Saturday, April 25, 2020

UCHAMBUZI WA KITABU CHA KITABU CHA THINK ANDA GROW RICH NAPOLEON HILL

KARIBU KATIKA SEHEMU INAYOFUATA YA UCHAMBUZI WA KITABU CHA THINK AND GROW RICH  NAPOLEON HILL.


4.Kanuni ya nne kuelekea utajiri ni kupata MAARIFA MAALUMU
Kuna aina mbili za maarifa moja ni ujuzi wa jumla na mwingine ujuzi maalumu.Ujuzi wa jumla pasipo kujali ni mkubwa kiasi gani au ni mwingi kiasi gani una matumizi kidogo sana katika kujipatia pesa.Ujuzi aupati pesa kama haujapangiliwa  na kuongozwa kwa akili kupitia mipango inayotekeleka ya kivitendo kuelekea kwenye lengo lililokuwa dhahiri la kujipatia pesa unayoitaka.Hapa watu wengi waga  wanachanganya na kusemea ujuzi ni nguvu ya kufanya upate unachotaka ,hii haiwezi kutimizika endapo auna mipango mizuri inayotekelezeka.

Mfano ukiangali katika vitengo mbalimbali vyuoni vimejaa watu wenye elimu kubwa,wastarabu na wabobezi lakini linapokuja swala la ujuzi bado hawajabobea katika kuyapanga na kuyatumia maarifa zaidi na kuwafanya wawe matajiri.Ukija kuangalia mtu aliyeelimika siyo lazima awe ni Yule mwenye ujuzi mwingi wa jumla au maalumu.Bali ni wale walioelimika na wamejenga vitivo vya vya akili zao kusudi ziweze kupokea kitu chochote wanachotaka mfano Henry Ford hakuwa na elimu kubwa lakini alikuwa ana uwezo mkubwa wa kuthubutu kufanya jambo pasipo kurudi nyuma tofauti na wengine wanavyoishia njiani.Mtu yeyote aliyeelimika  ni Yule ambaye anaweza kupata maarifa anayoyahitaji,najinsi ya kuyapangilia hayo maarifa katika mipango dhahiri ya kivitendo kupitia sehemu mbali mbali inaweza kuwa kundi lake la kushauriana n.k. 
 
Kabla hujaweza kuwa na uhakika wa uwezo wako wa kubadilisha shauku kuwa katika kiwango chake cha fedha kinacholingana nayo,unahitaji ujuzi maalumu wa huduma,bidhaa au utaalamu unaokusudia kuutoakwa ajili ya kupata utajiri.Pengine unaweza kuhitaji ujuzi maalumu zaidi kuliko vile ulivyokuwa nauwezo au mwelekeo wa kuupata na kama hii itakuwa kweli,unaweza ukauziba udhaifu wako kupitia kundi lako la kushauriana.Mfano Endrew Carnegie hakuwa  anajua kitu kuhusu biashara ya chuma cha pua na hakujisumbua bali ujuzi aliouhitaji aliupata kutoka kwa mmoja kati ya kundi lake la kushauriana.Ukihitaji kuwa tajiri inabidi uongeze jitihada kupitia ujuzi maalumu uliopangiliwa vizuri sana.

Amua juu ya aina ya aina ya ujuzi unaohitaji kuwa nao lengo unalofanyia kazi ili kulifikia na hapa inabidi ujiulize kuhusu taarifa na vyanzo sahihi vya maarifa unayopata;
(i)Uzoefu na elimu ya mtu mwenyewe
(ii)Uzoefu na elimu vinavyopatikana kupitia ushirikiano na watu wengine
(iii)Makataba za umma au kupitia  vitabu na majarida mbalimbali
(iv) Kozi maalumu za mafunzo kama kupiti mafunzo ya madarasa ya jioni na zaidi mfumo wa njia za posta.Hivyo ujuzi maalumu,pamoja na ubunifu  ni viungo bora vya kukufanya wewe kufanikiwa katika kila kitu aunachokifanya.

5.Kanuni ya tano kuelekea utajiri ni kuwa na UBUNIFU
Ubunifu maana yake ni karama ambayo mipango yote inayopangwa na mtu hutengenezwa.Msukukumo shauku hupewa umbo au vitendo kupitia msada wa kitengo cha ubunifu wa akili.
Kuna msemo wa kuwa ,tunaweza kutengeneza  chochote kile ambacho tunakifikiria.Katika zama zote za ustarabu,hizi ndiyo zama zinazofaa zaidi kwa ajili ya ukuzaji na ubunifu kwa sababu ndiyo zama za mabadiliko ya haraka sana.Karibia kila mahali tunakutana na vichocheo vinavyotufanya tuweze kubuni vitu mbalimbali.

Kwa sasa wapo wabunifu mbalimbali mbao wamefanya mambo makubwa ya kuishangaza dunia pia na kuisaidia dunia,hsahasa katika kutatua baadhi ya matatizo mfano waliobuni ndege,meri ,Gaari,vifaa vya mawasiliano kama simu tarakirishi na vitu vnginevyo vingi.Ndugu yangu mpendwa unawezaa ukabuni kitu kwa sasa na kisakusaidia wewe lkutataua baadhi ya matatizo yanayoikumba jamii na kukusaidia wewe mwenyewe.

Mwandishi anaonesha aina mbili za ubunifu:
1.Ubunifu sanisi,Hapa mtu anaweza akapanga fikra za zamani,mawazo au mchanganyiko mpya.Kitivo hiki akiumbi kitu chochote, bali hufanya tu kazi na vitu kama uzoefu,elimu na ushuhuda ambavyo kinalishwa.Kinatumika sana an wagunduzi,ukiacha watu wenye akili nyingi sana ambao hutumia ubunifu wanaposhindwa kutatua tatizo kupitia ubunifu sanisi.

2.Ubunifu wa kujenga,Kupitia kitivo cha ubunifu wa kujenga,akili ya mwanadamu  inayo mawasilianao ya moja kwa moja na nguvu ya uumbaji,hiki ni kitivo ambacho hutumia hisia na ufunuo unaopokelewa yaani hapa mtu anaweza kuwasiliana na akili za watu wengine mfano( mzuri angalia mafundisho ya dini yalivyo unaweza kuelewe ufunuoni nini).Kitivo hiki huwa makini kwa sababau kinahusiana na uwezo wa kutuia hisi za wngine na mara nyingi hufanya kazi chenyewe lakini katika umakini mkubwa sana.

Hivyo kadili kitivo chako cha ubunifu kinavyotumika ndivyo kinavyozoidi kuwa bora na kisivyotumika ndivyo kinavyokuwa dhaifu.Kumbuka kuibadili shauku ya kuwa na pesa siyo jambo linalofanyika siku moja au kwa akauli moja inabidi lifanyike mara nyingi   ili akili na viungo vyako vya mwili vizoee.Viongozi wakubwa wa biashara makampuni,viwanda fedha wasanii waandishi wakubwa wameweza kufanikiwa kwa sababu walikuza vitivo vyao vya ubunifu.Shauku ni wazo tu ,msukumo ni kama nyota ya mbali sana au wingu la muda mfupi sana,nikitu kisichoshikika ni kitu kisocho na thamanimpaka kigeuzwe kuwa kitu kinachoshikika.Hapa ubunifu sanisi ndio unaotumika mara nyingi zaidi katika mchakato huu wa kubadilisha msukumo wa shauku kuwa pesa.Unapaswa kuelekeza umakini wako katika kubdili ubunifu wako sanisi kuwa unaoshikikia maana unahitaji pesa an pesa ni kitu kinachoshukika.Una mipango mbalimbali pesa inabidi itumike uwezi kumwambia mtu ninamipango mbalimbali lakini pesa sina kwa sasa ntakulipa nikiipata ,hapo mtu hawezi kukuelewa. Kila kitu uanweza ukakifanya kwa sababu kimeshawahi kufanyika kabla.

Jiulize ningefanya kitu gani kama ningepewa dola milioni moja
Penye nia pana njia’ Nilisimuliwa na yule mpendwa mwalimu na mchungaji, Frank W. Gunsaulus, ambaye alianza kazi yake ya kuhubiri katika eneo la Stockyards la Kusini mwa Chicago.Wakati Dr. Gunsaulus alipokuwa chuoni, aligundua mapungufu mengi katika mfumo wetu wa elimu, mapungufu ambayo aliamini angeliweza kuyarekebisha ikiwa kama angelikuwa Mkuu wa Chuo. Shauku yake kubwa kabisa ilikuwa ni kuwa kiongozi mkuu wa chuo cha elimu ambacho vijana wadogo wa kiume na wa kike wangeweza kufundishwa “kujifunza kwa vitendo”.

Alifanya uamuzi wa kuanzisha chuo kipya ambacho angeweza kutekeleza wazo lake jipya pasipo kulemazwa na njia za jadi za utoaji elimu. Alihitaji Dolla Milioni moja ili kutekeleza mradi ! Ni wapi angelaza mikono yake kwa kiasi kikubwa hivyo cha pesa? Hilo lilikuwa ni swali lililotawala sehemu kubwa ya mawazo ya mhubiri huyu kijana aliyekuwa na malengo makubwa.
Lakini hakuweza kuonekana kupiga hatua yeyote.

