetu ya kila siku .

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Karibu pia katika page ya Instagram lackiusrobert

Wish you all the best.

Tuesday, June 11, 2019

Fanya kazi muhimu kwanza


Fanya kazi muhimu kwanza:

Watu wengi tumekuwa na kazi nyingi tunazofanya katika maisha yetu ya kila siku.Miongoni mwa wengi tumekuwa tukiishia njiani yaani kuacha kazi tunayofanya na kufanya nyingine,huku ya kwanza haijaisha,kwa maana aujafanya tathimini ya kwanini aujafanikiwa kama ulivyotarajia.

Hali hii imetufanya wengi kushindwa kuwa na mpangilio maalumu wa kazi hali hii ya tunaiita KUTANGATANGA

Mfano umenza biashara fulani ,lakini baada ya muda mfupi unaona anayeendesha bodaboda anapata Pesa zaidi ukaachana na biashara yako na kuingia kwenye kazi ya bodaboda .
Baada ya muda mfupi unaona bado aijakupatia fedha unazohitaji unaenda tena kwenye biashara nyingine mpya tofauti na mwanzo uliyofanya,Baada ya kuona aina umuhimu sana.

Mwisho wa siku unajikuta mambo yako yote hayaendi sawa baada ya hapo unaanza kulalamika .Nchi hii bhana bora ningezaliwa Nje nikawa tajiri.Nikukumbushe """" Kuwa karibu na mahakama sio kujua sheria"""".Hivo kuzaliwa Nchi tajiri bado hakukufanyi kuwa tajiri Bali utajiri inaanzia kwenye nafsi na mawazo yako.Naomba Ubadilike maana

" Ushindi upo mikononi mwako kwa Kuwa umebarikiwa"

For more
Karibu katika page yangu ya Instagram
Lackius robert

Sunday, June 09, 2019

Faida za neno asante



Mwambie Asante

Karibu,
Siku ya Leo nikushirikishe tatafakri kuhusu neno asante.

Asante ni neno la kuwashukuru watu wengine kwa kizuri ambacho wamefanya kwa ajili yako.

Unapomwambia asante mtu anaamini unamjali lakini pia huonesha jinsi gani umemheshimu kwa kizuri alichokufanyia.

Ni neno dogo sana lenye herufi chache kulitamka kwake hakutumii sekunde nyingi,lakini huwa linaleta faraja kwa yule anayelisikia, hasa linapotolewa kwa uhalisia. Linamsukuma mtu kujituma zaidi,na zaidi katika kila kitu anachofanya.

Ni neno lenye ushawishi mkubwa, ambalo tunapaswa kulitumia sana kwenye maisha yetu.

Watu wengi wamekosa fursa mbalimblai kutoka na kushindwa kuonesha shukrani baada ya kufanyiwa kitu kizuri.

Unapomwambia mtu asante kuna hisia fulani hivi !!!!!! Yaani zinaonekana kuamka katika ubongo.Ili ujue kwamba unayemwabia amefurahia asante yako utaona tabasamu fulani  au ishara fulani ya kutingisha kichwa kama ni(Face to face).
Kama ni kwa njia ya mazungumzo ya simu utajua pia kwa kusikia mwitikio.

Miongoni mwa faida ni kuimarisha mahusiano ,hali ambayo  kama sio kutoweka.Pia linaongeza ufanisi katika sehemu za kazi,Mahusiano n.k .

Nikualike sehemu inayofatia ambapo  nitaelezea Ni wakati gani unapaswa kusema asante.

Wish you all the best with favourable day.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kupata mafunzo yaliyopita tembelea ukurasa wangu wa Instagram
Lackius Robert
Pia blog ya
https://darajalamafanikio.blogspot.com/?m=1

Tuesday, June 04, 2019

Jinsi ya kuishinda hofu ya kushindwa season III



Jinsi ya kuishinda hofu ya kushindwa season III

Ndugu,
Karibu katika sehemu ya tatu na ya mwisho katika jinsi ya kuishinda hofu ya kushindwa.

=•Uvumilivu,
Watu wote waliofanikiwa wamekuwa na uvumilivu mkubwa maana ,Hofu haianzi siku moja bali inaweza kujengwa kwa siku  kadhaa kuendana na mazingira watu wanaoukuzunguka n.k .
Mfano watu waliokuzunguka wanaweza kukwambia hawezi,wakakudharau ukiwasikiliza yote wanayosema tayali hofu itakuwa kubwa.
Mara nyingi unapokuwa na uvumilivu pia  imani yako tayari inakuwa na falsafa ya ushindi.Yapo mambo magumu yanakutokea lakini kwa tayali subconscious mind yako inakuwa na positive thinking kitu kinachokupeleka katika ushindi.
Kumbuka safari ndefu aijuaye msafiri Uvumilivu katika safari ya mafanikio ni wa msingi sana.Elly David finest speaker aliwahi kusema 'Uvumilivu siku zote unakupa kilicho bora'.
Ukiishinda hofu ya kushindwa hakika utapata mafanikio bora.

