Monday, January 30, 2023

HAKUNA WA KUNYWA DAWA ILI UPONE

"Hakuna wa kunywa dawa ili mgonjwa apone tofauti na mgonjwa mwenyewe" Kila nikisoma kitabu Cha Kusudi Lako Hatma Yako na kukuuona msemo huu. Huwa Kuna vitu vingi naviwaza. Na maswali mengi kujiuliza. Hivi ingetokea, ni kwa mfano lakini sawa! Kukawa na uwezekano wa mtu mwingine kunywa dawa Kwa niaba ya mgonjwa. Hii ingekuwaje? Unafikiri ni upande upi ungepata shida zaidi? Watu wa aina ipi wangeonewa katika hili? Na je, hospital zingeweza kulaza wagonjwa? Ni swali lenye utata mkubwa. Huenda Mungu aliona Dunia isingekuwa fair. Kundi Fulani la watu wangewaonea kundi lingine. Yaani wao wakiumwa Ili lingine linaangaika kupewa dawa na sindano. Parefu hapo.... Ila hayo yote hayakuwezekana na inapofika ugongwa hakuna Cha wewe ni bosi katika kampuni Fulani, kiongozi katika Jimbo Fulani. Bali mwili kukosa nguvu ni kule kule, maumivu ni yale yale sawa na watu wengine wa kawaida. Ugonjwa wako ni biashara Yako, ndoa Yako au kazi Yako.Huenda unapata changamoto kila siku. Lakini tambua ni wewe tu unayejua Maumivu unayopata. Hakuna mtu wa kutimiza wajibu au majukumu kwa ajili Yako. Wewe ndiye kiongozi mkuu katika Kila jambo unalohitaji kufanikiwa. Dozi Yako ni namna unavyotumia vema muda wako, nidhamu, kujifunza na kujituma. Kadiri unavyoiongoza vema ndivyo inavyozidi kuwa imara. Ukiachia dawa katikati kisa ni chungu na hapo ndipo mambo uharibika. Jitahidi umalizie dozi Yako. Ili upone vema na kurejea kwenye Hali Yako ya kawaida kiutendaji. Ambayo ndiyo matokeo unayotaka kuyapata. Karibu upate nakala Yako leo ya kitabu cha Kusudi Lako Hatma Yako. Lackius Robert 0767702659 #mwangaza2023

No comments:

Post a Comment