UCHAMBUZI WA KUHUSU
MAISHA NA MAFANIKIO NA LACKIUS ROBERT
Zingatia haya machache yafuatayo
TABIA YA
KUBAGUA KAZI;
Hakuna binadamu aliyeumbwa kufanya kazi fulani na mwingine
afanye kazi ile sote tunafanya kazi kuendana na maisha yetu yalivo.utfiti
unaonesha kuwa asilimia 80% ya kushindwa kufikika kwa malengo kunachangiwa na
sisi mwenyewe katika fikra zetu yaani
inner feeling halafu asilimia 20% ni Sababu za nje,matumaini yangu makubwa
kwamba wengi wetu tunazitambua changamoto zinazotukabili kwa ambao tupo kwenye
masomo tunatambua kwamba changamoto kama vile
ajira ipo tumeisikia hata wengi wetu
bado hatujaingia kwenye elimu ya juu na cha kushangaza ni kwamba baadhi
yetu pesa tunazopewa na wazazi wengine
wnapewa na bodi lakini tunazitumia katika matumizi ambayo wakati mwingine
yasiyo sahihi simanishi kwa wote ila kama unazitumia katika matumizi ambayo sio
sahihi inakuhusu na tutambaua mlima ulio mbele yetu kwenda nyumabani kulima
hautaki wakati pesa unazipata umazitumia vibaya je nani wa kulamiwa mzazi wako
serekali au nafisi yako.nayaongea hayo maana nimewatazama vijana wengi
wakiangaika baada ya kuhitimu masomo yao,huku wakilaumu sana.
Pia vijana
wenzangu baada ya kuhitimu masomo kubagua kazi kunakuwepo wapo wengine wanaona
kazi kama vile kuuza maji ,kupakia mizigo ni kazi ambazo anaona hazimfai kabisa
tunashindwa kutambua kwamba hio pesa yenyewe tunayoitafuta haijawahi kumbagua
mtu yeyote ndio maana utajiri auna ubaguzi utakuta vijana wengine miaka
ishirini ana pesa za kutosha mzee mwenye miaka sitini au hamsini ana pesa za
kubabaisha ,wzazee wengine wanapesa za kuosha wengine wamesoma wengine hata
chekechekea hawajaenda lakini pesa anazo kwa hio vijana wenzangu swala la
kubagua linatufanya tunabaki kuhangaika tu mijini na vijijini.Kinachoshangaza
ni kwamba unamkuta kijana mwenzangu hana hata mia lakini ukimwambia njoo basi
tukapige kibarua hata kusomba tofali kwa siku elfu saba au elfu kumi anakwambia
hizo kazi sio za kwetu wapo wenye uwezo kwa kuzifanya ,na je! pesa na yenyewe
ingesema mi nataka nishikwe na huyu Yule hafai ingekuwaje au kama ingewachagua
wasomi tu,au ambao hawajasoma duniani tungeishi je?.
Vijana wenzangu ambao hatupo kwenye masomo ni mengi sana
tunayaona pamoja na kuyasikia redio mbali mbali zinatangaza viongozi mbali
mbali wanasema kuhusu namna gani vijana tuwe na maisha mazuri.Mimi nafurahi
sana ninapowakuta vijana wanajishughulisha na shughuli kama vile biashara ndogo
ndogo siku moja nilikuwa Ubungo nikakutana na kijana mmoja anabeba mizigo kwenye
mkokoteni na kuzipereka sehemu tofauti kutegemea na wasafiri wanapoelekea
nikabaatika kuzungumza nae kwa kina akanieleza jingi gani anavyopenda kazi yake
licha ya kwamba pesa anayopata sio nyingi lakini mahitaji ya familia anayapata
pia na kulipa kodi ya nyumba..
Changamoto yetu vijana wengi tunadharau kazi hasa
hasa zile za kutumia nguvu nyingi lakini tukumbuke imeandikwa kila mtu atakula
kwa jasho lake ,mbuzi anakula kulingana na urefu wa kamba yake ila tunashindwa
kufanya mfano mdogo wa kuku,nafukili wengi tunamjua jinsi gani anavyotafuta
chakula chake kwa kuparua parua huku asipopata wadudu anageukia pale pale
upande wa pili na kupata wadudu na kuwala .Vijana tuchotaka kuona ni kupata
kazi nyepesi nyepesi kwa hali hio hatutafka mbali tuutume ujana wetu kufanya
kazi nzito juani wakati huo tukitegema
kuvuna mazao tukiwa kivulini Walen Buffet anasema’ kivuli cha mti uliokalia leo
kuna mtu aliupanda’kwa hio tupande mbegu bora kwa ustawi wa maisha yetu. Kila
mtu anaouwezo mkubwa wa kufanya kazi yoyote endapo akilegeza mwili na kururusu
moyo kuwa na amani kwa kila kazi iliyoko
mbele yetu. .
ILE HARI YA TAMAA;
Hali ya kutamani kitu fualani haiepukiki kwa maisha ya mwanadamu
yeyote maana kutoka na kutamani ndiko tuapata ushindani pengine mafaikio pia
wapo wanaotamani wazaliwe kama wachezaji wakubwa kama hapa Tanzania Mbwana
Samatta kina Msuva na wengineo,wasanii wakubwa kama Diamond ,Lady Jay Dee
,waamashishaji maarufu kama Eric Shigongo,Nanauka Antony Luvanda na wengineo
wengi tamaa ya namna hio kama tukitamani na kuongeza juhudi inakuwa ni nzuri
.Kiuharisia kila mwanadamu anapaswa kutamani
tama mbele mauti nyuma maana kutokana na kutamani ndipo tunapata namna
ya kusogeza maisha yetu mbele tama ipo katika Nyanja tofauti maana kila mmoja
wetu ana namna anavyotamani.
