Ni matumaini yangu kwamba umzima na unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku, Ni jamabo la kumshukuru mungu kwa kuzidi kutupatia pumzi bila gharama yoyote.
Karibu katika mwendelezo unaohusu MIMI NI NANI ? sehemu iliyopita tuliangalia kidogo kuhusu msemo huu ,najua walio wengi tunashindwa kuupambanua msemo huu katika maisha yetu ya kila siku.
Na hali hii inapelekea waliowengi kuendelea kutafuta kitu gani tufanye pia na sababu ya uwepo wetu katika ulimwengu huu.
Naomba nikushirikishe kwamba kila mmoja anacho kitu cha upekee katika maisha yaani kitu ambacho ni unic,na kitu hicho hakuna mwingine anaweza kukifanya.
Mungu ametujalia vipawa mbalimbali kama vile uchaezaji wa mpira,uimbaji,uhandishi na vipaji vingine mbalimbali na kila mmoja anachokipaji chake.MIMI NA WEWE tunacho kipaji fulani ambavyo tukivitumia vinaweza kutusaidia kuyafikia mafanikio.
Kwa mfano mamba maisha yake makubwa ni kukaa majini na chakula chake kkubwa ni nyama ,ina maana ukimchukua mamba ukamuweka nchi kavu kwa muda fulani maisha yake yanakuwa hatarini.Akijaribu kuwinda nje ya maji hutumia nguvu na muda mrefu kulinanisha na anapokuwa majini maana ndio maisha yake na nguvu zilipo.
Kila mmoja akifanya kazi kwa uaminifu na kujituma katika ile kazi hata kama ni ndogo inaweza kusaidia katika kuvuka DARAJA LA UMASKINI NA KUYAFIKIA MAFANIKIO.
Kumbuka mwaka 2019 ni mwaka wa mafanikio katika maisha na mipango yako . Ndugu msomaji maisha ni haya haya na mafaikio yapo mikononi mwako.
Karibu uendelee kufuatria Blog hii hakika hili ni daraja la mafanikio.
''Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa''
kwa maoni na ushauri maarifarobert@gmail.com
Instagram @lackiusrobert
KARIBU.
Nice one keep it up
ReplyDelete