=•Kujaribu ,
kutokana na changamoto unazopitia njia bora ni kujaribu kufanya jambo  ambalo unawiwa nalo mfano biashara ,kuanzisha familia, n.k na unaposhindwa jaribio usione kama umefika mwisho jaribu tena.
Mfano wanasayansi waga hawakubali kufanya jaribio mara moja, bali wanafanya mara kadhaa ili kuona majibu ya majaribio.

Mfano  Thomas Edison  mgunduzi maswala ya umeme(bulb) alifanya majaribio zaidi ya 1000 licha ya kwamba yote yalikuwa yanagoma lakini aliendelea mpaka akafanikiwa kushinda kuanzia 1001.Kuna wakati najiuliza je angeishia jaribio la 100 ingekuwaje ?.

Kumbuka,Unapoanza kitu kipya unaweza ukashindwa Mara kadhaa lakini ni vema kujipa  moyo kujaribu kufanya na unafanikiwa.
Jaribu Jaribu Jaribu  Tena Wish all the best.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".
Karibu katika page yangu ya katika page yangu ya instagram lackius Robert.

Pia kwa maoni Maarifarobert@gmail.com.
Karibuni.

Monday, June 03, 2019

Jinsi ya kiishinda hofu ya kushindwa



Jinsi ya kuishinda hofu ya kushindwa season II

=•Kujiamini,
 Mafanikio ya kweli yanaanzia moyoni mwako .Siku zote Ukitaka kumshinda adui yako, hakikisha unamfanya apunguze kujiamini .Hali hiyo inamfanya akose mwamko au msukumo katika kufanya jambo.

Hivyo kwa kujiamini unakuwa na nguvu na mwamko kutoka akilini mwako hata viungo vingine vya mwili pia vinakuwa active katika kupambana hofu hiyo.
Watu wasio jiamini siku zote huwa hawapati wanayostahili,bali  inafanya wanaishia kutamani.
Mfano mzuri kwa mwandishi na mhamasishaji Rodrick Nabe kabla ya miaka ya 2016,alikuwa anafanya kazi zake za ufundishaji shuleni,
Lakini kuna kitu alikuwa anaona akiendi sawa hasa hasa katika kipato.

Baadae akaja kugundua kuna kitu inabidi afanye kinaweza kuwa na mabadiliko makubwa kwenye maisha na malengo pia.Ndipo akaanzisha road to success kwa maana  ya kutoa mafundisho mbalimbali.
Aliweza kujiamini licha ya kwamba safari ilikuwa na changamoto kibao lakini hakuwa na hofu yoyote ya kushindwa.
Mpaka sasa amegusa maisha ya wengi nikiwemo Mimi pia na wewe msomaji kwa namna moja ama nyingine. Ata wewe unaouwezo mkubwa wa kufanya makubwa kama ukijiamini.

=• Kutokata tamaa,
 Mwandishi na mhamasishaji Joel Nanauka aliwahi kuwa katika nafasi za chini sana kimasomo hali hiliyompelekea kudharauliwa na kila mmoja ikiwemo walimu wake.Mfariji mmoja tu amabaye ni mama yake ndiye aliyemwambia unaweza kila jambo endapo autakata tamaa. Ilikuwa ni amazing pale aliposhika nafasi ya kwanza darasani mpaka kila mmoja akawa anamyoshea kidole amewezaje kufika pale.
Ni kweli yapo makubwa unataka kuyafanya lakini ,kwa kuyaangalia na kuyafikilia unaona auwezi hadi unakata tamaa.

Hali hiyo usipoivua hautaweza kusogea kamwe utabaki pale pale siku zote.Washindi wote hawakuta tamaa mwishowe wakaishinda hofu ya kushindwa.
Itaendelea sehemu ya tatu na ya mwisho kuhusu mada hii wish you nice day

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Karibu
Kupata ujumbe zaidi follow on Instagram page lackius Robert
Email Maarifarobert@gmail.com.
Asante.