Kila siku aliingia kitandani na lile wazo. Aliamka nalo asubuhi alitembea nalo kila mahali alipokwenda. Aliligeuza tena na tena katika akili yake mpaka likageuka kuwa shauku isiyotulizika. Dolla Millioni moja ni fedha nyingi. Alitambua ukweli huo lakini pia aligundua ukweli kwamba kikwazo pekee ni kile ambacho mtu hujiwekea katika akili yake mwenyewe
Alikuwa mwanafilosofia na pia mhubiri, Dr.Gunsaulus alitambua, kama wafanyavyo wale  wote wanaofanikiwa maishani kuwa, udhahiri wa lengo ndiyo kituo ambapo mtu ni lazima aanzie. Alitambua pia kwamba udhahiri wa lengo huchukua umbo, uhai na nguvu unaposaidiwa na Shauku kubwa kulibadilisha lengo hilo kuwa katika kitu kinacholingana nalo.Alifahamu ukweli wote huu mkubwa, lakini bado hakujua ni wapi au ni jinsi gani angeweza kuweka mikono yake kwenye dola milioni moja. Utaratibu wa asili ingeliweza kuwa ni kukata tamaa na kuacha, akisema , ‘Ah sawa, wazo langu ni zuri lakini siwezi kufanya nalo chochote kwa sababu kamwe siwezi kupata dolla millioni moja zinazohitajika’. Hivyo ndivyo hasa ambavyo watu wengi wangeliweza kusema, lakini sivyo Dr. Gunsaulus alivyosema.Alichosema yeye, na alichokifanya, ni muhimu kiasi kwamba sasa namtambulisha na kumuacha azungumze, mwenyewe.

Siku moja Jumamosi mchana nilikuwa chumbani kwangu nikifikiria njia na namna ya kupata fedha ili kutekeleza mipango yangu. Kwa karibu miaka niwili nilikuwa nikifikiria, lakini sikuwa nimefanya chochote zaidi ya kufikiria.
Muda ulikuwa umewadia wa kuchukua hatua !
Niliamua mara moja kwamba ningeweza kupata dolla milioni moja zilizohitajika, ndani ya wiki moja. Ki vipi? Sikujali kuhusiana na hilo. Jambo kubwa na la muhimu lilikuwa ni uamuzi wa kuzipata fedha ndani ya muda uliopangwa. Dakika niliyofikiria uamuzi huo, hisia ya ajabu ya kujiamini ilinijia kwa namna ambayo kamwe sikuwahi kuhisi hapo kabla. Kitu ndani yangu kilionekana kusema, “Kwanini hukufikia uamuzi huo muda mrefu? Pesa zilikuwa zikikusubiri muda wote !”
Mambo yalianza kutokea kwa haraka. Niliita magazeti na kutangaza kuwa ningeweza kutoa mahubiri(hotuba) asubuhi ya siku iliyofuata yanayohusu, “Ningefanya nini kama ningepata Dola million moja”.‘Nilikwenda kuifanyia kazi hotuba ile mara moja. Ni lazima nikueleze, ukweli haikuwa kazi ngumu kwasababu nilikuwa nikiiandaa hotuba hiyo kwa karibu miaka miwili. Roho yake ilikuwa sehemu yangu !muda kabla ya usiku wa manane nilikuwa nimemaliza kuandika hotuba. Niliingia kitandani na kulala na hisia za kujiamini kwani niliweza kuona mwenyewe kama tayari nilikuwa nazo dolla milioni moja.

Asubuhi iliyofuata niliamka mapema, nikaenda bafuni, nikasoma hotuba, kisha nikapiga magoti na kusali ili hotuba yangu iweze kusikika na mtu ambaye angeliweza kutoa pesa zilizohitajika.‘Wakati nikiwa nasali, tena nilijiwa na zile hisia za kujiamini, kwamba pesa zingeliweza kupatikana haraka. Kwa taharuki niliondoka bila kuchukua hotuba yangu, na sikugundua kosa hilo mpaka nilipokuwa kwenye mimbari yangu na karibu kuanza kuhutubia.

‘Muda ulishakwenda mno kurudi tena kuchukua karatasi, Baraka iliyojea akili yangu ilifikiria vyote ninavyohitaji niakavisema nilipomaliza mikakati ,wakati nimeketi mwanamme mmoj alikuja mbele akanishika mkono akaseam nimeipenda hotuba yako unaweza kupata kiasi hicho ukichokihitaji naitwa Philip Armour.Kesho asubhu alienda ofisini kwake akapewa hicho kiasi cha pesa akaanzisha taasisi ya teknolojia Armor.Dola milioni moja zilipatikana kutokan ana wazo liliotokana ana shauku aliyokuwa nayo muda mrefu,Ndani ya dakika 36 mpango wake ulikamilika na kufanikiwa kupatab kila alicho kihitaji.
Unaweza kupata chochote unachokihitaji kwa kutumia ubunifu wako.

6. Kanuni ya sita kuelekea utajiri ni KUWEKA MIPANGO MATHUBUTI
Umeshajifunza kuwa kila kitu kinachoumbwa na kumilikiwa ukianza na shauku.Shauku hiyo huchukua safari yake ya mwanzo pasipokuwa na kitu chochote mpaka kwenye kitu kinachoweza kushikika katika karakana ya ubunifu mahali ampapo mipango kwa ajili ya mabadiliko huandaliwa.
Katika sura ya pili ulielekezwa kuchukua hatua kama hizi  za kivitendo amabayo kupitia hizo mageuzi haya yanaweza kufanyika.Hapa uanelekezwa namna ya kutengeneza mipango kuwa vitendo:
1.Shirikiana wewe mwenyewe na kundi la watu wengi kadili utakavyohitaji kwa ajili y kutengeneza na kutekeleza mpango wako au mipango yako ya kujichumia fedha,ukitumia kanuni ya ‘’ushirika wa kushirikiana unaleta maendeleo’’.

2.Kabla ujaunda ushirika wako wa kushauriana amua faida zipi na manufaa unayoweza kutoa kwa mwanachama mmoja mmoja wa kundi lako kama malipo ushirikiano wao,hakuna mtu atakayefanya kazi milele pasipokuwa na malipo au kumtegemea mwingine afanye kazi pasipokuwa na malipo yanayofaa ingawaje malipo yale yanaweza yasiwe ya pesa moja kwa moja.
3.Panga kukutana ana wanachama awa kundi lako la kushauriana anagalau mara mbili kwa juma au zaidi kwa malengo makubwa ya kuwezesha uwezekano wakuchuma zaidi pesa.
4.Dumisha masikilizano kati yako na wengine amabao ni wana kikundi cha kushauriana,maana popote pasipo na kusikilizana amna  kitu chochote kinachoendelea,Katika hili zingatia kuyatenda majukumu yako kikamilifu pia kuangalia uezo na ubunifu wao.
Hakuna mtu yeyote mwenye uzoefu wa kutosha,elimu,uwezo wa asili wa kuhakikisha anajipatia utajiri pasipokuwa na ushirikianao na wengine.Mipango mingi inafanikiwa mkiwa katika kundi kubwa la kushauriana pamoja na kuchangiana mada mbalimbali ,maana kuna mipango utakayopanga .Hii itaangaliwana wengine ambao mko nao katika kikundi cha kushauriana.

Ukitengeneza mpango ukashindwa usiache anza upya na mara nyingi zaidi ili ifike hatua ufanikiwe.Mfano Thomas Edison alishindwa zaidi ya mara 1000 kabla hajafanikisha kuunda balbu ya umeme,katika hali hiyo alikutana na vikwazo vingi sana mpaka kufikia hatua ya kubwa ya kuiwasha balbu hiyo.Henry Ford alipata utajiri si kwa sababu alikuwa na akili nyingi bali alikubali kufuata mipango mathubuti mpaka akafanikiwa ,lakini wapo wengi wanaopewa elimu bora kuliko ya Ford lakini bado ni maskini kwa sababu hawana mipango mizuri.
Hakuna mfuasi wa falsafa hii anayeweza kwa makusudi kutegemea kupata utajiri pasipo kukutana na anguko fulani,Anguko linapokuja ni ishara kwamba mipango yako siyo mizuri tengeneza upya mipango yako vizuri usiachie njiani.’’Muachaji kamwe hashindi ,mshindi kamwe haachi’’.
Unapokuwa unachagua watu wa kushirikiana naoa jaribu kuangalia watu wanajari ,wasiopenda kuanguka anguka.wajasiri,amabo wanaweza kujizuia binafsi,matazamo ,uwezo wa kuamua wanaoweza kutengeneza mipango mathubuti hao ndio wanaoweza kukupatia mafanikio/utajiri.

