Friday, April 03, 2020

UCHAMBUZI WA KITABU CHA RICH DAD POOR DAD

Karibu katika mwendelezo wa uchambuzi wa kitabu cha Rich dad Poor dad chake Robert Kiyosaki.


3. SOMO LA PILI: KWANINI TUNAFUNDISHA ELIMU YA FEDHA?
Katika sura hii Robert Kiyosaki anaelezea zaidi kwamba rafiki yake Mike alichukua mali za baba yake na akazitunza vizuri mpaka kuwa na mafanikio.Robert na mke wake Kim walistaafu mwaka 1996 akiwa na umri wa miaka 47 na mke wake 37 .Kustaafu kwao hakukumanisha kuwa waliacha kufanya kazi .Ila kipindi hicho walikuwa wanafanya kazi zao  zingine na pesa ilikuwa inaingia na yeye aliona hali hiyo kama uhuru wa kifedha.Hivyo mike alichagua kutumia ufalme wa baba yake na Robert alichagua kustaafu.
Watu wengi wanakuwa wakiniuliza kuwa ninapataje pesa ?  Na wao wanaweza wakaanzia wapi ? na nini siri ya mafanikio nimekuwa nikiwajibu hivi:
Kama wako tayali kuendana na mabadiliko na kufungua akili yao pamoja na kujifunza watakuwa matajiri na matajiri kwa sababu fedha bila kuwa na ufahamu wake itapotea bule.
Ili kuwa milionea haijalishi kiasi gani unapata bali kiasi gani umewekeza na kiasi gani unazalisha kwa sasa.Ukitaka kuwa tajiri unapaswa kuwa na elimu ya fedha( financial literacy).Ndio maana mimi na   Mike tunauwezo mzuri wa kuhifadhi pesa zetu ,tuna msingi mzuri wa fedha tuliofundishwa na Baba yetu tajiri.
Shule zetu hazituandalii msingi mzuri kuhusu fedha bali zinatuandalia ufaulu mzuri na kupata kazi yenye mshahara mzuri.Kama unataka kuwa tajiri lazima ujue kutofautisha faida (asset) na hasara ( liability).Asset ni kitu kinachoingiza fedha mfukoni lakini liability ni kitu kinachotoa fedha mfukoni.Matajiri wanahifadhi vitu vinavyowaletea faida lakini watu wa kipato cha kati wanamiliki vitu ambavyo haviwaingizii faida wanadhani ni faida kama mchoro unavyoonesha.

Ø  Mchanganuo wa mapato kwa mtu masikini                                      
 KAZI
MAPATO
MSHAHARA
MATUMIZI
Kama vile
Kodi ya serikali
Chakula mavazi ,kodi ya nyumba n.k

Faida na hasara kwa mtu maskini hapo ni kwamba fedha inaimgia na kutoka hakuna unachobakiza.
Ø  Mchanganuo wa mtu wa kipato cha kati
KAZI
MAPATO
MSHAHARA
MATUMIZI KAMA :
Kodi ya nyumba
,shule,malipo ya rehani.

    MADENI kama; Mkopo wa nyumba,shule na kadi za benki.




Ø  Mchanaganuo wa kipato cha tajiri

MAPATO(income) KAMA:
Kodi za nyumba,uaminifu,
Mgawanyo wa riba.

MATUMIZI(expances)
Kodi na malipo rehani.
Assert(faida)                            Liability (hasara)
Hisa ,Nyumba.                        
                                    Malipo ya kodi             rehani,Kadi za Benki.

