KARIBU KATIKA BLOG MPYA YA DARAJA MAFANIKIO.
Ni matumaini yangu kwamba hapo ulipo ni mzima wa afya,napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha katika blog hii mpya ya DARAJA LA MAFANIKIO ili tuweze kubadilishana mawazo kuhusu mada mbalimbali zitakazozungumziwa katika blog hii.
Maisha yetu ya kila siku yameambatana na mambo mengi ikiwemo furaha,huzuni,matatizo ya hapa na pale lakini hatuna budi kuvumilia na kutafuta njia zinazostahili ili kuhakikisha matatizo hayakai kwenye kiti bali tunayakabili vya kutosha .
Kila mmoja wetu katika nafasi aliyonayo anayo shauku kubwa ya kufanikiwa na kuwa na maisha bora kulingana na kazi yoyote anayoifanya.
Neno DARAJA linajulikana kabisa miongoni mwetu kwamba ni kivuko kutoka ng'ambo moja ya mto hadi nyingine. NENO MTO HAPA linamaanisha vile vikwazo mbali mbali kama vile kukata tamaa,umasikini,kutofikia malengo,woga na mengine kadha wa kadha. Mimi ni kiongozi wako nakuongoza wewe pia kukuelekeza namna ya kuvuka mto kupitia daraja lililopo na kuingia ng'ambo ya pili mahali penye mafanikio ,ambapo panaitwa DARAJA LA MAFANIKIO .
HAKIKA KUFIKA PALE SIO VIGUMU WALA SIO RAHISI SANA PANAHITAJI UVUMILIVU MAANA UVUMILIA NI MTIHANI .
"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"
Kwa ushauri zaidi maarifarobert @gmail.com
Instagram @lackiusrobert.
KARIBU.
No comments:
Post a Comment