Sunday, June 02, 2019

Jinsi ya kishinda hofu ya kushindwa season I

MOTIVATION DIARY

Jinsi ya kuishinda hofu ya kushindwa, Season 1

Ndugu,karibu
Ni siku nyingine tena tunakutana katika motivation diary yenye lengo la kufanya siku yako kuonekana murua.

Siku ya Leo naomba nikushirikishe maelezo ya kina juu  ya kuishinda hofu ya kushindwa.

Hofu naweza ifananisha na hisia zilizolala,kwa maana muda wowote zinaweza kuamka.
Neno hofu linatumika katika nyanja tofauti mfano kuwa na hofu ya mungu,kwamba nikifanya kitu hiki mh! Si itakuwa ni dhambi n.k.

Ukiachana hiyo hofu kubwa miongoni mwa wengi ni katika hatua ya kufikia mafanikio.
Hapo ndipo hofu ya kushindwa inapoanzia.

Hofu sio kwamba ni mbaya muda wote maana kuna wakati inasaidia katika kupata positive impact.

Bali hofu mbaya ni yenye negative impact.
 Ninapozungumzia hofu ya kushindwa hiyo iko katika negative way.

Najua kazi kubwa uliyonayo kwenye safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio yako ni kuishinda hofu ya kushindwa.
Maana  hofu hiyo ndicho kikwazo kikubwa cha ndani yako, ambacho kama hutakivua, hutaweza kujaribu mambo makubwa.Utajawa na woga wasiwasi kwa kila unachojaribu kufanya iwe biashara,kuboresha mahusiano,kuanzisha familia n.k

Hakuna mtu ambaye hana hofu kabisa, kila mtu anakutana na hofu mbalimbali, lakini kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa ni jinsi wanavyozikabili hofu zao.

Wanaoshindwa wanachukua hofu kama kikwazo, na kwa kuwa hawataki kuonekana wakishindwa au hawataki lawama, basi hawachukui hatua yoyote.

Wanaoshinda wanaiona hofu kama mrejesho kwamba wanajaribu kitu kikubwa, hivyo wanachukua hatua na hofu hiyo inapotea.

Nini kifanyike au hatua gani zichukuliwe ili kuishinda hofu ya kushindwa karibu katika sehemu itakayofata.

Siku zote naamini wewe ni mshindi na thamani yako ni kubwa na  utabaki kuwa juu maana

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Karibu pia katika ukurasa wangu wa Instagram
Lackius Robert
Maarifarobert@gmail.com.

Saturday, June 01, 2019

Tafakari kuhusu tathimini



Tafakari kuhusu tathimini

Ndugu,karibu katika blog hii ya daraja la
mafanikio yenye lengo la kukuongezea maarifa zaidi katika kuyafikia malengo yako.

Siku ya leo napenda kuchukua wasaa huu kukumbusha kufanya tathimini katika malengo uliyoweka.Katika kipindi chote cha mwaka 2019 ili kujua yalipofikia.

Lengo la kufanya tathimini ni kutaka kujua ulipotoka,ulipo na unapoelekea katika kuyafanikisha malengo uliyoweka. Ni ngumu sana wewe kufikia malengo uliyojiwekea bila kufanya tathimini maana utaona changamoto ni zile zile .
Huoni mabadiliko yoyote na  Unashangaa siku,miezi inaenda bila kupiga hatua yoyote au uko palepale au hatua kidogo ndo umepiga.

Nikumbushe kuwa bado haujachelewa kufanya tathimini .Lakini pia inakusaidia kujua vitu gani umekamilisha, vitu gani hujakamilisha, na vitu gani unategemea kuvikamilisha.

Tathimini inakusaidia kujua vizuizi vya vinavyokuzonga au kukukwamisha kukamilisha malengo yako.Kwa kuweza kuvitambua je vizuizi hivuo ni muda,watu, ni mtaji ? Au kwa kufanya tathimini utaweza kutambua kipi ni kizuizi zaidi. Pia utatafuta mbinu za kutatua vizuizi hivyo.

Usisubilie ufanye kesho maana KESHO inaandaliwa na bwana mmoja aitwaye LEO. Huyu LEO unatembea naye popote unapokwenda lakini KESHO atabiliki hata kidogo.

Ili kuweza kuyafikia makubwa unahitaji kubadilika ,Mwezi mpya na mabadiliko mapya anza kwa kufanya tathimini.

Jicho lako lielekeze palipoandikwa tathimini hii hapa.

Usiangalie wanaongea nini kuhusu mipango yako bali angalia unataka nini kwenye maisha yako.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Karibu.
Kupata post zilizopita follow on Instagram page
@ lackiusrobert