Kwa ufupi  ili kuwa tajiri au kupata uhuru wa kifedha inabidi mapato yako yawe chini ya matumizi  yako.Ukiangalia michanganuo   mitatu hapo juu  utakuja kugundua kwamba maskini pamoja na mtu wa kipato cha kati bado wako kwenye madeni kipato chao havilingani na matumizi yao .Lakini tajiri kipato chake na matumizi yake havijapishana  ndiyo maana matajiri wataendelea kuwa matajiri na maskini na watu wa kipato cha kati watazidi kuwa masikini.
4. SOMO LA TATU : FANYA SHUGHULI ZAKO MWENYEWE.
Unapokuwa unamfanyia kazi mtu mwisho wa siku hautatoka na chochote atabaki nacho yeye,kama unahitahi kuacha mapambano ya kifedha fanya kazi zako mwenyewe,mfano ukiangalia wafanya kazi benki,wanasayansi wahasibu wote hawa shule imewaandaa kufanya kazi nakupata kupata mshahara lakini baada ya kustaafu hawabaki na kitu chochote.
·         Utaalamu wako kipato chako
·         Mali zako kipato chako.
Kuna utofauti mkubwa kati ya utaalamu wako wa kazini na shughuli zako mwenyewe mfano Robert wakati anazungumza na  wafanayakazi wa benki aliwauliza hivi nyinyi  shughuli zenu ni zipi ?, wakasema za kibenki, mkimaliza inakuwaje wakasema  tunaziacha. Ukimlinganisha  mtu mwenye shughuli zake anaendelea kubaki nazo.Tatizo linaokumba wasomi wengi ni kwamba wanakuwa walichokisomea, kama umesomea uhasibu utafanya kazi benki,kama umesomea mpishi utakuwa mpishi kama umesomea sheria utakuwa jaji kama umesomea ualimu utakuwa mwalimu na wengine hawajiongezi katika kufanya shuli zao wenyewe wanaendelea kuwafanyia kazi na kuwatajirisha mabosi.
Ukitaka kuwa tajiri fanya uwekezaji ambao utakuondoa kwenye madeni,vile vile watoto wetu tuwaandalie mazingira mazuri ya kuwafundisha elimu ya fedha na jinsi ya kufanya uwekezaji sahihi kama;
(i)  Mfumo mzuri wa biashara ambao hata kama haupo unajiendesha wenyewe (ii) Stock( hisa)
(iii) Bond( dhamana),(iv) Mutual fund (mfuko wa pamoja),(v) Motes( vidokezo),(vi) Royalities intellectual property such as music, scripts, patents,(vii) Real estate( Mali isiyohamisika)mfano nyumba.
Kama mtoto akifundishwa hivi pia na mzazi akazingatia vitu hivi kwa kufanya kazi zake mwenyewe tayali atakuwa na uwezo mkubwa wakupata uhuru wa kifedha.
5. SOMO LA NNE: HISTORIA YA KODI  NA NGUVU YA MASHIRIKA.