7.Kanuni ya saba kuelekea utajiri ni MAAMUZI

Katika sura hii mwandishi anasema utafiti wa kweli uliofanyika kwa watu zaidi ya 25000 unaonesha wengi wao kitu kinachofanya wanashidwa kufanikiwa ni kushindwa kufanya maamuzi.Wengi wao wanashindwa kufanya maamuzi ya haraka na kuyaghairisha kitu kinachowaletea madhara baadae.
Kuna wakati tunaona fursa ila kutokana na kwamba adui mkubwa kughairisha ametuzingira hivyo tunajikuta tunaipoteza fursa ile.Mfano wa mtu ambaye alikuwa na uharaka katika kutoa maamuzi alikuwa ni Henry Ford amabaye alikuwa ni mkurugenzi wa magari ya “Ford”ambayo yaliamika kuwa na kasi sana.

Watu wengi hushindwa kupata mahitaji yao ya msingi hasa hasa ya kifedha kutokana na kusikiliza maoni ya watu na kuruhusu majungu kutoka kwa ndugu na majirani na kujikuta wanashindwa kufanya maamuzi mazuri wakiofia kuwapoteza.Ili kuweza kuwa na maamuzi mazuri badala ya kufungua mdomo na kuanza kuwaambia yaliyo yako ,Funga modomo fungua macho na masikio ukiufuata ushauri huu utakusaidia sana kuufikia utajiri.Simamia maamuzi yako ,simamia imani yako.Maamuzi ni baba wa IMANI na UJASIRI
Socrate aliona bora kunywa sumu kuliko kubadilisha imani yake na huu ulikuwa ni uamuzi wa busara kwa sababu mengi aliyoyafanya yameisaidia dunia hata na vizazi vinavyokuja.Jiulize je! Maamuzi yangu kuelekea utajiri ni yapi?.

8.Kanuni ya nane kuelekea utajiri ni  UVUMILIVU
Mwandishi anajaribu kuelezea kwa jinsi Uvumilivu ulivyo kitu cha msingi sana  ambacho msingi wake unaleta hamu nia katika ushindi.
Amejaribu kuonesha dalili za mtu mwenye uvumilivu na vitu anavyokuwa amepanga kama ifuatavyo;
(i)malengo ya vitu anavyotaka kuvipata kwa kipindi Fulani. (ii) Hamu ya kufanya kazi yake muda wote. (iii) Anayejitegemea. (iv) Mipango mizuri ya kazi zote anazotaka kuzifanya ili kuufikia utajiri. (v) Anatumia ujuzi  alionao katika kuyatatua magumu anayopitia. (vii)Ushirikiano. (viii) Yuko tayali kubadili tabia mpya lengo kuu ni kuufikia utajiri .
Pia mwandishi amejaribu kuonesha dalili za mtu anayekosa uvumilivu vitu anavyokuwa navyo au anavyoonesha;

(i) Kushindwa kuwa dhahiri kuwa na kitu anachokitaka hapa unamkuta mtu mara anataka kile,ajakaa sawa anataka kingine yeye muda wake wote ni kutaka vitu vingi pasipokuwa na msimamao wa kitu kikbwa kimoja anachotaka.(ii)Mtu wa kughairisha mambo bila kuwa na sababu yoyote. (iii)Anakosa hamu ya kupata maarifa mengine zaidi. (iv)Anakosa kuwa na maamuzi ya msingi mara kwa mara. (v) Tabia ya kuwategemea wengine badala ya kutengeneza njia za kutatua changamoto. (vii) Anakosa matumaini katika kile anachofanya (viii) Anapenda kulalamika kwa makosa madogo madogo yanayofanyika. (ix) Anakosa nia na ni mtu wa majuto muda wote .(xi) Anakosa mipango imara. (xii) Analalamikia umasikini badala ya kuwazia utajiri (xiii) Anapenda kupata badala ya kutoa .(xiv) Anatufa njia za mkato kuupata utajiri (xv) Anaofia sana kukosolewa .

9.Kanuni ya tisa kuelekea utajiri  NGUVU YA AKILI
Mastermind ni kuwa na timu ya watu mahali, ambayo kazi yake ni kukusaidia kufanikiwa na kutekeleza mipango yako. Katika hali hii unachagua watu wanaoendene na wewe kimawazo ili muweze kusaidiana. Hakuna mtu anayeweza kupata nguvu  kubwa ya mafanikio bila ya kuwa na nguvu ya akili yaani mastermind. Kusudi la mastermind ni kubadili maarifa kuwa nguvu, kwa kupanga mipango kuwa  dhahiri  kisha kutafsiri mipango hiyo katika matendo.Jiulize je !watu wangu ninaoungana nao kila siku ni wakina nani?, Majibu yako yafanyie kazi.

10. Kanuni ya kumi kuelekea utajiri SIRI YA USAMBAZAJI WA NGONO
Kitendo hiki huleta furaha kubwa miongoni wa wawili wafanyao kwa wakati sahihi maana huleta hali ya ujasiri, utashi, uvumilivu na uwezo wa ubunifu ambao haujulikani na watu wakati mwingine.Pia ameizungumzia siri ya usambazaji wa ngono katika makundi makubwa matatu;
(i) Utangulizi wa wanadamu
(ii) Utunzaji wa afya
(iii) Mabadiliko ya upatanishi kuwa fikra.
Japokuwa ngono ni nzuri lakini anasema inabidi ifanyike kwa wakati sahihi maana ikiendekeza inaweza kumpoteza mtu kufika katika safari yake ya mafanikio.

11.  Kanuni ya kumi na moja kuelekea utajiri AKILI YA CHINI YA UFAHAMU
Akili ya chini ya fahamu (sub conscious mind ) ni kiunga kinachounganisha kati ya akili laini ya mwanadamu na akili isiyo na mipaka. Akili ya chini ya ufahamu inaweza kutumika kama njia ya kupitisha tamaa zako kuwa sawa na za mwili au pesa.lakini, ukishindwa kupanda matamanio yako ndani yako hautapata matokeo mazuri.
Ili kupata udhibiti wa akili yako unapaswa kutumia faida hizi zifuatazo kuu za hisia zifuatazo: Tamaa, Imani, Upendo, Jinsia, Ushirikiano na Tumaini.
Unapaswa kupata ufahamu zaidi katika vitu hivi ili kuweza kuifikia safari yako ya utajiri Hofu, Wivu, chuki, kulipiza kisasi, Penzi, Ushirikina, Hasira.Tumia ufahamu wako vizuri kwa ajiri ya manufaa yako.

12. Kanuni ya kumi na mbili kuelekea utajiri  ni UBONGO
Mwandishi analinganisha ubongo kama kituo cha Utangazaji ,Kupokea na Kufikiria,Kila ubongo wa mwanadamu ni kituo cha utangazaji na kupokea kwa mtetemeko wa mawazo kutoka sehemu tofauti tofauti.Ubongo wetu na wanyama wengine hauna tofauti kubwa ila tumewashinda tu kwenye kufikiria na kuchukua hatua lakini wao wanaendeshwa kwa hisia tu.Hivyo kama mtu unayetaka kuwa na utajiri kifedha lazima kuruhusu ubongo wako kufikiria kisawa sawa na kuchukua hatua juu ya maisha yako.Kufikiria kunapaswa kuambatana na ubunifu mkubwa wa mawazo mbalimbali yatakayo kupelekea kuupata utajiri.

13. Kanuni ya kumi na tatu kuelekea utajiri  HISIA YA SITA
Mwandishi anailinganisha sixth sense (akili ya sita) kama lango Kwa Hekalu la Hekima
Uelewa wa akili ya sita unakuja tu kwa kutafakari, kupitia maendeleo ya akili kutoka ndani.Mara tu unapofahamu hisia ya sita, utakuwa na uwezo wa kupokea maonyo juu ya hatari zinazokuja kwa wakati ili kuziepuka na kujulishwa fursa za kukumbatia.Akili ya sita haitaweza kamwe kufanya kazi ikiwa mawazo, shaka, na woga zitabaki akilini mwako.
Hofu 6 za msingi ni; Umasikini, Ukosoaji, Afya mbaya, Upotevu wa upendo, uzee, Kifo anaongezea ya saba ambayo ni  ushawishi mbaya. Ili kujikinga na adui huyu, kama watu wote wanaokusanya utajiri mkubwa, lazima uweke matumizi yako ya nguvu kila wakati, hadi ujenge kinga dhidi ya ushawishi mbaya katika akili yako mwenyewe,Tafuta kwa hiari kampuni ya watu wanaokushawishi kufikiria na kutenda kwa mtazamo mzuri, na Tumia nguvu yako ya dhabiti kupata udhibiti wa mawazo yako na ushawishi akili yako ndogo.
Tambua hofu ni hali ya akili tu. Imewekwa chini ya udhibiti na mwelekeo. Tumia maarifa haya kwa faida yako.

MWISHO KWA MAELEZO ZAIDI NA JINSI YA KUJIUNGA NA GRUOP LETU TUMA UJUMBE KUPITIA 0767702659 LACKIUS ROBERT.
KARIBU TUJIFUNZE ZAIDI au bonyeza link hii https://t.me/SOMAONLINETELEGRAM

Saturday, April 04, 2020

UCHAMBUZI WA KITABU CHA THINK AND GROW RICH (FAKIRI NA KUA TAJIRI.Napoleon Hill

Karibu sana katika program ya uchambuzi wa vitabu program inaitwa "SOMA ONLINE'Improve yourself.

