MIMI NI NANI
Karibu kabisa katika Juma la kwanza la mwaka 2019,Natumaini umzima unaendelea vizuri na majukumu yako.
Jambo la kwanza naomba tumshukuru Mungu kwa kutufanya kuuona mwaka 2019 ,wapo wengi walitamani sana kuuona lakini hawakuweza kuuona,wewe na mimi tunayo thamani kubwa mbele ya mwenyezi mungu ndio maana anazidi kutupatia uhai.
Katika ukurasa wako mpya wa kuhakikisha unafanikiwa, hakika huu ni mwaka wa mafanikio kwako nakukaribisha katika Blog hii ya DARAJA LA MAFANIKIO ili uweze kuyafahamu mambo mbalimbali amabyo unayajua au pengine ni mara yako ya kwanza kuyasikia.
Watu walio wengi wamekuwa wakijiuliza katika nafsi ya kwanza wao ni kina nani yaani .Mfano mimi nasema hivi MIMI NI NANI?.
Namimi pia nimejiuliza mara nyingi swali hili lakini nikajaribu kupitia pitia kurasa za maandishi mbali mbali ya watu tofauti tofauti nikaja kugundua kwamba mimi ni wa thamani kubwa sana maana akuna mtu ata mmoja katika ulimwengu huu mwenye upekee kama nilivyo mimi,Kuna kitu ninacho ambacho mungu amenipatia na hakuna yeyote wa kukiondoa isipokuwa yeye mwenyewe muumba.
Wengi tumekuwa tukitamani sana kuwa kama kina fulani mfano mchezaji furani wa mpira ,msanii fulani na hatimaye tumeanza kuyaiga wanayoyafanya.
Msomaji wa BLOG hii naomba nikuabarishe kwamba wewe ni wa pekee sana unao uwezo mkubwa tu wa kuyafanya makubwa katika ulimwengu huu,usiendelee kufikilia kwamba labda wakati wako bado ila unaweza kuwa sahihi lakini sio sana kama bado hujaanza kufanya bado haujachelewa .
Najua changamoto kubwa inayotukabili ni kwamba BADO TUNASHINDWA KUJUA ENEO NA WAKATI SAHIHI WA KUYAFANYIA MAMBO HAYO.Huu ni mwaka wa mafaikio fanya kazi kwa bidii katika sehemu uliopo kwa moyo wako wote utafanikiwa kuyaona mafanikio japo yanaanza kidogo lakini shukuru.
Nakusuhi uambatane na mimi wakati mwingine katika kuielezea mada hii.
karibu mimi ni Kiongozi lengo ni kukuvusha salama katika daraja na kuyafikia mafanikio.
''Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa''
Kwa maoni maarifarobert@gmail.com
Instagram @lackiusrobert.
KARIBU.
No comments:
Post a Comment