Thursday, January 17, 2019
KWANINI MIMI (WHY ME) PART 2
Ni matumaini yangu kwamba uhu mzima wa afya na unaendelea vizuri na kazi za ujenzi wa taifa,nakuomba usisahau kumshukuru mwenyezi mungu kwa zawadi ya uhai anayozidi kutupatia
Karibu katika blog hii ya Daraja la mfanikio uzidi kupata maarifa fulani fulani pengine ushawahi kusikia au ndo mara ya kwanza.
Karibu katika sehemu ya pili KWANINI MIMI (why me) kumbuka aliye na kwanini anaweza kuyafikia mafanikio kwa kuyakamilisha malengo yake.
Kwa sababu kila kitu anachofanya anajiuliza kwanini nafanya hivi? na nikifanya hivi majibu yake yatakuwa yapi au nini kitatokea endapo nikifanya hivi.
Naomba ujaribu kufanya majaribio kidogo kwa kujiuliza kwanini mimi,sio muda wa kuanza kulalamika kwamba haujafanikiwa bado muda unao maana naamini kama nguvu ,akili na uwezo unavyo yote yanawezekana.Katika sehemu ya kwanza nilisema Mungu anayo makusudi makubwa sana nawewe na kamwe hawezi kukutupa.
Chagua eneo sahihi kufanya na ufanye kwa bidii utaiona maana ya kwa nini yako pia sababu ya uwepo wako hapa ulimwenguni utaikamilisha .Ebu jiulize mpaka sasa hivi kitu gani ambacho utakumbukwa kuwa ulikifanya hapa ulimwenguni kama bado zungumza na moyo wako.
Nakusihi uendelee kuifatria Blog hii kazaaa!!!
''Compete and learn''
Monday, January 14, 2019
KWA NINI MIMI(WHY ME)
KWA NINI MIMI
Ushawahi kujiuliza kanini upo katika huu ulimwengu,Nini sababu ya uwepo wako
Karibu katika Blog hii ya DARAJA LA MAFANIKIO nikushirikishe kidogo japo upate kuongezea uelewa kuhusu kusudio la uwepo wako .
Kila mmoja anayo kwanini yake,kutokana na fikra alizonazo pia na umri kwa mfano ukimuuliza mtoto mwenye miaka mitano kwanini upo hapa duniani atakwambia si nimezaliwa na mama utatamani hata kucheka ila ndio ilivyo maana uelewa wake ndio huo.
Mungu analokusudi kubwa tambua uwepo wako ni msaada kwangu mimi maana nikipata tatizo wewe utanisaidia,vile vile katika utendaji kazi tunategemeana kwa kiasi kikubwa.
Kusudi ndio sababu inayofanya kitu kiwe kama kilivyo au kinavyoonekana.Mwandishi Joel Nanauka anasema mfano ukiangalia muundo wa kijiko ulivyo unakuelekeza namna ya kukitumia na ukitaka kukitumia kama kisu hautafanikiwa.
Ukijaribu kuishi katika kusudi amabalo sio lako utatumia muda mwingi sana kufikia malengo.
Yapo baadhi ya mswali unaweza kujiuliza kwamba kwa nini mimi ,nimezaliwa kwa kusudi gani pia ntakuwa nani maisha yangu ya baadae?
unaamka asubuhi na kuelea katika miangaiko yako labda kazini ,kwenye biashara n.k lakini kila mmoja anajua anapoelekea na kwa kuwa tunaona maisha yanazidi kusogea tunaendelea hivo .Wengi wanakuja kushtuka baadae kwamba njia walizopitia sio sahihi.
Kazi kwako kuifahamu kwanini yako je? umezaliwa ili uwe nani wengi tunajua kwamba mtu kuwa msanii ndicho kipaji chake hakika kila mmoja anao usanii wake tatizo lipo kwa kiasi gani usanii wako unauonesha kwa watu wanaokuzunguka.
Nakusihi usikose sehemu inayofata endelea kufatria BLOG HII ,KARIBU .
''Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa''
kwa maoni maarifarobert@gmail.com
instagram @lackiusrobert
KARIBU.
Tuesday, January 08, 2019
MIMI NI NANI? part 2
Ni matumaini yangu kwamba umzima na unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku, Ni jamabo la kumshukuru mungu kwa kuzidi kutupatia pumzi bila gharama yoyote.
Karibu katika mwendelezo unaohusu MIMI NI NANI ? sehemu iliyopita tuliangalia kidogo kuhusu msemo huu ,najua walio wengi tunashindwa kuupambanua msemo huu katika maisha yetu ya kila siku.