JINA LA KITABU THINK AND GROW RICH, (Fikiri na kua tajiri).
MWANDISHI : NAPOLEON HILL
MCHAMBUZI : LACKIUS ROBERT.

KUHUSU KITABU:
Mwandishi Napoleon Hill japokuwa aliandika vitabu vingi kuhusu mafanikio binafsi lakini kitabu hiki chaThink and Grow Rich ( Fikiri na Kua Tajiri ) alichokiandika mwaka 1937 hakujua kama kinaweza kuwa kizuri na  kubadilisha maisha ya watu wengi. Alitarajia kitabadilisha maisha ya watu wachache ila haikuwa hivo kimebadilisha maisha ya wengi.Mimi na wewe tupo bado tunaendelea kujifunza zaidi,naamini hata vizazi vijavyo watajifunza pia. Kuanzia kuchapishwa kitabu cha kwanza mnamo 1937 hadi kifo cha Napoleon Hill mnamo 1970. Kitabu cha Fikiria na Kua Tajiri kimetolewa nakala zaidi ya milioni 20 na tayali nakala hizo zilikuwa zimeuzwa. Tangu wakati huo mauzo yameongezeka mara nyingi zaidi na ni kitabu kilichoorodheshwa miongoni mwa vitabu bora zaidi hata katika karne ya 21.

Mwandishi anasema mawazo yasiyoshikika yanaweza yakageuzwa yakawa ya kushikika kama vile mali mfano  pesa kwa kutumia kanuni mbalimbali endapo mtu akiamua.Chanzo kikubwa cha kuanguka miongoni mwa watu wengi ni  kukata tamaa muda mfupi baada  ya kukutana na vikwazo mbalimbali pindi  waanzapo kazi zao walizopanga.Baadhi wanapoanguka wanashindwa kunyanyuka huku wakianza kutoa lawama kwa watu wengine badala ya kutumia anguko ilo kama funzo.
Mafanikio siku zote humjia mtu ambaye anatumia muda wake kuwaza sio yule asiyewaza na mara nyingi kitu kama utajiri kikija unajiuliza sana kwa nini hakikuja mapema ukiangalia ulivyongaika kuupata lakini utajiri huo unaanza na wazo kichwani mwako.

Lengo kuu la kitabu hiki ni kukuelezea siri za utafutaji fedha,Lakini anasisitiza kuwa siri hiyo uanzia kwenye FIKRA ndiyo maana anasema Fikiri na kua tajiri.
Mwandishi anasema watu wote waliofanikiwa ni wale waliokubali kuchukua hatua za kubadili mawazo yao,Kupitia (semina/warsha)conference mbalimbali walizowahi kuhudhulia.
Pindi wapatapo tatizo hulitatua huru kwa kutafuta suruhu ili kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri.

Hivyo inabidi muda wote uanze kufikiria utajiri ili tayali ata ubongo wako uwe na mazoea ya kufikiria hivyo ili siku ukikutana na magumu isiwe rahisi kuyakubali yakurudishe nyuma.
Mwisho.

Karibu katika uchambuzi wa kitabu cha Think and Grow Rich ,Fikiri kua Tajiri. Kitabu kinafundisha njia za kuelekea kuutafuta utajiri.

Sehemu ya kwanza
1.Hatua ya kwanza kuelekea utajiri ni kuwa na SHAUKU/Tamaa.

Katika sura hii mwandishi anajaribu kumuelezea Bwana mmoja aitwaye Edwin C Barnes ambaye watu walipokuwa wanamuona mtaani walikuwa wanamchukulia kama mzululaji, lakini yeye moyoni mwake alikuwa na shauku kubwa ya kuingia ubia kibiashara na mgunduzi mkubwa wa umeme Thomas Edisoni.
Wakati anaenda ofisi kwa Thomas alikuwa anawaza kama tayali yupo ofisini anafanya kazi licha ya kwamba bado hajafika ofisini na halikuwa anahisi kama tayali yupo mbele ya Edisoni wakizungumza fursa mbalimbali za kibiashara.Miaka michache baadae shauku aliyokuwa nayo kubwa ,au tunaweza kusema ndoto kubwa aliyokuwa nayo Barnes ilikuja kuwa kweli baada ya kuwa katika ofisi moja na Edisoni wakifanya shughuli zao za  kibiashara.Hali hiyo ilipelekea watu wengi waliokuwa wanamjua awali kuanza kumuonea wivu baada ya mafanikio aliyoyapata kutokana ufanyaji biashara na bwana Edison.

Lakini ukija kuangalia Bwana Barnes alitumia muda wake mwingi kuwaza swala hilo na kulichukulia kama kitu ambacho kinaweza kumpatia kile anachokihitaji kwenye maisha yake ,alikataa roho ya woga wa kuzungumza na Bwana Edison.Na haikuwa rahisi kumpata bwana Edison takribani miaka mitano ilipata kabla hajakutana naye ,alikuwa yuko tayali kuanzia chini lakini apate japo nafasi ya kuonana na Edisoni.Hakuwahi kumapata mtu wa kumwambia utaweza labda yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa akiamini itawezekana.
Unaweza kuona nikwa jinsi gani shauku inavyoweza kukusababisha kuwa tajiri baada ya kutumia jitihada.

Karibu katika sehemu ya pili ya uchambuzi wa Think and grow Rich Fikiri na kua tajiri.


KANUNI YA PILI KUELEKEA UTAJIRI:
Ni Kuwa na  IMANI.

Imani ndio mkemia mkuu wa akili,imani inapochanganywa na msisimuko wa fikra iliyo  ndani mara moja huchukua msisimuko kuutafsiri na kuusafirisha kwenda kwa nguvu kubwa isiyo ya kawaida.Mfano ukiangalia imani ,mapenzi na ngono ndivyo vitu vyenye nguvu zaidi kushinda mihemuko yote mikubwa.vitu hivi vinapochanganywa vina athari za kufungua moja kwa moja msitali wa mawasiliano baina ya akili ya kawaida  ya kufikiria na ule uwezo usiokuwa wa kawaida.

JINSI YA KUJENGA IMANI
Imani ni hali ya akili ambayo inaweza kuambukizwa kupitia kukiri au maelekezo  yanayojirudia kwenye akili ya ndani kutona na uwepo wa kanuni za kujishauri wewe mwenyewe,Mfano unaamini kuwa ukifanya kazi yako vizuri utapata pesa nyingi zitakazokufanya wewe kuwa tajiri.Hali hii mara nyingi inatokanaa na jinsi unavyoizoesha akili yako kuwa utapata kile unachoiomba mara zote na kwa wakati wowote.
Ni vema uanze mara moja kuitafsiri yenyewe kuwa kitu halisi ambacho kinawezekana , katika hili kuna hatua kadhaa za kuijenga imani yako.
Mara nyingi imani huanzia katika hali ya fikra,ukomo wa utajiri hupangwa na mtu amabaye ndani yake hautawaliwa na vitendo.Imani huondoa ukomo,mfano ukiangalia mtu aliyeanzisha shirika la chuma cha pua la marekani hakuwa maarufu mpaka alikuwa tu msaidizi wa Andrew Carnegie mpaka pale alipozalisha wazo lake ndipo alipokuwa maarufu akaingia madakarani na akapata utajiri.

Licha ya kwamba Napoleon Hill hakuwa mtu wa dini, lakini aliona thamani ya Imani na kuiona ipo karibu na shauku ya kufanikiwa. Kile ambacho Hill huita Imani kwa kweli ni aina ya kujiamini ambayo ina mipaka juu ya udini. Ilikuwa kanuni ambayo mara moja alijifunza kutoka kwa mshauri wake, millionea wa chuma mkubwa Andrew Carnegie.
Kuna watu walikuwa wanamuuliza Andrew Carnegie ni jinsi gani tunaweza kufanikiwa?, alikuwa anawaambia ukishindwa mara moja usikate tamaa wala kuaanza kupunguza imani yako ya kufanikiwa badala yake ongeza juhudi maana viongozi na watu wengi wenye mafanikio waliinuka kutokana na kushindwa miongoni mwao na ndio maana wamefanikiwa zaidi na zaidi.

Kumbuka.
-Kama unaamini umepigwa tayali umepigwa.
-Kama unaamini unashindwa kuthubutu ,hautaweza kweli.
-Kama unafikiri autashinda katika kile uchofanya tayali umeshindwa.
-Kama unafikiri umepoteza tayali umepotea.

Katika dunia mafanikio yoyote tunayafuta kuanzia kwa marafiki wetu unapaswa kulijua hilo.
Kumbuka imani ni chanzo kibubwa cha utajiri ,imani inaanza na wewe mwenyewe kwa kuamini katika kile unachokifanya na kuongeza juhudi zaidi.
Karibu katika uchambuzi wa kitabu cha Think and Grow Rich ,Fikiri na Kua tajiri.

Dhumuni kubwa ni kukuongezea maarifa juu ya njia za kuzingatia ili uweze kuupata utajiri.

SEHEMU YA TATU: kuelekea utajiri ni KUJISHAURI BINAFSI.

