Friday, March 22, 2019

MAISHA NA MAFANIKIO

Kuna wakati maisha yetu kwa mambo tunayopitia tuyafananishe na maisha ya mtoto mdogo.

Mtoto anapofikia muda fulani uwa anajaribu kusimama lakini anashindwa na kuanguka chini.Lakini hawezi kumlaumu,kusikitika au kununa kisa mama yake kamuacha kaanguka.Baada ya muda kidogo hujaribu tena na tena ,kadri siku zinavyozidi kusogea anazidi kujaribu na kupata uzoefu.

Baada ya muda anajikuta anasimama vizuri na kutembea pia.Yote anayoyapitia waga hakumbuki wala kujutia.

Mara ngapi tumekutana na heka heka katika maisha yetu? Na tumejuta na kutoa lawama Mara ngapi? .Tukisema kwanini Mimi tu.Lakini tukumbuke   hakuna  kilichoanza bila msingi,heka heka zinakujengea msingi Fulani katika maisha,na wakati mwingine tujifanye kama mtoto mdogo tukianguka tunasimama tena na ikiwezekana kutembea.

" Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Karibu katika blogu hii ya Daraja LA mafanikio uzidi kupata vitu moto moto.
Nitumie ujumbe au maoni kupitia
 maarifarobert @gmail.com
Instagram @lackiusrobert

KARIBUNI.

No comments:

Post a Comment