Mwandishi anazungumzia kuwa kodi siku zote inawanyonya wazalishaji mali na kuwafaidisha wasiokuwa wazalishaji mali ,Hii kwake anaona sio sawa matajiri siku zote hutafuta namna ya kukwepa kulipa kodi lakini maskini wanalipa kodi kubwa sana kuliko hata kipato chao.
Pia anasema masikini wanaendeshwa na mashirika wakati matajiri wanayaendesha mashirika na wanayatumia kupata pesa,Wanatumia mashirika haya kulinda kuboresha vitega uchumi vyao. Wanayatumia mashirika haya kukwepa kodi,Wanajua kuyadanganya mashirika na kupata pesa zaidi,Wanachukua pesa, wanalipa kodi, na kuishi kwa pesa zilizobaki.Masikini wananyonywa na mashirika haya lakini hawajui kama wananyonywa. Ili kuwa tajiri ni mhimu kila mtu akaanzisha biashara ya kwake. lazima kila mtu ainue IQ yake ya uchumi, ujuzi wa soko, utunzanji wa fedha na uwekezaji.Pia anasema
Ninaposema shirika ni idara maalumu mfano kampuni inayoundwa ili kushughulikia usimamizi na utekelezajiwa shughuli maalumu kama vile za kibiashara,Mfano hapa Tanzania kuna Shirika la Reli ,Shirika la habari n.k.
Mwandishi anajaribu kelezea kidogo kuhusu kuanziswa kwa kodi nchini marekani na uingereza anasema kodi hizo zilianzishwa kwa lengo kubwa la kupambana na hasara iliyojitokeza kutokna na uwepo wa vita.Katika swala la kodi kuna watu wanajiuliza mbona maskini na tajiri wanalipa kodi sawa kwanini matajiri wasilipe kodi tofauti na maskini?.Anasema matajiri wanajua vizuri nguvu ya ushirika na wanawekeza huko kuliko watu wa kipato cha kati na maskini.
Nikikumbuka katika somo la kwanza kuhusu nguvu, unapofanya kazi kupata pesa unakuwa huna nguvu ya kujiongoza mwenyewe bali unampa nguvu mwajiri wako , lakini pesa inapokufanyia kazi unakuwa na uwezo wa kuithibiti ipasavyo.Baba msomi alinambia niende nikafanye kazi kwenye shirika kubwa nipate pesa zaidi lakini baba Tajiri anasema kwanini nisiwe nasimamia mshirika yangu? ,Nilipokuwa mdogo sikuwahi kumuelewa, nilianza kumuelewa nilipofikisha miaka 20 ,na ilipofika mwaka 1974 wakati bado ni mwajiriwa nilifungua kampuni yangu na nilikuwa nawafariji wafanyakazi wangu.
Ninawakumbusha watu kuwa elimu ya msingi wa fedha  imeundwa na maarifa kutoka makundi  manne ambayo ni;
 (i) Uhasibu, Ambayo ninaiita ujuzi wa kifedha ,Ujuzi muhimu ukiwa unataka kujenga msingi mzuri wa pesa zaidi unayoitaka. Huu ndio upande wa kushoto wa ubongo. Ujuzi wa kifedha ni uwezo wa kusoma na kuelewa taarifa za kifedha , uwezo huu hukuruhusu kutambua nguvu na udhaifu wa biashara yoyote.
 (ii) Uwekezaji, Ambayo ninaiita sayansi ya utengenezaji  pesa, hii inajumuisha mikakati na kanuni za upataji pesa. Huu ndio upande wa kulia wa ubongo, au upande wa ubunifu.
(iii) Kulielewa soko, Sayansi ya usambazaji na uhitaji. Kuna haja ya kujua mambo haya kiufundi  kuhusu kulifahamu  soko, ambayo huchochewa na hisia, Sababu nyingine ya soko huu ni msingi au hali ya kiuchumi ya uwekezaji. Watu wengi wanafikiria dhana za kuwekeza na kuelewa soko ni ngumu sana kwa watoto. Wanashindwa kuona kwamba watoto  ni vema wakawa wanajua masomo hayo kiundani wakiwa bado watoto.
 (iv) Sheria, Kwa mfano, kutumia shirika lililofunikwa kwa ustadi wa kiufundi wa uhasibu, uwekezaji na uelewa wa masoko yanaweza kusaidia ukuaji wa kifedha. Mtu aliye na maarifa ya faida ya ushuru na ulinzi inayotolewa na shirika anaweza kupata utajiri haraka sana kuliko mtu ambaye ni mfanyakazi au mmiliki wa biashara ndogo ndogo. Ni kama tofauti kati ya mtu anayetembea na mtu anayeruka.
6. SOMO LA TANO: MATAJIRI WANAWEKEZA KWENYE FEDHA.
Nimekuwa nikifundisha tangu 1984 nimekuwa uzoefu mzuri na pia na  kutoa taaluma niliyonayo.
Nilifundisha maelfu ya watu binafsi na ninaona jambo moja katika sisi sote kuwa tuna uwezo mkubwa, na sote tumebarikiwa na zawadi. Bado, jambo moja ambalo linashikilia yote kwetu nyuma ni kiwango cha kujiona tunajua. Sio ukosefu mkubwa wa habari za kiufundi ambayo zinatuzuia, lakini zaidi ukosefu wa kujiamini. Baadhi huathiriwa zaidi kuliko wengine mara tu tukiacha shule, wengi wetu tunajua kuwa swala la digrii za chuo kikuu au darasa zuri ndio zinahesabu mafanikio,kumbe unaweza pata mafanikio makubwa kupitia elimu ambayo haukufundishwa shuleni.
Katika uzoefu wangu wa kibinafsi, fikra zako za kifedha zinahitaji maarifa ya kiufundi pia ujasiri. Ikiwa hofu ni kubwa sana, akili hukandamizwa. Katika madarasa yangu nawasihi sana wanafunzi,jifunze kuchukua hatari, kuwa na ujasiri, kuiruhusu akili zao zibadilishe woga huo kuwa nguvu na uzuri. Nilinafanya kazi kwa wengine na nimegundua kwamba kwa watu wengi, wakati inakuja mada ya pesa, wangeamua kucheza salama. Nimelazimika kuhoji maswali kama haya kama, Kwa nini uchukue hatari? Kwa nini nijisumbue kukuza IQ yangu ya kifedha? Kwa nini niweke fedha kusoma na kuandika?.
Kuna mtu kama Bill Gates na kampuni zake  Microsoft zinazoundwa kila mwaka kote ulimwenguni na kote zinafanya kazi vizuri  ,sio kwamba yeye hana woga bali anathubutu na kuwekeza kwenye pesa ili imsaidie baadae hivyo ni vema  kufurahisha zaidi kuwa hai. Ningependa kufurahi juu ya kutengeneza mamilioni kuliko kuwa na wasiwasi juu sio kupata kipato. Kipindi hiki tulicho sasa ni kipindi cha kufurahisha zaidi mambo ambayo hayajawahi kufanywa ndani ya historia ya ulimwengu, na tutafurahia zaidi endapo tukiwekeza kwenye pesa.
Tutaendelea na sehemu sa Saba wakati mwingine.

karibu upate uchambuzi wa vitabu vingine ,nitumie ujumbe kupitia namba 0767702659 au email
maarifarobert@gmail.com.
Karibu tujifunze zaidi.

No comments:

Post a Comment