Kujishauri binafsi ni neno linalotumika kwa mawazo yote na vichocheo vyote vinavyosimamiwa binafsi ambavyo hufika katika akili ya mtu kupitia milango mitano ya fahamu.Ni wakala wa mawasiliano kati ya ile sehemu ya akili ambapo fikra za fahamu hutokea na ambayo hudumu kama kiti cha vitendo kwa ajiri ya akili ya ndani.
Kupitia mawazo yanayotawala,mtu huruhusu kubakia katika ufahamu iwe mawazo ni hasi au chanya haijalishi.

Kanuni ya kujishauri binafsi kwa hiyari huifikia akili ya ndani na kuiathiri kwa mawazo hayo.Ukiacha mawazo yanayochukuliwa kutoka angani hakuna mawazo chanya au hasi yanayoweza kuingia akili ya ndani bila msaada wa kanuni  ya  kujishauri binafsi,kwa lugha nyingine maneno yote utambuliwa kupitia milango mitano ya fahamu.
Uwezo wako wa kutumian kanuni hii ya kujishauri binafsi kutategemea nguvu kiasi kikubwa cha ni uwezo uliouweka katika shauku yako ya kupata ile unachokihitaji.

katika sura ya pili kuna hatua sita nilikuelezea  inabidi uweze kuwa imani kubwa ya kile kitu unachokitaka mfano kama unataka pesa nyingi,katika akili yako mwenyewe jione kama una kiasi kamili cha pesa unayoitamani endelea kushikiria mawazo hayo nguvu mpaka utakapoona umbo halisi la pesa.Fanya hivyo kila siku kadri utakavyokuwa uanafanya na imani itakuwa inaongezeka zaidi  fanya mara nyingi uwezavyo usifanye baade ukaacha fanya mpaka uone umezipata.

Katika hatua ya nne kati ya sita kwenye sura ya pili tumefundishwa kuweka mpango kamili kwa ajiri ya kutekeleza shauku yako,anza mara moja kuweka mpango katika vitendo, unapaswa kuanza mara moja usisubilie. Unapowaza akilini mwako fedha ambazo unakusudia kuizipata  jione mwenyewe ukitoa huduma ,au ukianza bidhaa unzokusudi kutoa kama malipo ya hizo fedha hii  hatua muhimu sana kuizingatia.Unavyokuwa unajishauri binafsi unapasw akuzingatia hii ili kuboresha imani yake:

1. Nenda katika sehemu tulivu yenye ukimya inaweza kuwa kitandani au wakati wa usiku,ambapo autasumbuliwa au kukatishwa Fumba macho yako toa sauti yenye kauli ya kiasi cha pesa ulichokusudia kwa jinsi ilivyoandikwa kwenye karatasi.Wakati unafanya hivyo jione kama tayali uko na hicho kiasi,na uweke kwamba labda tarehe 1 mwezi wa kwanza,au baaada ya miaka mitano nitakuwa na kiasi hiki,au kutoa huduma hii,Ninachosubilia ni mpango nitakaoutumia kupata pesa hizi na niatafuata mpango huo nitakapoupokea.

2. Rudia program hii usiku na asubuhi mpaka utakapoweza kuona katika   akili yako pesa unayokusudia kuipata.

3. Weka nakala ya kauli ya maandishi mahali unapoweza kuiona usiku na asubuhi ,Isome kila mara kabla ujalala na wakati unapoamka asubuhi mpaka ikae akilini mwako.Unapokuwa uantumia kanuni hii ujue unatumia kanuni ya kujishuri binafsi,unapaswa kujua imani ndio mhemko wenye nguvu zaidi kushinda zote na wenye faida kubwa zaidi,Uisurusu imani yako iyumbishwa na kitu chochote au kurudi nyuma.

Tukutane siku nyingine.
Nikukumbushe pia unakaribishwa kuchangia pia.
Tuwasiliane kupitia 0767702659 au email maarifarobert @gmai.com
Nakutakia siku njema yenye baraka Mungu akubariki na kukulinda,I'm Lackius Robert karibu.


Friday, April 03, 2020

UCHAMBUZI WA KITABU CHA RICH DAD POOR DAD

Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Rich dad poor dad chake Robert Kiyosaki.


7. SOMO LA SITA: FANYA KAZI KUJIFUNZA ,USIFANYE KAZI KUPATA  PESA.
Nilikuwa na kazi kubwa mbele yangu, lakini nilijiuliza  maswali mengi  ila baada ya miezi sita nilijiunga na kampuni ya Marine Corps kujifunza jinsi ya kuruka. Baba tajiri alinipongeza,Katika shule na mahali pa kazi, maoni maarufu ni wazo la"utaalamu." Hivyo ni, ili kupata pesa zaidi au kukuza, unahitaji"utaalamu." .Vile vile ni kweli kwa wahasibu,wasanifu, wanasheria, marubani na wengineo.Baba yangu aliyeelimishwa aliamini fundisho hilo hilo. Ndiyo sababu alifurahi wakati hatimaye alipata udaktari wake.Baba tajiri alinitia moyo kufanya tofauti kabisa na kusema"Unataka kujua kidogo juu ya mengi "yalikuwa maoni yake. Ndio maana kwa miaka mingi nilifanya kazi ndani na maeneo tofauti ya kampuni zake. Nilifanya kazi pia kama kijana wa mabasi na ujenzi, katika mauzo, kutoridhishwa na uuzaji yote hayo nilifanya. Alikuwa "akimuandaa" Mike na mimi. Ndio maana alisisitiza tukae kwenye mikutano na mabenki yake,wanasheria, wahasibu na madalali, alitaka tujue kidogo juu ya kila mtu tabia na ufalme wake.
Nilipoacha kazi yangu ya kulipwa vizuri kwenye mafuta ya Kawaida, baba yangu aliyesoma alikuwa na kwanini  moyoni  na alikuwa anashangaa. Hakuweza kuelewa uamuzi wangu kujiuzulu katika kazi ambayo ilitoa malipo makubwa, faida kubwa, muda mwingi mbali,na fursa ya kukuza. Aliponiuliza jioni moja, Kwanini umeacha? ,Sikuweza kumuelezea,zaidi maana nilijua haitakua rahisi kunielewa mantiki yangu ilikuwa ya baba yangu tajiri.
KOSA KUBWA ni kwamba wafanyakazi wengi huwa hawafikirii mbele, wao hufanya kile walichonacho wamefundishwa kufanya ambacho ni Pata kazi salama. Wafanyakazi wengi huzingatia kufanya kazi kwa malipo na faida ambazo hulipa katika muda mfupi, lakini mara nyingi huwa mbaya kwa muda mrefu.Badala yake napendekeza kwa vijana kutafuta kazi kwa ili kujifunza zaidi kuliko kile watapata. Mara tu watu wameshikwa katika mchakato wa maisha yote ya kulipa bili, Kwa bahati mbaya, kuna ukweli Fulani kuwa "Hauwezi kufundisha mbwa mzee mbinu  mpya.
Baba yangu tajiri, alitumia maisha yake kufanya bidii kutunza kampuni zake kutokana na kuunganishwa na alifanikiwa, ukitaka kufanikiwa zingatia,
(i) Usimamizi wa mtiririko wa pesa
(ii) Usimamizi mzuri wa  mifumo
(iii) Usimamizi wa watu.
Ujuzi muhimu zaidi ni mauzo na uelewa
Uuzaji ,Ni uwezo wa kuuza,kwa hiyo kuwasiliana na mwanadamu mwingine awe mteja,mfanyakazi, bosi, mke au mtoto  huo ni ujuzi wa msingi wa mafanikio ya kibinafsi. Ni ustadi wa mawasiliano kama vile kuandika, kuongea na kujadili ambayo ni muhimu kwa maisha ya kufaulu.
Uelewa Ni ustadi ambao unafanya kazi juu yake mara kwa mara, kuhudhuria kozi au kununua kanda za elimu kupanua maarifa yangu.Kama nilivyosema, baba yangu aliyesoma alifanya kazi kwa bidii.

8. ONDOKANA NA VIZUIZI/VIKWAZO
Mara  watu wanaposoma na kufundishwa elimu ya  kifedha, wanapata uwezo wa kupambana na vizuizi na kuwa na uhuru wa  kifedha.Mwandishi anasema kuwa sifa za ubinadamu zinaathiri sana utu wetu yaani woga, ubeuzi, tabia mbaya, wasiwasi na kiburi.
Woga wa kupoteza pesa, Anasema hajawahi kutana na tajiri ambaye hakuwahi kupoteza pesa. Njia rahisi ya kupambana na woga ni kuanza mapema na weka mipango. Ni kawaida kwa binadamu kuwa na woga lakini ni vipi anakabiliana nao.
Anazungumzia kikwazo cha pili ambacho ni ubeuzi,Ni kitu kinachowarudisha nyuma watu wengi. Hii ni tabia ambayo mtu anakuwa na mtazamo wake binafsi. anaweza amini kuwa duniani hakuna jema. Anayewezahisi harufu ya maua na kujua kuwa karibu yake kuna makaburi kwa sababu mara zote anajua kuwa maua hupandwa makaburini. Mwandishi anasema watu wanazipoteza fursa nyingi sana kwa sababu ndogo sana. Kwamba hawawezi kuwekeza kwa sababu wanaogopa kupoteza pesa.
Kikwazo kingine ni uvivu,Anasisitiza kuwa kama umepata au kupewa wazo usiseme huwezi kumudu bali sema ni vipi ntaweza kufanya?
Kikwazo cha nne ni tabia mbaya, Anazungumzia kuwa lazima ujilipe kwanza mwenyewe kabla ya kulipa kodi na ushuru. Baba maskini hulipa kodi na ushuru ndipo anaanza kutumia pesa. Anasisistiza kutafuta vyanzo vingine vya kukufanya ulipe kodi na ushuru.
Kiburi au majisifu, Kikwazo hiki pia kimezungumzwa na mwandishi. Watu wengi wanatumia kiburi kuficha ujinga wao. Watu wengi wanafanya biashara na wanawekeza lakini hawana ujuzi wa fedha. Ni bora kujifunza Zaidi na Zaidi kuliko kujifanya unajua
Mwandishi anasema watu wengi wanasikika wakisema wanapenda kuwa matajiri lakini ukiwashauri kuwa pesa inatengenezwa kwa kuwekezwa kwenye vitega uchumi na mali faida wanadai watakula nini Leo na muda wote huo wakati wanasubiri mafanikio hayo kuyapata.