Tamaa ya moyo, yaani tama hii Kwetu vijana imekuwa ni tamaa
ambayo wakati mwingine hutususumbua na kuharibu mipango yetu ya maisha 20%
katika wimbo wa’’ tama mbaya’’ anasema moyo sifa yake kutamani tama ya moyo
inaweza kukuweka matatani. Mara nyingi tumekuwa tunatamani mambo makubwa kuliko
uwezo wetu kama vile nyumba magari
nyingi wakati hatujaweka njia za kupata vitu hivyo na tamaa hiyo mara
nyingi inapelekea kuhahirisha baadhi ya vitu tunavyokuwa tumeweka tumeona
vijana wawili waliokuwa na mpango wa kujenga nyumba na mmoja wao akatamani
ashobokewe na mabinti hadi akaamua kununua pikipiki ambayo hakudumu nayo muda
mrefu na tama yake ilimponza.
Pia kuona kitu chochote kizuri moyo unakitamani
kwetu vijana unamwona binti au mvulana mzuri moyo unamtani hadi akili nzima
kichwani ivnavurugika unatamani kupata japo hata dakika kadhaa za kuzungumza
nae ,uwepo pia wa mitandao ya kijamii umechangia sana vijana wengi kutamani
sana maana kuna wengine wanapost picha zinazoonesha nguo za ndani ,aina
mbalimbali za mitindo mara nywele,nguo n.k na sisi vijana tukiona wanapata
comments na likes nyingi tunapata shauku ata kubadilisha miili yet undo wengine
tunaona wanajichubua wananyoa mitindo tofati ya nywele na vijana wa kuime
kutoboa masikio lengo ni kutaamani kuwa kama wale anaowaona lakini tutambue
vijana kusimama imara na kutunza miili
yetu ni jambo ambalo linaleta heshima hata kwa jamii inayotuzunguka.
Tamaa ya pesa,jambo lisilo napingamizi kwamba kila mmoja wetu
anataka awe na pesa za kutosha ili kujikimu kimaisha tama ya pesa hauwezi
kuikwepa hata siku moja wengi tunaishia tu kutamani lakini hatuweki mipango
madhubuti ya kupata pesa hizo inafika hatua wengi wetu wanaingia kwenye
wizi,unyanganyi kwa watu wanoonekana wanapesa ,mali lengo ni kutaka kuwafanya
hao vijana waingie katika ulimwengu wa matajiri.
Kuwa UNSTOPPABLE maana yake
usitishiwe au kuyumbishwa na vitu vinavyoonekana havina tija kwa maisha yako ya
kila siku,vijana tunyanyuke na kufanya kazi kwa bidii pes ipo ukiitafuta
utaipata lakini kuendelea kulalamika pesa hakuna vyuma vimekaza hakutatusaidia
kumbuka wanasema hata safari ya maili elfu moja huanza na hatua moja Yule
tajiri tunayemuona anapesa za kutosha naye alianza na shilingi 100 na kuendelea
je mimi na wewe tunataka tuanzie shilingi ngapi ?.
Jambo la muhimu kuzuia tama
ya pesa kutusumbua tuweke ratiba maalumu ya kuwa tunatunza akiba kila baada ya
kupata kiasi fuani cha pesa haijarishi tumetunza kiasi gani baada ya muda
alienza na mia moja tutakuwa katika harakati za kumfikia .Natambua changamoto
zipo kila siku na hazitaisha lakini najiuliza kama baadhi ya vijana wenzetu
wamefaulu kuzishinda changamoto hizo wakawa unstoppable kwa nini mimi na wewe?
Je! Wao wana miguu,macho na mikono zaidi
ya mbili? .
Tufanye maamuzi sasa wakati ndio huu, katika kutamani kupata pesa
Elieshi Lema katika kitabu cha ‘’In the Belly of Dar es salaam ‘’ amejaribu
kuonesha baadhi ya vijana wanaotamani kuja mjini wakifikilia kuna maisha mepesi
na kukimbia maisha yao ya kijiji baada ya kufika mjini wanakuta ni tofauti
kabisa na matarajio waloyawaza pindi wapo nyumbani baada ya kuona maisha
yamekuwa magumu huanza kujiingiza katika matendo mabaya ikiweo kufanya ukahaba
wizi n.k.
Tamaa hii mara nyingi inachochewa sana na makundi ya marafiki
tunaokuwa nao nimesoma stori kadhaa za madada wenye kutamamani pesa za haraka
mpaka wakajiingiza kwenye biashara ya kuuza mwili,vijana wengi wa kiume kuishia
kucheza kamali lengo ni kutaka kuwa na pesa alizonzo Fulani katika kundi lao na
hali hii ya tamaa humfanya mambo yasiyo na tija kubwa kwa maisha ya badae mfano
madwa ya kulevya, mtu anakosa amani anafanya kazi kufa na kupona mpaka apate
kama cha mwenzake badala ya hizo nguvu kuziweka katika maendeleo ambayo
yatanufaisha familia yake na taifa kwa ujumla.
Mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu sana. Ili kuendelea kupata chambuzi mbali za vitabu bonyeza link hii ili uendelee kupata ucambuzi wa vitabu kwa lugha ya kiswahili.
htthttps://t.me/SOMAONLINETELEGRAM