Na hali hii inapelekea waliowengi kuendelea kutafuta kitu gani tufanye pia na sababu ya uwepo wetu katika ulimwengu huu.
Naomba nikushirikishe kwamba kila mmoja anacho kitu cha upekee katika maisha yaani kitu ambacho ni unic,na kitu hicho hakuna mwingine anaweza kukifanya.
Mungu ametujalia vipawa mbalimbali kama vile uchaezaji wa mpira,uimbaji,uhandishi na vipaji vingine mbalimbali na kila mmoja anachokipaji chake.MIMI NA WEWE tunacho kipaji fulani ambavyo tukivitumia vinaweza kutusaidia kuyafikia mafanikio.
Kwa mfano mamba maisha yake makubwa ni kukaa majini na chakula chake kkubwa ni nyama ,ina maana ukimchukua mamba ukamuweka nchi kavu kwa muda fulani maisha yake yanakuwa hatarini.Akijaribu kuwinda nje ya maji hutumia nguvu na muda mrefu kulinanisha na anapokuwa majini maana ndio maisha yake na nguvu zilipo.
Kila mmoja akifanya kazi kwa uaminifu na kujituma katika ile kazi hata kama ni ndogo inaweza kusaidia katika kuvuka DARAJA LA UMASKINI NA KUYAFIKIA MAFANIKIO.
Kumbuka mwaka 2019 ni mwaka wa mafanikio katika maisha na mipango yako . Ndugu msomaji maisha ni haya haya na mafaikio yapo mikononi mwako.
Karibu uendelee kufuatria Blog hii hakika hili ni daraja la mafanikio.
''Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa''
kwa maoni na ushauri maarifarobert@gmail.com
Instagram @lackiusrobert
KARIBU.
Sunday, January 06, 2019
MIMI NI NANI
MIMI NI NANI
Karibu kabisa katika Juma la kwanza la mwaka 2019,Natumaini umzima unaendelea vizuri na majukumu yako.
Jambo la kwanza naomba tumshukuru Mungu kwa kutufanya kuuona mwaka 2019 ,wapo wengi walitamani sana kuuona lakini hawakuweza kuuona,wewe na mimi tunayo thamani kubwa mbele ya mwenyezi mungu ndio maana anazidi kutupatia uhai.
Katika ukurasa wako mpya wa kuhakikisha unafanikiwa, hakika huu ni mwaka wa mafanikio kwako nakukaribisha katika Blog hii ya DARAJA LA MAFANIKIO ili uweze kuyafahamu mambo mbalimbali amabyo unayajua au pengine ni mara yako ya kwanza kuyasikia.
Watu walio wengi wamekuwa wakijiuliza katika nafsi ya kwanza wao ni kina nani yaani .Mfano mimi nasema hivi MIMI NI NANI?.
Namimi pia nimejiuliza mara nyingi swali hili lakini nikajaribu kupitia pitia kurasa za maandishi mbali mbali ya watu tofauti tofauti nikaja kugundua kwamba mimi ni wa thamani kubwa sana maana akuna mtu ata mmoja katika ulimwengu huu mwenye upekee kama nilivyo mimi,Kuna kitu ninacho ambacho mungu amenipatia na hakuna yeyote wa kukiondoa isipokuwa yeye mwenyewe muumba.
Wengi tumekuwa tukitamani sana kuwa kama kina fulani mfano mchezaji furani wa mpira ,msanii fulani na hatimaye tumeanza kuyaiga wanayoyafanya.
Msomaji wa BLOG hii naomba nikuabarishe kwamba wewe ni wa pekee sana unao uwezo mkubwa tu wa kuyafanya makubwa katika ulimwengu huu,usiendelee kufikilia kwamba labda wakati wako bado ila unaweza kuwa sahihi lakini sio sana kama bado hujaanza kufanya bado haujachelewa .
Najua changamoto kubwa inayotukabili ni kwamba BADO TUNASHINDWA KUJUA ENEO NA WAKATI SAHIHI WA KUYAFANYIA MAMBO HAYO.Huu ni mwaka wa mafaikio fanya kazi kwa bidii katika sehemu uliopo kwa moyo wako wote utafanikiwa kuyaona mafanikio japo yanaanza kidogo lakini shukuru.
Nakusuhi uambatane na mimi wakati mwingine katika kuielezea mada hii.
karibu mimi ni Kiongozi lengo ni kukuvusha salama katika daraja na kuyafikia mafanikio.
''Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa''
Kwa maoni maarifarobert@gmail.com
Instagram @lackiusrobert.
KARIBU.
Subscribe to:
Posts (Atom)