9. KUANZA
Nalidhani  kupata utajiri kwangu ingekuwa rahisi ,lakini haikuwa hivyo.
Kwa hivyo kujibu swali "Nitaanzaje?"
Ninatoa mchakato wa mawazo niliopitia, linapokuja swala la pesa, ni uamuzi kupata njia ya kutetemeka hiyo ni jambo la kibinafsi. Naamini kila mmoja wetu ana fikra za kifedha ndani yake. Shida ni kwamba, akili yetu ya kifedha imelala, na kungojea kuitwa.Huu ni uongo kwa sababu tamaduni yetu imetuelimisha kuamini hivyo kupenda pesa ndio mzizi wa mabaya yote. Imetutia moyo kujifunza taaluma ili tuweze fanya kazi kwa pesa, lakini umeshindwa kutufundisha jinsi ya kufanya kazi ya pesa kwetu. Ilitufundisha tusiwe na wasiwasi kuhusu hatma yetu ya kifedha, kampuni yetu au serikali itatutunza wakati wetu siku za kazi zi mekwisha. Walakini, ni watoto wetu, waliosoma katika mfumo huo wa shule, ambao itaishia kulipia. Ujumbe bado ni kufanya bidii, pata pesa na uitumie, na lini tunakimbia kifupi, tunaweza kukopa zaidi zaidi.
Kwa bahati mbaya, asilimia 90 ya ulimwengu wa Magharibi wanakubali mafundisho haya hapo juu, kwa sababu tu ni rahisi kupata kazi na kufanya kazi kwa pesa. Ikiwa wewe sio mmoja wa raia, ninakupa kufuata hatua kumi za kuamsha fikra zako za kifedha kama ifuatavyo;

(i) Tafuta sababu ya kufanya kuliko ukweli au uhalisia wa kukufurahisha: Hapa anamaanisha kuwa kuamsha maarifa ya uchumi kwa kuisaidia akili yako. Tafuta sababu ya kufanya yenye nguvu kuliko uhalisia wa mambo,hivyo kama mtu anayependa mafanikio lazima awe na majukumu makubwa ya kimaisha na sio kukaa tuu na kufikiria vitu vidogovidogo.
(ii). Nachagua kila siku: Nguvu ya uchaguzi, Hiyo ndiyo sababu kuu watu wanataka kuishi katika nchi huru. Tunataka nguvu ya kuchagua.Mfano kifedha, kwa kila pesa tunayopata mikononi mwetu, tunashikilia nguvu ya kuchagua hatma yetu kuwa tajiri, masikini au tabaka la kati. Tabia zetu za matumizi zinaonyesha sisi ni nani. Watu masikini wanayo tabia duni ya matumizi. Watu wengi huchagua sio kuwa tajiri. Kwa asilimia 90 ya idadi ya watu, kuwa tajiri ni "sana shida. "Kwa hivyo wanazindua maneno ambayo huenda," Sina nia ya pesa, Sitakuwa tajiri kamwe. Shida na taarifa hizo ni wanamuibia mtu anayechagua fikiria mawazo kama haya ya vitu viwili:
 wakati, ambao ni mali yako ya thamani zaidi, na kujifunza. Kwa sababu tu hauna pesa, haipaswi kuwa kisingizio cha kutojifunza. Lakini hiyo ni chaguo sisi sote hufanya kila siku, uchaguzi wa kile tunachofanya na wakati wetu, pesa zetu na kile tunachoweka vichwani mwetu. Hiyo ndiyo nguvu ya chaguo. Wote tunao uchaguzi ,kazi kwako kuchambua ,Ninachagua tu kuwa tajiri, na mimi nilifanya chaguo hilo kila siku. Mali ya kweli ulinayo ni akili yako, ndio zaidi zana yenye nguvu tunayo kutawala juu. Kama tu nilivyosema juu ya nguvu ya uchaguzi, kila mmoja wetu ana uchaguzi wa yale tunayoweka katika akili zetu mara tu tutakapokuwa na umri wa kutosha.
(iii) Chagua marafiki wako kwa uangalifu, Kwanza kabisa, sijachagua  marafiki kwa taarifa zao za kifedha. Nina marafiki ambao wamechukia kiapo cha umaskini na pia marafiki wanaopata mamilioni kila mwaka. Jambo ni kwamba ninajifunza kutoka kwa wote, na mimi kwa uangalifu kufanya bidii ya kujifunza kutoka kwao.Ukweli ni kwamba sijawatafuta kwa sababu ya pesa zao, bali nilikuwa natafuta maarifa yao. Katika visa vingine, watu hawa ambao walikuwa pesa wamekuwa marafiki, lakini sio wote.Nakushauri kuwa makini katika uchguzi wa marafiki wako.
(iv) Ijue kanuni yako na kujifunza  kitu kipya: Ishike kanuni na jifunze kanuni mpya. Mwandishi anazungumzia umhimu wa kujifunza haraka na kujifunza mambo mengi mengi. Jifunze namna ya kufanya jambo fulani vizuri zaidi na kubadilika haraka.Chagua kile unachosoma kwa uangalifu. Linapokuja suala la pesa, wazee kwa ujumla wana formula moja ya msingi waliyojifunza shuleni. Na hiyo ni, fanya kazi kwa pesa. Mfumo ninaouona ambao ni muhimu katika ulimwengu ni kwamba kila siku mamilioni ya watu huamka na kwenda kufanya kazi, kupata pesa, kulipa bili, vitabu vya ukaguzi wa mizani, nunua pesa za kuheshimiana na kurudi kazini. Hiyo ndiyo njia ya msingi, au kichocheo.  Ikiwa umechoka na kile unachofanya, au hautengenezi vya kutosha, ni kesi ya kubadilika formula kupitia ambavyo unapata pesa. Kwa hivyo baada ya kufahamu utaratibu huo, nilienda kutafuta njia zingine, Kwa madarasa mengi, mimi sikutumia habari niliyojifunza moja kwa moja, lakini kila wakati nilijifunza kitu kipya. Nimehudhuria madarasa iliyoundwa kwa wafanyabiashara . Nilikuwa mbali na ligi yangu, nikiwa kwenye chumba kilichojaa watu na madaktari katika fizikia ya nyuklia na sayansi ya anga. Walakini, nilijifunza mengi ambayo yalifanya hisa yangu na uwekezaji wa mali isiyohamishika yenye maana zaidi na faida kubwa.
(v) Jilipe mwenyewe, Hapa anataka kila mtu aweze kujilipa mwenyewe hata kama ni kiasi kidogo sana. Watu wengi hawafanyii kazi suala la kujilipa kwanza, hakikisha unapunguza madeni na kama yapo basi yasiwe yanakurudisha nyuma.Unaweza tenga asilimia kadhaa kutoka kwenye kipato chako labda asilimia 10 au pungufu ukawa unaihifadhi kwa ajiri ya matumizi yako ya msingi na ikitokea ni mradi basi faida unayopata ndiyo unayoitumia.
(vi) Walipe madalali wako vizuri, Hawa ni watu muhimu kwako kuweza kuwajari na kuwalipa vizuri."DALALI." Baba yangu tajiri alinifundisha kuchukua jukumu la kukabili. Aliamini katika kulipa wataalamu vizuri, na mimi wamepitisha sera hiyo pia. Leo, nina mawakili wa gharama kubwa, wahasibu, na mali isiyohamishika madalali na wafanyabiashara. Kwa nini? Kwa sababu ikiwa, na ninamaanisha ikiwa, watu ni wataalamu, wao huduma zinapaswa kukufanya pesa. Na pesa zaidi wanazotengeneza, pesa zaidi mimi hutengeneza. Tunaishi katika enzi ya Habari. Habari haina thamani, Dalali mzuri anapaswa kukupa habari na pia chukua wakati wa kukuelimisha. Nina madalali kadhaa ambao wako tayari kufanya hiyo kwangu na wengine walinifundisha nilipokuwa na pesa kidogo au sina pesa, na bado mimi niko nao.
(vii) Kuwa  mtoaji:kuna msemo unasema unachokitoa nicho unachokipata li kuweza kupata uhuru wa kifedha inabidi uwe unatoa kwa watu wenye uhitaji ili na wewe ukiwa unahitaji upate zaidi.
(viii) Mali za faida: Anasema unapopata pesa wekeza kwanza katika asset(faida)  ndipo ununue bidhaa za anasa.
(ix) Uhitaji wa mashujaa: Anahamasishwa na uwepo wa watu kama Warren Buffet na Donald Trumph. Anavutiwa na mafanikio yao, kujiamini na uzoefu wao katika kutafuta mafanikio na njia walizaopitia kuyapata.
(x) Fundisha utarajie kupata: Baba yangu tajiri alinifundisha hili somo nalimebeba maisha yangu yote,Baba yangu tajiri alitoa pesa na elimu,Aliamini kabisa katika kutoa zaka,hivyo ukitaka kupata kitu unahitaji kwanza kutoa.Baba yangu tajiri lalikuwa akisema kila mara fundisha utarajie kupata zaidi .
10. Bado Unataka Zaidi?
Hapa kuna baadhi ya mambo  ya Kufanya watu wengi wanaweza kutoridhika na hatua zangu kumi. Wanaaona zaidi kama falsafa kuliko Vitendo. Nadhani kuelewa falsafa ni muhimu kama hatua. Kuna mengi watu ambao wanataka kufanya, badala ya kufikiria, na kisha kuna watu ambao hufikiria lakini hawafanyi. Mimi naweza kusema kwamba mimi ninapenda maoni mapya na ninapenda kupiga hatua.Hivyo kwa wale ambao wanataka "kufanya" jinsi ya kuanza, nitashiriki nawe mambo kadhaa ambayo mimi nilifanya, kwa fomula iliyofupishwa.
Acha kufanya kile unachofanya, Kwa maneno mengine, pumzika na uone ni nini kinachofanya kazi na nini haifanyi kazi.Kuna watu hufanya jambo moja na wanatarajia matokeo tofauti. Acha kufanya kile kisichofanya kazi na utafute kitu kipya cha kufanya. Tafuta maoni mapya kwa maoni mapya ya uwekezaji, mimi huenda kwa duka la vitabu na hutafuta vitabu tofauti na masomo ya kipekee. Kwa mfano, nilikuwa katika duka la vitabu ambapo nilipata kitabu The 16 Percent Solution, cha Joel Moskowitz. Nilinunua kitabu hicho na kukisoma. Niliamua KUCHUKUA HATUA, Alhamisi iliyofuata, nilifanya kama vile kitabu kilivyosema. Hatua kwa hatua.Nilifanya hivyo kwa kutafuta biashara ya mali isiyohamishika katika ofisi za mawakili na katika benki. Watu wengi hawafanyi hivyo chukua hatua, au wacha mtu azungumze kwa aina yoyote mpya wanayojifunza.
Tafuta mtu ambaye amefanya kile unachotaka kufanya, Wapeleke kwenye chakula cha mchana,Waulize vidokezo, kwa hila kidogo za biashara. Kuhusu vyeti vya uwongo vya kodi ya asilimia 16, nilienda kwa ofisi ya ushuru ya kaunti na kupatana na mfanyikazi wa serikali ambaye alifanya kazi katika ofisi. Niligundua kuwa yeye kuna uwekezaji aliufanya. Mara moja, alialikwa kwenye chakula cha mchana. Alifurahi kuniambia kila kitu yeye alijua na jinsi ya kuifanya baada ya chakula cha mchana, alitumia alasiri yote akinionesha kila kitu. Siku iliyofata nilipata mali mbili kubwa na msaada wake na tumekuwa tukipata riba ya asilimia 16 tangu hapo. Ilichukua siku kusoma kitabu, siku ya kuchukua hatua, saa ya chakula cha mchana, na siku kwenda pata mikataba miwili mikubwa.
TAFAKARI:
Utajiri ni wa kila mmoja,kila mtu alenge kumiliki mfumo au njia zake za kibiashara na sio kufanya kazi za watu wengine. Kufanya kazi kwa mtu mwingine ni kunyonywa ,akili ya kiuchumi ni rasilimali ya thamani na yenye nguvu kuliko zote. Maarifa ya fedha ni mhimu zaidi,kuliko kutengeneza mnyororo wa matumizi na kushindwa kujenga vitega uchumi kama uwekezaji.

