Monday, January 14, 2019

KWA NINI MIMI(WHY ME)

                                                          KWA NINI MIMI

Ushawahi kujiuliza kanini upo katika huu ulimwengu,Nini sababu ya uwepo wako

Karibu katika Blog hii ya DARAJA LA MAFANIKIO  nikushirikishe kidogo japo upate kuongezea uelewa kuhusu kusudio la uwepo wako .

Kila mmoja anayo kwanini yake,kutokana na fikra alizonazo pia na umri kwa mfano ukimuuliza mtoto mwenye miaka mitano kwanini upo hapa duniani atakwambia si nimezaliwa na mama  utatamani hata kucheka ila ndio ilivyo maana uelewa wake ndio huo.

Mungu analokusudi kubwa tambua uwepo wako ni msaada kwangu mimi maana nikipata tatizo wewe utanisaidia,vile vile katika utendaji kazi tunategemeana kwa kiasi kikubwa.

Kusudi ndio sababu inayofanya kitu kiwe kama kilivyo au kinavyoonekana.Mwandishi Joel Nanauka anasema mfano ukiangalia muundo wa kijiko  ulivyo unakuelekeza namna ya kukitumia na ukitaka kukitumia kama kisu hautafanikiwa.

Ukijaribu kuishi katika kusudi amabalo sio lako utatumia muda mwingi sana kufikia malengo.
Yapo baadhi ya mswali unaweza kujiuliza kwamba kwa nini mimi ,nimezaliwa kwa kusudi gani pia ntakuwa nani maisha yangu ya baadae?
unaamka asubuhi na kuelea katika miangaiko yako labda kazini ,kwenye biashara n.k lakini kila mmoja anajua anapoelekea na kwa kuwa tunaona maisha yanazidi kusogea tunaendelea hivo .Wengi wanakuja kushtuka baadae kwamba njia walizopitia sio sahihi. 

Kazi kwako kuifahamu kwanini yako je? umezaliwa ili uwe nani wengi tunajua kwamba mtu kuwa msanii ndicho kipaji chake hakika kila mmoja anao usanii wake tatizo lipo kwa kiasi gani usanii wako unauonesha kwa watu wanaokuzunguka.

Nakusihi usikose sehemu inayofata endelea kufatria BLOG HII ,KARIBU .
''Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa''
kwa maoni maarifarobert@gmail.com
instagram @lackiusrobert
KARIBU.

No comments:

Post a Comment