Monday, March 16, 2020

UCHAMBUZI WA KITABU CHA RICH DAD POOR DAD ROBERT KIYOSAKI



KITABU KINAITWA, RICH DAD AND POOR DAD, What the Rich teach their kids about money -that the Poor and  middle class do not!.( Baba tajiri baba maskini ,Jinsi matajiri wanavyofundisha watoto wao kuhusu Pesa ,kitu ambacho watu maskini na watu wa kipato cha kati hawafanyi.)

 MWANDISHI : ROBERT KIYOSAKI
MCHAMBUZI : LACKIUS ROBERT

Rich dad and Poor dad, Ni stori inayomhusu mwandishi Robert Kiyosaki aliyekuwa akiishi huko Hawaii akiwa na baba wawili yaani baba maskini (baba mzazi) na baba tajiri (asiye mzazi wake ).Baba maskini aliyekuwa mwajiriwa mwenye elimu ya juu na ajira kubwa pia baba tajiri aliyekuwa na elimu ndogo sana lakini ni mjasiriamali. Kiyosaki aliamua kufuata hatua za baba tajiri.

Lengo kuu la kitabu hiki ni kutoa ushauri na elimu ya uchumi ambayo Kiyosaki aliipata kutoka kwa baba tajiri.Anawafananisha na kuwatofautisha baba hawa kwa kuangalia ufanyaji wa kazi wao kwa bidii, kuelimika, kuwekeza, na namna ya kutafuta pesa.

UTANGULIZI:
Kuna huhitaji mkubwa wa watu kujua hili,
Mwandishi anaanza kwa kuuliza je shule zinawaandaa watoto kielimu kulingana na dunia ya leo?.
Wazazi wangu  waliniambia kuwa nenda shule soma sana pata alama nzuri upate kazi nzuri yenye manufaa.Malengo yao makubwa yalikuwa ni kutupa elimu nzuri ya chuo  mimi na dada yangu.Mwaka 1976 nilimaliza diploma na kuajiriwa kama mhasibu katika kiwanda kimoja.Mimi pamoja na Michael tulikuwa tukifanya kazi na kupandishwa vyeo mara kadhaa lakini kuongezeka kwa  mafao yetu yote kumekuwa kunategemea mchango wetu.Tumejaliwa kupata watoto watatu na wote tumewapa elimu nzuri.Siku moja mtoto wetu alikuja akiwa anaonekana kuboreka na shule akatuuliza hivi ‘’nimechoka kusoma masomo ambayo sitayafanyia kazi maishani mwangu’’. Bila kufikiria nikamjibu usipopata alama nzuri autaenda chuo, akaniuliza je nisipoenda chuo sitokuwa tajiri,nikamjibu usipoenda chuo autapata kazi na usipopata kazi autapata utajiri.
Watoto wengi siku hizi wanakuwa na kadi za benki hata kabla hawajaenda shule,pia wapo wafanyakazi wengi  wahasibu,wanasheria lakini bado hawana elimu ya msingi wa fedha na  hii ni kwa sababu shule zetu zinatufundisha kusoma kwa bidii,kupata alama nzuri,kwenda chuo na kupata kazi nzuri yenye mafao sio zaidi ya hapo.

Utangulizi unaishia hapo karibu uchangie.Kesho tunaenda sehemu ya kwanza.
 Baada kumaliza utangulizi hii ni sehemu ya kwanza.

Rich dad poor dad
 (BABA TAJIRI NA BABA MASIKINI),Katika sura hii anajaribu kuwaelezea vizuri baba wawili alionao ,naomba usome vizuri sehemu hii maana imebeba maana kubwa katika dhana nzima ya jinsi baba tajiri anavyofundisha watoto wake kuhusu fedha,na baba maskini anavyofundisha watoto wake kuhusu fedha.


Nina baba wawili mmoja masikini na mwingine tajiri.Mmoja amefanikiwa kusoma katika vyuo mbali mbali kama vile Stanfordbridge na vinginevyo pia ana elimu ya uzamili (PhD) mwingine hata darasa la nane hajamaliza.
Wote wamefanikiwa katika maeneo yao wapambanaji ,Wako vizuri wakalimu ,walinipa ushauri, lakini wa kitofauti mmoja anasema kupenda pesa ni chanzo cha maovu mwingine anasema ukosefu wa fedha ni chanzo cha maovu.Kuwa na wazazi wawili wenye ushauri huu wananitatiza kidogo.

Maana nawaza nichukue upi niache upi wamenifanya nikae nawaza kila wakati. Nimekuja kugundua kwamba sababu kubwa inayopelekea matajiri kuendelea kuwa matajiri ,wenye kipato cha kati kubakia pale pale na masikini kuendelea kuwa  maskini ni kwamba somo la elimu ya fedha linafundishwa nyumbani tu  sio shuleni.
Shuleni tunafundishwa kusoma na kufaulu zaidi baade kutafuta kazi mfano ukiwaangalia madaktari  ,wahasibu, wafanyakazi wa benki shuleni wamefauru vizuri lakini wanaagaika kupata pesa za kujikimu kwenye maisha yao.
Baba maskini  anasema soma sana utafute kampuni ukafanye kazi  ,Baba tajiri   anasema soma sana utafute kampuni ya kununua uwaajiri watu .Tena mwingine anasema sababu inayonifanya kuwa maskini ni kwa sababu niko na wewe mtoto ,mwingine anasema ninapaswa kuwa tajiri kwa sababu niko na wewe mtoto.

Naomba kuishia hapo unaweza kupata uchambuzi huu kutumia namba 0767702659
Lackius Robert karibu sana

No comments:

Post a Comment