Ni matumaini yangu kuwa umejifunza mengi kutokana na chambuzi hizi kilichobaki ni kwako kuchukua hatua.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa" 
Kwa mawasiliano na kupata chambuzi zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu tujifunze zaidi au email maarifarobert@gmail.com.
Mungu akubariki.

UCHAMBUZI WA KITABU CHA RICH DAD POOR DAD

Karibu katika mwendelezo wa uchambuzi wa kitabu cha Rich dad Poor dad chake Robert Kiyosaki.


3. SOMO LA PILI: KWANINI TUNAFUNDISHA ELIMU YA FEDHA?
Katika sura hii Robert Kiyosaki anaelezea zaidi kwamba rafiki yake Mike alichukua mali za baba yake na akazitunza vizuri mpaka kuwa na mafanikio.Robert na mke wake Kim walistaafu mwaka 1996 akiwa na umri wa miaka 47 na mke wake 37 .Kustaafu kwao hakukumanisha kuwa waliacha kufanya kazi .Ila kipindi hicho walikuwa wanafanya kazi zao  zingine na pesa ilikuwa inaingia na yeye aliona hali hiyo kama uhuru wa kifedha.Hivyo mike alichagua kutumia ufalme wa baba yake na Robert alichagua kustaafu.
Watu wengi wanakuwa wakiniuliza kuwa ninapataje pesa ?  Na wao wanaweza wakaanzia wapi ? na nini siri ya mafanikio nimekuwa nikiwajibu hivi:
Kama wako tayali kuendana na mabadiliko na kufungua akili yao pamoja na kujifunza watakuwa matajiri na matajiri kwa sababu fedha bila kuwa na ufahamu wake itapotea bule.
Ili kuwa milionea haijalishi kiasi gani unapata bali kiasi gani umewekeza na kiasi gani unazalisha kwa sasa.Ukitaka kuwa tajiri unapaswa kuwa na elimu ya fedha( financial literacy).Ndio maana mimi na   Mike tunauwezo mzuri wa kuhifadhi pesa zetu ,tuna msingi mzuri wa fedha tuliofundishwa na Baba yetu tajiri.
Shule zetu hazituandalii msingi mzuri kuhusu fedha bali zinatuandalia ufaulu mzuri na kupata kazi yenye mshahara mzuri.Kama unataka kuwa tajiri lazima ujue kutofautisha faida (asset) na hasara ( liability).Asset ni kitu kinachoingiza fedha mfukoni lakini liability ni kitu kinachotoa fedha mfukoni.Matajiri wanahifadhi vitu vinavyowaletea faida lakini watu wa kipato cha kati wanamiliki vitu ambavyo haviwaingizii faida wanadhani ni faida kama mchoro unavyoonesha.

Ø  Mchanganuo wa mapato kwa mtu masikini                                      
 KAZI
MAPATO
MSHAHARA
MATUMIZI
Kama vile
Kodi ya serikali
Chakula mavazi ,kodi ya nyumba n.k

Faida na hasara kwa mtu maskini hapo ni kwamba fedha inaimgia na kutoka hakuna unachobakiza.
Ø  Mchanganuo wa mtu wa kipato cha kati
KAZI
MAPATO
MSHAHARA
MATUMIZI KAMA :
Kodi ya nyumba
,shule,malipo ya rehani.

    MADENI kama; Mkopo wa nyumba,shule na kadi za benki.




Ø  Mchanaganuo wa kipato cha tajiri

MAPATO(income) KAMA:
Kodi za nyumba,uaminifu,
Mgawanyo wa riba.

MATUMIZI(expances)
Kodi na malipo rehani.
Assert(faida)                            Liability (hasara)
Hisa ,Nyumba.                        
                                    Malipo ya kodi             rehani,Kadi za Benki.

