Sunday, March 24, 2019

UMUHIMU WA KUWA FURAHA


Furaha ni utulivu ulio ndani ya nafsi ya mtu mwenyewe,mara nyingi msingi wa Furaha uleteleza utulivu wa Mwili na Roho ambavyo uleta matumaini na upendo kwa ndani ya nafsi ya mtu.
Wakati mwigine ili kuipata  vema  kukaa na watu wanaokupa furaha na kufanya mambo yanayokupa furaha, . Watu wengi wanakosa furaha na amani na kujaa na msongo wa mawazo katika maisha yao ya kila siku hasa makazini, majumbani, kifamilia.
Kama unaamini kuwa unakosa furaha kutokana na ugumu wa maisha, haujapata kazi, unasumbuliwa na mahusiano, umefeli kwenye masomo, umetengwa kwenye familia, unatafuta mtoto lakini hupati na mengine kadha wa kadha inabidi  ubadilike kwani hata ukifanikiwa kuvipata vitu hivyo unavyovihitaji kamwe furaha yako haiwezi kukamilika kutoka na tabia za asili za binadamu.

Msomaji wa BLOG Hii Naomba nikushirikishe kidogo umuhimu kwa kuwa na furaha maishani;
 Kuwa na furaha kunalinda moyo wako
Utafiti unaonesha kuwa asili ya upendo na furaha siyo moyoni lakini husaidia kuulinda huku ikibainika kuwepo kwa uhusiano baina ya furaha na vipimo vingine vya afya ya moyo kama vile muda unaotumika wakati wa pigo moja la moyo na lingine na kuzilinganisha na hatari kadhaa za magonjwa ya moyo.
Furaha huzuia mkazo
Makazo yaani sterss hausababishi matatizo ya kisaikolojia pekee bali pia husababisha mabadiliko ya kibiology katika homoni zetu na shinikizo la damu. Furaha inatajwa kupoza hasira za athari hizi na wakati mwingine kutusaidia kurudi katika hali ya kawaida kwa haraka.

VITU VYA KUEPUKA
Hali ya kukata tamaaa,
Walio wengi hali hii imetukumba sana na tumeikosa furaha lakini ili  uweze kuwa na furaha ya kudumu epuka kukata tamaa au kukatishwa tamaa na mtu, kwa sababu kitendo cha kuruhusu kukataa tamaa ni hatua ya mwisho ambayo hauna uwezo wowote wa kujitoa.Kamwe usiruhusu hali hiyo jitahidi kuishi kwenye mtazamo chanya muda wote kuwa utafanikiwa kila jambo unalopigania hata kama ukifeli usikate tamaa utayashinda.
Epuka kutoridhika,
Katika maisha hakuna hatua ambayo mwanadamu utafika na kusema kuwa umeridhika kwa maana hata mwandamu apewe kitu gani hakuna wakati atakaposema inatosha.Wengi wamepoteza furaha kutokana na kutoridhika,akipata kitu hiki anataka kingine . Simaanishi watu waridhike  nachomanisha kiridhika na unachokipata kutegemeana na hali ya kipato chako.Mfano kama auna uwezo wa kunua gari na unatarajia upate furaha baada ya kupata gari itachukua muda hio furaha yako kuipata kama ukifeli usikate tamaa utayashinda.

Ni matumaini yangu kwamba umeweza kuongeza kidogo uelewa namna furaha ilivyo bora katika maisha yetu.
Kauli za washindi nikwamba hawakubali kuikosa furaha .Je mimi na wewe tunaikosaje kwa mfano?.
''Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa''
Kwa maoni na ushauri maarifarobert@gmail.com
Instagram @lackiusrobert
KARIBU.


Friday, March 22, 2019

MAISHA NA MAFANIKIO

Kuna wakati maisha yetu kwa mambo tunayopitia tuyafananishe na maisha ya mtoto mdogo.

Mtoto anapofikia muda fulani uwa anajaribu kusimama lakini anashindwa na kuanguka chini.Lakini hawezi kumlaumu,kusikitika au kununa kisa mama yake kamuacha kaanguka.Baada ya muda kidogo hujaribu tena na tena ,kadri siku zinavyozidi kusogea anazidi kujaribu na kupata uzoefu.

Baada ya muda anajikuta anasimama vizuri na kutembea pia.Yote anayoyapitia waga hakumbuki wala kujutia.

Mara ngapi tumekutana na heka heka katika maisha yetu? Na tumejuta na kutoa lawama Mara ngapi? .Tukisema kwanini Mimi tu.Lakini tukumbuke   hakuna  kilichoanza bila msingi,heka heka zinakujengea msingi Fulani katika maisha,na wakati mwingine tujifanye kama mtoto mdogo tukianguka tunasimama tena na ikiwezekana kutembea.

" Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Karibu katika blogu hii ya Daraja LA mafanikio uzidi kupata vitu moto moto.
Nitumie ujumbe au maoni kupitia
 maarifarobert @gmail.com
Instagram @lackiusrobert

KARIBUNI.

Wednesday, March 20, 2019

MAANDALIZI KATIKA MAFANIKIO

Mafanikio yoyote yanahitaji muda  na maandalizi ya kutosha
Ili uweze kufanikiwa ni lazima vitu vifuatavyo uvizingatie;

 upambanaji ,inabidi kupambana kufa na kupaona kuhakikisha kile unachokitafuta unakipata.Lakini pia inakubidi ujiulize kwanini wewe tu,kwa kujiuliza na kupata majibu fulani fulani yatakuweka katika hatua nzuri kuelea mafanio yako.

uvumilivu;miongoni mwa hatua kubwa zilizofanya watu wengi wenye mafanikio ni uvumilivu.mfano mzuri ni mwanzirishi wa mgahawa wa KFC( Bwana Colonel Sanders,licha ya kufiwa na Baba yake akiwa mdogo,kufukuzwamara nne kazini ndani ya mwaka mmoja na kukataliwa sehemu za kazi tofauti tofauti.Alikuja kupata mafanikio makubwa akiwa mzee miaka zadi ya 65 na kuwa miongoni    mwa mabilionea duniani lakini alivumilia.Ndugu yangu ambaye bado muda unao uvumilivu unakushinda nini?                                  .



kutokubali kukata tamaa; mafanio yoyote  yanakuja na chanamoto vikwazo vya hapa na pale ukiyumbishwa na chanagmoto hizo utajikuta unaishia kuyatazama kwa majirani . bwana Colonel  angeweza kukata tamaa na kuishia kulamika mgahawa wa KFC ambao ni maarufu kwa kuuza chips  sidhsni kama tungekuwa tunaisikia,na kwa sasa imeenea nchi zaidi  ya 
 ya 80 na matawi zaidi ya 9000.

                                                 


Ndugu kaza kamba usiyumbishwe na changamoto unazokutana nazo.
 "Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Nakusihi uendelee kfatria blogu hii ya DARAJA LA MAFANIKIO HAKIKA TUTAFIKA
for more maarifarobert@gmail.com
instagram @lackiusrobert.
KARIBU SANA.