Kwa ufupi  ili kuwa tajiri au kupata uhuru wa kifedha inabidi mapato yako yawe chini ya matumizi  yako.Ukiangalia michanganuo   mitatu hapo juu  utakuja kugundua kwamba maskini pamoja na mtu wa kipato cha kati bado wako kwenye madeni kipato chao havilingani na matumizi yao .Lakini tajiri kipato chake na matumizi yake havijapishana  ndiyo maana matajiri wataendelea kuwa matajiri na maskini na watu wa kipato cha kati watazidi kuwa masikini.
4. SOMO LA TATU : FANYA SHUGHULI ZAKO MWENYEWE.
Unapokuwa unamfanyia kazi mtu mwisho wa siku hautatoka na chochote atabaki nacho yeye,kama unahitahi kuacha mapambano ya kifedha fanya kazi zako mwenyewe,mfano ukiangalia wafanya kazi benki,wanasayansi wahasibu wote hawa shule imewaandaa kufanya kazi nakupata kupata mshahara lakini baada ya kustaafu hawabaki na kitu chochote.
·         Utaalamu wako kipato chako
·         Mali zako kipato chako.
Kuna utofauti mkubwa kati ya utaalamu wako wa kazini na shughuli zako mwenyewe mfano Robert wakati anazungumza na  wafanayakazi wa benki aliwauliza hivi nyinyi  shughuli zenu ni zipi ?, wakasema za kibenki, mkimaliza inakuwaje wakasema  tunaziacha. Ukimlinganisha  mtu mwenye shughuli zake anaendelea kubaki nazo.Tatizo linaokumba wasomi wengi ni kwamba wanakuwa walichokisomea, kama umesomea uhasibu utafanya kazi benki,kama umesomea mpishi utakuwa mpishi kama umesomea sheria utakuwa jaji kama umesomea ualimu utakuwa mwalimu na wengine hawajiongezi katika kufanya shuli zao wenyewe wanaendelea kuwafanyia kazi na kuwatajirisha mabosi.
Ukitaka kuwa tajiri fanya uwekezaji ambao utakuondoa kwenye madeni,vile vile watoto wetu tuwaandalie mazingira mazuri ya kuwafundisha elimu ya fedha na jinsi ya kufanya uwekezaji sahihi kama;
(i)  Mfumo mzuri wa biashara ambao hata kama haupo unajiendesha wenyewe (ii) Stock( hisa)
(iii) Bond( dhamana),(iv) Mutual fund (mfuko wa pamoja),(v) Motes( vidokezo),(vi) Royalities intellectual property such as music, scripts, patents,(vii) Real estate( Mali isiyohamisika)mfano nyumba.
Kama mtoto akifundishwa hivi pia na mzazi akazingatia vitu hivi kwa kufanya kazi zake mwenyewe tayali atakuwa na uwezo mkubwa wakupata uhuru wa kifedha.
5. SOMO LA NNE: HISTORIA YA KODI  NA NGUVU YA MASHIRIKA.

Mwandishi anazungumzia kuwa kodi siku zote inawanyonya wazalishaji mali na kuwafaidisha wasiokuwa wazalishaji mali ,Hii kwake anaona sio sawa matajiri siku zote hutafuta namna ya kukwepa kulipa kodi lakini maskini wanalipa kodi kubwa sana kuliko hata kipato chao.
Pia anasema masikini wanaendeshwa na mashirika wakati matajiri wanayaendesha mashirika na wanayatumia kupata pesa,Wanatumia mashirika haya kulinda kuboresha vitega uchumi vyao. Wanayatumia mashirika haya kukwepa kodi,Wanajua kuyadanganya mashirika na kupata pesa zaidi,Wanachukua pesa, wanalipa kodi, na kuishi kwa pesa zilizobaki.Masikini wananyonywa na mashirika haya lakini hawajui kama wananyonywa. Ili kuwa tajiri ni mhimu kila mtu akaanzisha biashara ya kwake. lazima kila mtu ainue IQ yake ya uchumi, ujuzi wa soko, utunzanji wa fedha na uwekezaji.Pia anasema
Ninaposema shirika ni idara maalumu mfano kampuni inayoundwa ili kushughulikia usimamizi na utekelezajiwa shughuli maalumu kama vile za kibiashara,Mfano hapa Tanzania kuna Shirika la Reli ,Shirika la habari n.k.
Mwandishi anajaribu kelezea kidogo kuhusu kuanziswa kwa kodi nchini marekani na uingereza anasema kodi hizo zilianzishwa kwa lengo kubwa la kupambana na hasara iliyojitokeza kutokna na uwepo wa vita.Katika swala la kodi kuna watu wanajiuliza mbona maskini na tajiri wanalipa kodi sawa kwanini matajiri wasilipe kodi tofauti na maskini?.Anasema matajiri wanajua vizuri nguvu ya ushirika na wanawekeza huko kuliko watu wa kipato cha kati na maskini.
Nikikumbuka katika somo la kwanza kuhusu nguvu, unapofanya kazi kupata pesa unakuwa huna nguvu ya kujiongoza mwenyewe bali unampa nguvu mwajiri wako , lakini pesa inapokufanyia kazi unakuwa na uwezo wa kuithibiti ipasavyo.Baba msomi alinambia niende nikafanye kazi kwenye shirika kubwa nipate pesa zaidi lakini baba Tajiri anasema kwanini nisiwe nasimamia mshirika yangu? ,Nilipokuwa mdogo sikuwahi kumuelewa, nilianza kumuelewa nilipofikisha miaka 20 ,na ilipofika mwaka 1974 wakati bado ni mwajiriwa nilifungua kampuni yangu na nilikuwa nawafariji wafanyakazi wangu.
Ninawakumbusha watu kuwa elimu ya msingi wa fedha  imeundwa na maarifa kutoka makundi  manne ambayo ni;
 (i) Uhasibu, Ambayo ninaiita ujuzi wa kifedha ,Ujuzi muhimu ukiwa unataka kujenga msingi mzuri wa pesa zaidi unayoitaka. Huu ndio upande wa kushoto wa ubongo. Ujuzi wa kifedha ni uwezo wa kusoma na kuelewa taarifa za kifedha , uwezo huu hukuruhusu kutambua nguvu na udhaifu wa biashara yoyote.
 (ii) Uwekezaji, Ambayo ninaiita sayansi ya utengenezaji  pesa, hii inajumuisha mikakati na kanuni za upataji pesa. Huu ndio upande wa kulia wa ubongo, au upande wa ubunifu.
(iii) Kulielewa soko, Sayansi ya usambazaji na uhitaji. Kuna haja ya kujua mambo haya kiufundi  kuhusu kulifahamu  soko, ambayo huchochewa na hisia, Sababu nyingine ya soko huu ni msingi au hali ya kiuchumi ya uwekezaji. Watu wengi wanafikiria dhana za kuwekeza na kuelewa soko ni ngumu sana kwa watoto. Wanashindwa kuona kwamba watoto  ni vema wakawa wanajua masomo hayo kiundani wakiwa bado watoto.
 (iv) Sheria, Kwa mfano, kutumia shirika lililofunikwa kwa ustadi wa kiufundi wa uhasibu, uwekezaji na uelewa wa masoko yanaweza kusaidia ukuaji wa kifedha. Mtu aliye na maarifa ya faida ya ushuru na ulinzi inayotolewa na shirika anaweza kupata utajiri haraka sana kuliko mtu ambaye ni mfanyakazi au mmiliki wa biashara ndogo ndogo. Ni kama tofauti kati ya mtu anayetembea na mtu anayeruka.
6. SOMO LA TANO: MATAJIRI WANAWEKEZA KWENYE FEDHA.
Nimekuwa nikifundisha tangu 1984 nimekuwa uzoefu mzuri na pia na  kutoa taaluma niliyonayo.
Nilifundisha maelfu ya watu binafsi na ninaona jambo moja katika sisi sote kuwa tuna uwezo mkubwa, na sote tumebarikiwa na zawadi. Bado, jambo moja ambalo linashikilia yote kwetu nyuma ni kiwango cha kujiona tunajua. Sio ukosefu mkubwa wa habari za kiufundi ambayo zinatuzuia, lakini zaidi ukosefu wa kujiamini. Baadhi huathiriwa zaidi kuliko wengine mara tu tukiacha shule, wengi wetu tunajua kuwa swala la digrii za chuo kikuu au darasa zuri ndio zinahesabu mafanikio,kumbe unaweza pata mafanikio makubwa kupitia elimu ambayo haukufundishwa shuleni.
Katika uzoefu wangu wa kibinafsi, fikra zako za kifedha zinahitaji maarifa ya kiufundi pia ujasiri. Ikiwa hofu ni kubwa sana, akili hukandamizwa. Katika madarasa yangu nawasihi sana wanafunzi,jifunze kuchukua hatari, kuwa na ujasiri, kuiruhusu akili zao zibadilishe woga huo kuwa nguvu na uzuri. Nilinafanya kazi kwa wengine na nimegundua kwamba kwa watu wengi, wakati inakuja mada ya pesa, wangeamua kucheza salama. Nimelazimika kuhoji maswali kama haya kama, Kwa nini uchukue hatari? Kwa nini nijisumbue kukuza IQ yangu ya kifedha? Kwa nini niweke fedha kusoma na kuandika?.
Kuna mtu kama Bill Gates na kampuni zake  Microsoft zinazoundwa kila mwaka kote ulimwenguni na kote zinafanya kazi vizuri  ,sio kwamba yeye hana woga bali anathubutu na kuwekeza kwenye pesa ili imsaidie baadae hivyo ni vema  kufurahisha zaidi kuwa hai. Ningependa kufurahi juu ya kutengeneza mamilioni kuliko kuwa na wasiwasi juu sio kupata kipato. Kipindi hiki tulicho sasa ni kipindi cha kufurahisha zaidi mambo ambayo hayajawahi kufanywa ndani ya historia ya ulimwengu, na tutafurahia zaidi endapo tukiwekeza kwenye pesa.
Tutaendelea na sehemu sa Saba wakati mwingine.

karibu upate uchambuzi wa vitabu vingine ,nitumie ujumbe kupitia namba 0767702659 au email
maarifarobert@gmail.com.
Karibu tujifunze zaidi.